CCM wakubaliana kutua 'mizigo'

tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,565
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,565 2,000
Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mikoa mbalimbali nchini, wametoa tamko la kuwataka mawaziri na viongozi wote wa serikali waliotakiwa kuripoti mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho, kufanya hivyo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tamko hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na wenyeviti hao kupitia viongozi wao, wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kuunga mkono jitihada zilizoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na sekretarieti ya chama hicho.

“Viongozi na watendaji wengine wote wa serikali walioonyesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ambao walipewa wito wa kuhudhuria mbele ya Kamati Kuu ya CCM, wachukuliwe hatua zinazostahili,” alisema Mgana Msindai, ambaye ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Mikoa nchini na kuongeza:

“Tunawakumbusha viongozi wa serikali watambue kuwa Chama Cha Mapinduzi, kinaisimamia serikali kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015, sura ya tisa. Tunaitaka serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha udhaifu huo.”

Msindai alisema Kinana amekuwa akikemea kwa nguvu zote udhaifu mbalimbali ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali kama vile ubadhirifu wa mali za umma na utekelezaji duni wa miradi ya maendeleo.

Wenyeviti hao walisema wanamuunga mkono Kinana na sekretarieti ya CCM kwa msimamo huo, kwani tangu alipopewa wadhifa huo wa Ukatibu Mkuu, ameonyesha uwajibikaji mkubwa ambao umekiwezesha chama hicho kupata uhai mpya na kuamsha ari na matumaini kwa Watanzania.

Wenyeviti hao pia waliwataka viongozi wote ndani ya chama hicho ambao hawatekelezi majukumu yao kikamilifu kwamba bora waondoke na wawachie Chama chao.

Akiwa katika mikutano ya hadhara katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, wakati wa ziara kwa ajili ya kukiimarisha Chama na kuangalia iwapo ahadi za chama hicho kwa Watanzania zimetekelezwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alisema Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima, wameshindwa kazi na kumtaka Rais Jakaya Kikwete, awashughulikie.

Katika orodha hiyo pia yumo Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, ambaye Kinana alisema mawaziri hao wataitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM, ili wahojiwe juu ya utendaji wao wa kazi na utekelezaji wao wa majukumu kwa Watanzania.

Taarifa zinaeleza kuwa leo Sekretarieti ya CCM inakutana kuandaa ajenda za kikao cha Kamati Kuu kitakachokaa kuanzia kesho mjini Dodoma.

SOURCE: NIPASHE
 
amakyasya

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Messages
3,463
Points
0
amakyasya

amakyasya

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2013
3,463 0
chama chakavu = mawaziri chakavu(mizigo)= utendaji chakavu= ccm
 
M

mbezisa

Senior Member
Joined
Dec 31, 2012
Messages
131
Points
0
M

mbezisa

Senior Member
Joined Dec 31, 2012
131 0
Ingekuwa chadema tungeambiwa wanaotaka kuwajibishwa si wachaga, ni kwasababu ya ubaguzi wa udini na ukabila! Je kwa upande wa ccm tusemeje? Karibu mkuu geti 6 na kundi lako.
 
Ivonya-Ngia

Ivonya-Ngia

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Messages
704
Points
195
Ivonya-Ngia

Ivonya-Ngia

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2009
704 195
Haya mambo ni kukorogana sasa.

Sielewi inashindikana vipi Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua hao mawaziri kama rais na mteuzi wao halafu tunaaminishana kuwa mamlaka hayo yatafanyika kwenye CC ya CCM? Ni yupi Jakaya mwenye nguvu za kimamlaka? Rais wa serikali ya JMT ama mwenyekiti wa CC ya CCM?

Hawezi kuwahoji na kuwawajibisha ministers kama rais nchi na kiongozi wa serikali bali anauwezo huo kama mwenyekiti wa CCM ndani ya CC, kweli???

Hizi ni hekaya za nani amfunge paka kengele, unafki wa hali ya juu!
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,565
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,565 2,000
halafu kwenye uzi wa maana kama huu huwezi kuwasikia Lumumba buku 7 (LBK 7) wakichangia, lakini linapokuja suala la zitto utaona jinsi wanavyokomaa nalo.
 
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2013
Messages
22,549
Points
2,000
N

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2013
22,549 2,000
Ni maajabu ya dunia, mawaziri wanawajibishwa na Kamati kuu ya ccm badala ya rais wa nchi, je kazi ya rais ni nini?
 
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Messages
15,565
Points
2,000
tpaul

tpaul

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2008
15,565 2,000
Baada ya mizigo mikubwa kutuliwa, imebaki mizigo hii ya kinana. Kawambwa, chiza, malima, ghasia, mwanri na mgimwa mnasubiri nini kuachia ngazi? au mnasubiri mfukuzwe kwa aibu?
 
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
8,185
Points
1,250
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
8,185 1,250
Naona mawaziri mizigo imekuwa nyepesi kuliko la gamba
 

Forum statistics

Threads 1,324,624
Members 508,740
Posts 32,168,262
Top