mzozaji
JF-Expert Member
- Jul 28, 2010
- 255
- 15
Kuna tetesi kuwa washabiki na wanachama wa CCM wanapanga kuandamana kulaani wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni wakati Mwenyekiti wao alipokuwa anahutubia. Hii inaonyesha wazi kuwa sasa imefikia hatua watu wanataka kukwepa hoja ya msingi ambayo ni uchakachuaji wa matokeo ya Uraisi na kutaka wanaolaani mtindo mzima wa uchakachuaji waonekane 'wabaya' wakati ni sehemu ya Demokrasia kupinga matokeo yale. Nadhani watakuwa na busara zaidi kama wakijibu hoja ya msingi kuliko kukoleza mambo kwa kuzusha mengine zaidi.