CCM wakiri kukosa matokeo waliyotarajia uchaguzi wa marudio Kinondoni

SAMMY DANNY

Member
Jan 10, 2012
24
6
Mwaka 2015 Mtulia alipata kura 70,337 huku Idd Azan akipata kura 65,964. Idadi hii ya kura inatengeneza jumla ya wapiga kura wa Chadema na CCM 136,301.

Jana (JUMAmosi) Mtulia kapata kura 30,247 hata nusu ya Kura alizopata 2015 hazijafikia. Huku Salum Mwalimu akiambulia kura 12,353. Jumla ya kura zao hazijafikia kura za 2015.

Tafsiri.

1.Mtulia kapoteza watu 40,090 Chukua kura zikizopigwa 2015 kura 70,337 toa kura alizopata jana (jumamosi) 30,247 utaona kadondosha watu wengi 40,090 ambao wanazidi idadi ya waliomchagua jana.

2. Hata wale waliomchagua Idd Azan mwaka 2015 wengine wameshahama au kuachana na siasa. Chukua kura alizopata Idd Azan 2015 toa kura alizopata mtulia jana utapata kura 35,717. Hawa wanazidi tena kura za Mtulia za Jana.

3. Ukichukua kura 35,717 ambazo zilimchagua Idd Azan lakini jana hawakupiga kura ukijumrisha zile ambazo Mtulia amezidondosha 40,090 utapata kura 75,807 ambazo zipo nje ya Mtulia.

Hizi ndizo zilizotulaza nje na viongozi wetu kuhama maofisini kwenda kupiga kambi kule Siha na kwingineko (Kinondoni). Kwa maana rahisi kabisa input ya nguvu tuliyoiweka haiendani na output tuliyoipata.

Toka mwaka 2015 mpaka leo 2018 kuna makundi mengi ya vijana yamevuka kuja kwenye umri wa kupiga kura.

Idadi ya wapiga kura ibapoongezeka kulingana na aina ya population tuliyonayo "pyramid" kwamba vijana ni wengi kuliko wazee inatoa tafsiri chanya kwa upinzani (CHADEMA).

Hii namaanisha kuwa itategemea tumeshughuLIkia matatizo ya vijana kiasi gani hadi kufikia 2020 ambapo kutakuwa na kundi kubwa sana la vijana watakaojiandikisha kutokana na kundi hili kuathiriwa na ukuaji wa teknolojia ya habari.......

Kuna kitu wananchi hawajatuelewa.... tuna kazi kubwa bado.

Chanzo: Kada wa CCM- Ole Mushi
 
ccm wamekiri mengi tu, sio hilo pekee.! jana tu wemekiri kudedisha denti, hawa kwa sasa waendelee kuwalaghai wazee kwa kuwapiga mboyoyo!
 
UKAWA ndio umekiona cha mtema kuni uchaguzi wa kinondoni
Mgombea wa Ubunge wa UKAWA Kinondoni 2015 alipata kura elfu 70, mgombea wa UKAWA kinondoni uchaguzi huu wa juzi Salum mwalimu kapata kura elfu 12,pungufu ya kura elfu 58 ukilinganisha na za uchaguzi wa 2015
 
Daa, huwa nikionaga Comment zako na jina lako haviendani, Means unawakili UPUMBAVU, nadhani wengi humu hukuona USIYEJITAMBUA, aise Siku utakapo shikwa sehemu nyeti ndio utatambua haya watu wayasemayo. Huwa Unajitoa ufahamu kabisa kwa jambo lililo wazi. Angalau kada Mwenzio Ole Mushi kaongea facts na Future ya haya yanayoendelea na kaendakwa statistics na kuonesha nguvu na rasilimali kubwa iliyotumika kwa chaguzi hizi Siha na Kinondoni V/S kura zilizopatikana, Daa anyway wahi Buku 7 yako tuu pale ukanywe chai

UKAWA ndio umekiona cha mtema kuni uchaguzi wa kinondoni
Mgombea wa Ubunge wa UKAWA Kinondoni 2015 alipata kura elfu 70, mgombea wa UKAWA kinondoni uchaguzi huu wa juzi Salum mwalimu kapata kura elfu 12,pungufu ya kura elfu 58 ukilinganisha na za uchaguzi wa 2015
 
Back
Top Bottom