CCM wajumbe wengi wa NEC taifa ni watu wenye pesa na wamehonga kupata nafasi hizo, tutarajie nini huko mbeleni?

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
2,593
3,148
Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha, nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hawana kabisa ufahamu kabisa wa masuala ya siasa zaidi ya biashara,hii imepelekea wanaccm wafiia chama kushindwa kupenya.

Hii CCM ya sasa au inayoundwa na kina Kinana ni ya ubavu wa pesa.

Je, bado wananchi waweke matumaini kwa hiki chama?

Kwanini hao matajiri wasianzishe chama chao cha matajiri wanakimbilia CCM kunanini?,
Yanayoendelea ndani ya CCM kwa sasa si falsafa,itikadi na malengo ya kuanzishwa kwake

Imani yangu NEC taifa ndio injini ya nchi sasa imejaa wafanyabiashara, hatutauzwa kweli? Nchi itabakia kuwa ya wachuuzi na si wazalishaji mali.

Hata mtawala atakayepatikana kupitia hii NEC taifa atakuwa influenced na hili tabaka la wafanyabiashara kupitiaha mambo yao.

Shime wananchi watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama vyetu, ikifika 2025 tuwakatae hawa wahuni kwa gharama yoyote ile.
 
CCM inaonekana imeachana na mfumo wao wa Kikomunisti, watu wenye fedha ndio huwa Viongozi wazuri, kuliko kung'ang'ania Masikini wacheza Bao hohe hahe ambao hata kuziongoza familia zao kutoka kwenye Ufukara wa kutisha wameshindwa.

Sisi Chadema mfumo wetu ni wa Kibepari.

Mfano Rishi Sunak WM wa UK tu ni Bilionea hawezi kuiba fedha za Umma.

Mfumo wa CCM wa kuwaabudu Masikini ndio uliolifikisha Taifa hili kwenye huu mkwamo na tumetengeneza Taifa la wezi kila Maskini akitoka Kijijini anapewa wadhifa na kuanza kupora.
 
Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha,nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa ambao hawana kabisa ufahamu kabisa wa masuala ya siasa zaidi ya biashara,hii imepelekea wanaccm wafiia chama kushindwa kupenya.
Hao wafanyabiashara ndiyo wenye ufahamu wa siasa wacha kujidanganya. Wao wameshapiga mahesabu kwamba biashara zao zitakwenda vizuri zaidi wakipata connections na wabunge na watu wa serikali, sasa unataka ufahamu gani?
 
Jamaa wamerudi kwa wingi hao na safari awatorudia makosa.

Tanzania inaenda kuwa amongst the most corrupted countries in the world, nchi kama hizo uongozi wake uondolewa na mapinduzi ya kijeshi tu wakishachoka na mambo ya ovyo.

Huyu mama ameiharibu hii nchi ndani ya muda mfupi sana, hadi mafisadi yaliyotimuliwa na JK yamerudi upya.

Kaazi kweli kweli
 
Dah aseee
 
CCM inaonekana imeachana na mfumo wao wa Kikomunisti, watu wenye fedha ndio huwa Viongozi wazuri, kuliko kung'ang'ania Masikini wacheza Bao hohe hahe ambao hata kuziongoza familia zao kutoka kwenye Ufukara wa kutisha wameshindwa.

Sisi Chadema mfumo wetu ni wa Kibepari.

Mfano Rishi Sunak WM wa UK tu ni Bilionea hawezi kuiba fedha za Umma.

Mfumo wa CCM wa kuwaabudu Masikini ndio uliolifikisha Taifa hili kwenye huu mkwamo na tumetengeneza Taifa la wezi kila Maskini akitoka Kijijini anapewa wadhifa na kuanza kupora.
Kama walivyolipa lile shetani la Chato..
 
Nayasema haya si kwa kubahatisha,nimefanya uchunguzi karibu nchi nzima kujiridhisha,nafasi hizi zimejaa wengi wao matajiri na wafanyabiashara wakubwa
Hawa watakisaidia sana chama, hatutaki viongozi masikini wa kutupwa, tunataka viongozi matajiri ambao watautumia utajiri wao kuimarisha chama na kusaidia kutatua changamoto za wananchi.

Umasikini ni laana na utajiri sio dhambi!. Mkono mtupu haurambwi!. CCM ya sasa inahitaji viongozi walioshiba na walionitosheleza ili sasa wawatumikie wananchi na sio viongozi masikini hohehahe wenye njaa, ambao wakichaguliwa kazi yao ya kwanza itakuwa ni kula tuu na kushibisha njaa zao!.

P
 
CCM inaonekana imeachana na mfumo wao wa Kikomunisti, watu wenye fedha ndio huwa Viongozi wazuri, kuliko kung'ang'ania Masikini wacheza Bao hohe hahe ambao hata kuziongoza familia zao kutoka kwenye Ufukara wa kutisha wameshindwa.

Sisi Chadema mfumo wetu ni wa Kibepari.

Mfano Rishi Sunak WM wa UK tu ni Bilionea hawezi kuiba fedha za Umma.

Mfumo wa CCM wa kuwaabudu Masikini ndio uliolifikisha Taifa hili kwenye huu mkwamo na tumetengeneza Taifa la wezi kila Maskini akitoka Kijijini anapewa wadhifa na kuanza kupora.
Umejibu usichokielewa
 
Hawa watakisaidia sana chama, hatutaki viongozi masikini wa kutupwa, tunataka viongozi matajiri ambao watautumia utajiri wao kuimarisha chama na kusaidia kutatua changamoto za wananchi.

P
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa,utajiri wao so far umekusaidia nini?.

Mwisho CCM itikadi yake inasemaje?

Mwisho kabisa kwanini hao matajiri wasianzishe chama chao cha matajiri,wanakimbilia CCM kunanini?
 
Back
Top Bottom