CCM wakunjana wakitibu makovu ya Lowassa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Lowassa-10March2016.png

Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Katika kile kinachoonekana kuendelea kusumbuliwa na kivuli cha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, vikao vya CCM vya kutahmini sababu zilizofanya wapoteze baadhi ya majimbo, vimeingia dosari mkoani Mara kwa makada wa chama hicho kunusurika kupigana wakituhumiana kuisaidia upinzani wakati wa uchaguzi mkuu.


Lowassa alijiondoa CCM Julai 28, mwaka jana, na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Agosti 4,mwaka huo, mwanasiasa huyo mkongwe aliteuliwa kuwania urais akiungwa mkono na vyama vinne vilivyounda Umoja wa katiba ya Wananchi (Ukawa) na kuwa mshindi wa pili huku upinzani ukiwa na wabunge takribani 110 na zaidi ya halmashauri 25, idadi ambayo haijawi kufikiwa na vyama vyama vya upinzani tangu nchi ipate uhuru.

Taarifa ambazo gazeti hili ilizipata jana, zilisema makada wa chama hicho mkoani Mara, nusura wapigane wakiwa kwenye kikao kilichokuwa kinalenga kuangalia sababu ya kupoteza majimbo ya Bunda, Tarime Vijijini, Tarime Mjini na Serengeti.

Katika kikao hicho kilichofanyika Bunda, habari zinasema,vurugu zilianza baada ya baadhi ya viongozi kutaka kumtoa nje ya kikao Katibu Mwenezi wa CCM wa Wilaya, Ezekiel Sariro, kutokana na kurekodi kilichokuwa kinachoendelea kwenye kikao ili apeleke kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Stephen Wasira.

Sariro aliiambia Nipashe kuwa baada ya kutakiwa kuzima simu yake, awali aligoma kwa madai kuwa yeye hata kurekodi hawezi.

Alisema baada ya mvutano, viongozi wa mkoa waliokuwa wakiendesha kikao hicho, walimvuta na kutaka kumnyang’anya simu yake, ndipo alipokubali kuizima.

Sariro alisema Katibu wa Mkoa, Adam Ngalawa; Mwenyekiti wake, Christopher Sanya na Mwenyekiti wa Wilaya ya Bunda, Mwita Chacha, walifanya kitendo hicho kwa sababu walijua anataka kufichua walivyosaidia Ukawa kwenye uchaguzi mkuu.

Hata hivyo, walikana kumuunga mkono Lowassa na Ukawa kwa ujumla kwenye uchaguzi huo na badala yake wanaamini kinachoendelea sasa ni propaganda zenye mwelekeo wa kuwapaka tope.

Ngalawa kwa upande wake alisema ushiriki wake na Mwenyekiti Sanya, ulilenga kuzuia vurugu ambazo zingetokea kutokana na kutoelewana kwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Bunda na Katibu Mwenezi wake.

Naye Chacha anayetajwa kuwa mshirika wa viongozi hao wa mkoa, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa ‘washirika’ hao ndio walioitisha kikao hicho ili kuandaa taarifa itakayowasilishwa Makao Makuu ya CCM.

Chacha na Ngalawa kwa nyakati tofauti walisema kushindwa kwa CCM katika jimbo la Bunda kulitokana na kasoro za aliyekuwa mgombea ubunge wao, Stephen Wasira.

Wakati Chacha akisema Wasira alishindwa kutekelezwa ahadi kwa vipindi vya awali vya ubunge wake, Ngalawa alisema pamoja na mambo mengine, mwanasiasa huyo mkongwe hakuushirikisha uongozi wa wilaya, badala yake aliteua watu wachache hivyo kukosa fursa ya kupata mbinu za ushindi.

Viongozi hao walizielekeza shutuma zao kwa Sariro kwamba alikuwa mpambe wa karibu wa Wasira, hivyo kusababisha asikutane na viongozi na wanachama wengine.

Naye Sanya alisema kushindwa kwa CCM kwenye majimbo hayo, likiwamo Bunda, kulitokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza kwa kamati za ushindi za wilaya ambazo hata hivyo hazikuwa na ushirikiano.

Pia alisema baadhi ya wagombea wa CCM waliunda kamati zao binafsi zilizokuwa nje ya mfumo wa chama, hivyo kusababisha kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo, Wasira alikanusha madai hayo na kusema kabla na wakati wa kampeni, alishirikiana na sekretarieti ya CCM wilayani Bunda isipokuwa Mwenyekiti wake, Chacha anayemtaja kuwa miongoni mwa waliokisaliti chama hicho.

Licha ya Chacha kukanusha madai hayo, Wasira alisema kwa kushirikiana na wajumbe wa sekretarieti hiyo (isipokuwa Mwenyekiti), waliwafikia viongozi katika ngazi za mashina, matawi, kata na jimbo.


