CCM Wakiniua Mnizike Kenya

Ufunuo wa Yohana

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
318
67
ANGALIA JINSI MUNISHI ANAVYOPAMBANA NA CCM!!
"CCM Wakiniua, Mnizike Kenya." Asema Munishi. "Siyo kwamba nimebadili uraia, wala sitarajii kufanya hivyo.Mimi bado ni Mtanzania. Sikuchagua kuzaliwa Tanzania, lakini nitachagua pa kuzikwa.Serikali za CCM zimenifanya nisiwe na mahali ninapoweza kupaita nyumbani ndani ya nchi yangu. Kosa langu ni kusema CCM sera zake zimeiharibu Tanzania, na hawafai kuwa madarakani.Makachero wa Tanzania wamekuwa wakitumia kila mbinu chafu kuwasumbua na hata kuwaua wote walio na uhusiano wa karibu na Munishi. Ajabu ni kwamba Munishi mwenyewe akienda Tanzania wanafuatilia nyendo zake bila kutishia kumuua. Akiwa Kenya ambako ndipo sanaa yake ilimpatia uwezo wa kununua nusu ekari ambapo amejenga nyumba ya mabati kujisitiri na jamii yake, bado makachero hawaishi kumvamia kama majambazi, na kutishia kumuua. Munishi akiwaeleza wanahabari kwamba wavamizi walidai kutumwa, wao wanaandika kwamba ni majambazi wa kawaida. Walijuaje kama ni majambazi wa kawaida? Tena wangejuaje kwamba siyo majambazi wa kawaida? Basi kwa nini waandike ni majambazi wa kawaida? Mbaya zaidi wanasema Munishi ndiye aliyewaambia wakati sivyo. Mtu akikuuliza je! unaona waliokuvamia kama ni washindani wako kibiashara? Na jibu likawa ni vigumu kujua kwa hakika wavamizi wangu ni kina nani, Lakini walidai kutumwa na watu ambao hawakuwataja. Je hapo utakuwa umesema kwamba majambazi hawakuwa washindani wangu kibiashara bali ni wa kawaida? NATION wanapaswa mara moja kumjibu Munishi kwani mahojiano aliyanakili kwenye simu yake
Serikali ya Mkapa Tanzania inaamini kwamba Munishi na nyimbo zake ni mwanzo wa kuvurugika kwa amani Tanzania. Kinyume chake ndio sahihi. Amani ilivurugika pale Mkapa alipowaamuru Polisi wawaue Wazanzibari zaidi ya 70 kwa sababu za kisiasa. Majeshi Tanzania walikasirishwa sana na jambo hilo,na walikuwa tayari kuipindua serikali ya Mkapa. Munishi akaimba wimbo "MPENDE ADUI YAKO", Mkapa badala ajue kwamba wimbo huo ulikuwa ukimsaidia yeye ili serikali yake isipinduliwe na kisha afunguliwe mashitaka ya kuwaua raia wasio na hatia, Aliupiga marufuku wimbo huo na kuamuru polisi wamsake Munishi. Iko siku Mkapa atamkumbuka Munishi. Ngoja kipindi chake cha urais kimalizike, na tunaomba kimalizike salama, halafu Mkapa awe raia wa kawaida. Kombe aliyemwamuru amsake Munishi, ndiye atakayeamriwa amtie Mkapa mbaroni ili ajibu mashitaka ya kuua na kupora mali ya umma pamoja na kuiuza nchi kwa makaburu
 
Mchungaji Faustin Munishi amesema hakuna Uchaguzi Tanzania bila Katiba mpya. Akiongea katika Gospel GTV Pastor Munishi alivitaka vyama vya upinzani Tanzania kuususia uchaguzi kwani CCM wakitumia katiba ya sasa wameumaliza upinzani Tanzania. Kwa sasa ni sawa na hakuna upinzani. Kuingia kwenye uchaguzi ambao CCM hawaruhusu wengine waseme, ni sawa na kuwafunga vifaranga wa kuku na kuwashindanisha na mwewe. Matokeo mnayajua. CCM wanajua walichofanya Tanzania kwa miaka zaidi ya arobaini, ndiyo maana wananunua kila mtu. Pesa zilizo haki ya mikoa kimaendeleo, zinatumika kuinunua mikoa iiunge mkono CCM. Alisema lazima Katiba ibadilishwe kuwaruhusu wagombea binafsi ndipo upinzani wa kweli utakapoonekana Tanzania. Alielezea nia yake ya kugombea Urais Tanzania bila chama cha kisiasa. Mchungaji Munishi alisisitiza kwamba "Siasa ni uongo na hawezi kujiunga na uongo ili awatoe waongo." Alisema kwamba endapo CCM watakaidi kuibadili Katiba, basi wafuasi wake watamtangaza rasmi kuwa Rais wa Gospel Tanzania. Kwa mara ya kwanza Tanzania itakuwa na marais zaidi ya kumi. Huko ndiko tunakoelekea ikiwa CCM watawaburuza watanzania kwenye uchaguzi bila KATIBA mpya
 
Kuna fununu kwamba huyu Faustin Munishi aliwahi kuwa jambazi mbaya sana kabla ya kuokoka je wana JF ni kweli kuhusu tuhuma hizi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom