CCM wala Mutungi hawahusiki na Lipumba,UKAWA acheni upotoshaji

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,449
Kumekuwa na lawama zisizokuwa na maana kabisa kuhusu sakata la Lipumba na CUF, wanatudanganya kwamba eti Lipumba anapewa hela na CCM na Mutungi pia kalipwa na CCM, hawa viongozi wa UKAWA wanatufanya sisi ni wajinga sana,

kila kitu wanaisingizia CCM hivi ni kwa nini?wakishindwa uchaguzi wowote visingizio ni CCM,wakigombana kwenye vyama visingizio ni CCM,yaani kila wanachofeli basi kisingizio ni CCM.

Sasa kwa mfano sakata la Lipumba hivi kama CUF wangeisaini ile barua ya Lipumba ya kujiuzulu je haya mambo si yasingekwepo? Halafu nasema si CCM wala MUTUNGI wanaompa kiburi Lipumba kwa sababu ukiangalia kwenye mikutano yake Lipumba bado anakuwa na watu kibao(wafuasi),

Hiyo maana yake ni kwamba Lipumba ana wafuasi na ndio maana anajenga jeuri,we unadhani kama asingekuwa na wafuasi angepata wapi jeuri? Angemuongoza nani wakati wanachama wote hawamtaki?

Kwa hiyo mambo mengine CCM inasingiziwa jamani khaaaa
 
Nadhani wamekutuma uje uwasomee nyota,
Kawaambie wamesema hakuna wasichokijua.
 
kama kusoma na kuandika hujui,hata picha huoni?..basi huo ni upofu wa macho na fikra..
 
Back
Top Bottom