CCM wakemea ukabila na udini, wasema wanaohubiri wakamatwe mara moja

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,772
18,726
Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kwamba wanasiasa wanaojihusisha na masuala ya ukabila ,udini wanatakiwa kukamatwa mara moja

Moshi. Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia wanasiasa wanaohubiri udini na ukabila.

Shaka ameyasema hayo leo Novemba 4 wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani kata ya Bomambuzi katika Manispaa ya Moshi, na kusisitiza kuwa vipo vyama vya siasa ambavyo vinataka kuwagawa watanzania.

“Tunu kubwa ya taifa letu ni upendo na amani kwa hiyo vyombo vya ulinzi na usalama viwashughulikie wanaohubiri udini, ukabila na ukanda ili kujipatia umaarufu wa kisiasa,” amesema.

Shaka aliwaambia wananchi waliofurika katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya soko la Pasua kuwa, alisema pamoja na yote yaliyojitokeza katika mkoa huo, bado wana imani na CCM.

Katika mkoa wa Kilimanjaro, upinzani unashikilia majimbo saba kati ya tisa huku CCM kikishikilia majimbo mawili tu ya Mwanga na Same Mashariki huku upinzani pia ukishikilia Halmashauri tano.

“Pamoja na yote yaliyojitokeza katika mkoa Kilimanjaro na kata mbalimbali bado mmeonyesha imani kubwa kwa Serikali ya CCM. Nawasihi sana katika uchaguzi huu msifanye makosa,” amesisitiza.

Pia ametumia mkutano huo kuwasihi wana CCM kutowabagua wala kuwatenga wanaorudi CCM wakitokea upinzani ambapo katika mkutano huo, baadhi ya wafuasi wa Chadema walijiunga na CCM.

Kwa upande wake, Katibu wa CCM mkoa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya, amewaomba wananchi kumchagua mgombea Udiwani wa CCM, Juma Raibu akisema amejipanga vyema kuwatumikia.

Katika mkutano huo, aliyekuwa mmoja wa marafiki wa Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Fred Mushi, alipewa fursa ya kuhutubia, na kusema huko upinzani alikoenda alikutana na moto.

Mushi ambaye alikuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa Kilimanjaro kati ya 2012 hadi 2015 alipojiuzulu na kumfuata Lowassa, alirejea tena CCM wiki mbili zilizopita akisema anamuunga mkono Rais John Magufuli.


Chanzo: Mwananchi
 
waanze na boss wao coz yeye ndo kabisaa anatakiwa ahukumiwe akiwa nje ya mahakama anaongea kilugha ovyo na anaonyesha double standard hadharani refer uko mwanza eti msiwabomolee hawa walinipa kura shame
 
Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kwamba wanasiasa wanaojihusisha na masuala ya ukabila ,udini wanatakiwa kukamatwa mara moja

Moshi. Kaimu Katibu mkuu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia wanasiasa wanaohubiri udini na ukabila.

Kwa nini watu tunajitutumua sana kama bata mzinga kwa vitu ambavyo hatuna hata kauwezo kidogo navyo?? Ati vyombo vya usalama viwakamate wanohubiri ukabila na udini na ukanda! Huyu ni nani anayetaka kumfundisha mkuu?? Mwambie anyamaze kimya aache kumfundisha.
 
Waanze na yule aliyesitisha zoezi la bomoa bomoa kwa wale wasukumwasukuma-mikokoteni wenzetu! !!
 
Hawa watu wanapenda kujitekenya na kucheka wenyewe, mambo ya ukabila na udini inabidi waongee na mwenyekiti kwanza harafu ndio waje huku. Pia huyo Fredi Mushi si amerudi kwenye chama chake jamani. Mtu akitoka ccm kwenda upinzani hapo ndio amehama chama kiukweli sababu 80% ya watanzania tumekulia na ccm.
 
Nimecheka utafikiri mazuri; sijajua kama Nerway kwa wavuvi wa samaki nao wanafikiri kama Shaka wa ccm.
 
Back
Top Bottom