“Huyo jamaa (Chacha) na viongozi wa mkoa ajenda yao ilikuwa moja tu, kuhakikisha kwamba wanasaidia CCM ishindwe, hakuna jambo jingine,” alisema Wasira wakati akijibu madai dhidi yake.

Akizungumzia kushindwa kwa CCM kwenye majimbo ya Tarime Mjini, Tarime Vijijini na Serengeti, Ngalawa alisema kulitokana na ukabila. Hata hivyo, uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa wagombea wote wa maeneo hayo walikuwa kutoka kabila la Wakurya.

Nape ageuka mbogu

Gazeti hili lilipomtafuta Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, ili kujua kwamba kufanya tathimini kujua sababu za kupoteza baadhi ya majimbo ni jambo linalofanyika nchi nzima na jinsi utaratibu wake ulivyo, alitaka mwandishi aandike maswali kwenye simu ili amjibu kwa maelezo kwamba yupo kwenye kikao.

Baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu yake ya kiganjwani, hakujibu na ndipo baada ya muda alipopigiwa tena alisema: “sijakiri wala sijakataa kama tumeagiza, nasema kaulizeni kwenye ngazi husika.

“Shida moja na hili lipo Nipashe na (gazeti lingine la kila siku analitaja jina) na mimi samahani kwa kukwambia hili, kama vile ni ajenda za kutokea wakati wa uchaguzi ambazo nyinyi mmezibeba sana, hili suala wewe mwenyewe umekiri limetokea katika wilaya na mkoa kwa nini msiwaulize wao wajibu.

“Mimi ni msemaji wa taifa, kama kuna shida ya utekelezaji ulizeni ngazi iliyofikia. Mimi sijaingia kwenye hivyo vikao, ninachojua si kila mahali vikao vimefanyika, ninyi mnataka kuwasaidia Ukawa kuwa na ajenda ya kuwasema CCM.

“Sasa hivi nipo Lindi, nikizungumza ni kama vile ni jambo limetokea nchi zima wakati si kweli na nimewajibu jana (anataja jina la gazeti jingine) wakaacha kuandika. Nilijua limetoka (anarudia kutaja jina la gazeti hilo) litakuja Nipashe na kwenda (anataja gazeti jingine la kila siku),” alisema Nape.

Baada ya maelezo hayo, Nape alisema: “Mwaambie wenzako kuwa uchaguzi umeshaisha na hata kama hamkubali CCM imeshinda na watatawala miaka mitano.

“Nyinyi mkiendelea kutumiwa kubeba ajenda ambazo hazina maana wala msingi na nimeshalisema sana hili. Kama kuna tatizo katika kikao chochote, mnatakiwa kutaja maeneo mahususi si kujumuisha maeneo yote,” alisema.

Alisema kila ngazi ya chama kuna msemaji wake na kama ni Mkoa wa Mara tukio lilipotokea, waulizwe wao.

“Mnachotaka kufanya ni kuifanya story (habari) iwe juu na ili iwe juu ni kumwuliza Nape, CCM ina Katibu Mwenezi Wilaya na Mkoa, ikishafikia ngazi ya taifa nitajibu, msilichokonoe, hili zoezi umenielewa?

‘’Nchi hii haiwezi kuendeshwa kila siku na siasa tu, mbona yapo mambo mengi ya kulifanya taifa hili lisonge mbele, kwa sababu wamekosa ajenda basi wanatafuta uchafu wa kufagia na smenti, natumaini story hamtaiandika vibaya, (anataja jina la gazeti lililofutwa) niliwaambia mkienda huku mimi nawafungia wakasema Nape anasema tu, sasa hivi mimi Waziri na Katibu Mwenezi wa chama be careful (kuwa mwangalifu),” alisema.

Aliongeza kuwa: “Mara yenyewe mimi ni mlezi wa Mara, kuna mahali wamekaa pale Rorya wakafukuzana, waulizeni ni hii ni stori ndogo sana ila mnataka kuikuza mnaniuliza mimi, mtu anayekwambia tumeagizwa si unamwambie awape ushahidi, kwa nini mnakimbilia kwangu, mchezo wa waandishi naujua, mnataka Nape azungumze ili story iwe kubwa,” alisema.


Chanzo: Nipashe
 

Attachments

  • IMG-20160310-WA0002.jpg
    IMG-20160310-WA0002.jpg
    45.2 KB · Views: 35
hivi bado wapo dunia hii.

kusanyiko la opportunists. nilidhani walikuwa wanamsaidia rais kutumbua majipu chamani au hilo halipo kwenye ilani.
 
Jamaa kukikucha tu anawaza CCM, hongera sana kwa kuiwaza CCM kuliko hao wana CCM.
 
Back
Top Bottom