CCM wakomba hela Hazina, mishahara ya Septemba hamna!

Tunasubiria EPA nyingine kwa style ya tofautie..Inabidi Prof Ndullu aangalie tusijemhamisha nchi..haya mambo ya siasa yasikie tu ila yakikujeuka utajuta kuwa kwenye gemu..

Sababu moja wapo ya kumuondoa Dr. Bukuku pale Bot na kumleta yule mama asiyejua lolote juu ya banking ni kuweka mambo sawa ili wakati ukifika iwe rahisi kuchota fedha a' la EPA; kwani Dr. Bukuku alikuwa kama vile alikuwa anawawekea kiwingu!! Baba ya yule mama ni rafiki ya mkweree na ndio maana nae pia ameula kwenye tume ya katiba; ni muendelezo wa kupendeleana na kulindana kwa kwenda mbele!! ccm oyeeeeeeeeeeeee!!!!!!!
 
kukosekana mshahara ni kweli,lakini eti zimechotwa na ccm ni propaganda za chadema kujipa umaarufu tu kwa kila baya kuitupia chadema
 
kukosekana mshahara ni kweli,lakini eti zimechotwa na ccm ni propaganda za chadema kujipa umaarufu tu kwa kila baya kuitupia ccm
 
kukosekana mshahara ni kweli,lakini eti zimechotwa na ccm ni propaganda za chadema kujipa umaarufu tu kwa kila baya kuitupia ccm

Watanzania walishakunywa maji ya bendera ya jembe na nyundo hawaelewi kitu kwa ccm.Leo hata kuendesha ,magari imeshindikana hata foleni haipo tena kumbe mijitu ya serikalini haijapata mishahara halafu yakilipwa tu yanakaa kwenye keyboard na kuanza kusifia LOWASSA.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Tunataka chanzo cha habari hii. Vinginevyo uzi wa siasa unaanza kuvamiwa na udaku taratibu
 
Nilikuwa UD naimeona barua ya Prof Mgaya akiwataarifu wafanyakazi kuwa chuo kimepokea cheque so pesa inanukia.
 
kukosekana mshahara ni kweli,lakini eti zimechotwa na ccm ni propaganda za chadema kujipa umaarufu tu kwa kila baya kuitupia chadema
Sasa hapo unataka kusema nini? Umejuaje kwamba mleta hoja ni Chadema? Lipeni mishahara ya watu msilete ujanja ujanja wa kwenda kukopa huko halafu mnataka watu wakae kimya? Mlengo wa Kati?
 
Last edited by a moderator:
We unadhani kukodi macoster na kuwalipa kuwalisha, kuwalaza wakereketwa na kuwapeleka arusha ni pesa ndogo!!!!

Kumbuka kila kitu kwa ccm kinanunuliwa.
 
Mimi ni mfanyakazi wa serikali kuu na mshahara unakalibia kuisha sasa hivi toka niuchukue! Jamani hizi habari bora JF waanzishe jukwaa la udaku na umbea/propaganda kuliko kutufanya watu wazima watoto.

"Kuna watu wanamiliki viwanda vya kuzalisha uongo" by JK.
 
Inawezekana kweli maana mpaka sasa mishahara wafanyakazi wa serikali kuu wengi hawajapata mishahara, eti wanadai ni system mpya inayotumika hazina ndio inachelewesha.

Mkuu Katavi,

1. System mpya wanayosema ni ipi? LAWSON au nini kingine?
2. Mpaka juzi, UDSM Hawakuwa wamelipwa mshahara. Na hii si mara ya kwanza kwao kupatwa na tatizo hilo. Huwa (wafanyakazi wa UDSM) husema kuwa wanapokeaga mshahara tarehe 37!

This is too bad kwa nchi ambayo nimesikia imekuwa uchumi kwa 6% . Mwaka jana nasikia ulikuwa kwa 5%. (Sijui chochote kuhusu UCHUMI, labda 1st class economist kwa kuwa yuko humu atasaidia)
 
Aisee! Kumbe ndiyo maana hata foleni zimepungua barabarani.
 
sasa huo utakuwa urafi, nasikia walipandisha bei ya mafuta kwa Shs 100, tena wamechukua na mishahara?
 
Kwa habari za
uhakika, kutoka chanzo cha uhakika ni kwamba mkutano wa CCM Dodoma na
chaguzi zinazoendelea ndani ya chama vinanendeshwa kwa mamil ya pesa
zilizochotwa Hazina.

Pesa hizo ambazo nyingi zilikuwa za mishahara ya wafanyakazi wa serikali
na mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini zimesababisha mpaka leo
wafanyakazi kadhaa hawajapata mishahara ya Septemba, na "boom" la
wanafunzi linapigwa danadana.

Hivi jamani,pesa za serikali toka lini zikawekwa ktk account ya CCM? hebu muwe mnaleta habari zenye ushuhuda thabiti.
 
Chama chetu cha magamba chajenga nchi. ubwabwa aaah maharage yajenga mwili,mihogo aaah ugali wajenga mwili.
dhaifu aaah riz1 wajenga nchi.


Daaa JF kweli ni raha sanaaa mtu huwezi kuacha kufurahi humu.......
 
Back
Top Bottom