Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Katika kile ambacho Mwanafalsafa Andrew Carnegie anakitambua kama, "Uncontrolled desire for something for nothing" viongozi wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wake kitaifa Mhe.Dr.Jakaya Kikwete wameonesha kukosa mantiki ya msimamo wao kuhusu haja ya kutambua kikatiba uwepo wa Tanganyika iliyoungana na Zanzibar mnamo mwaka tar.26.04.1964.
CCM ndicho chama pekee kilichoshindwa kutoa mwelekeo sahihi kuhusu aina ya muungano unaotakiwa kwa sasa na haja ya uwazi wa mambo yahusuyo Tanganyika.
CCM wamekuwa mstari wa mbele katika sherehe mathalani kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika ambayo wanapinga uwepo wake kinyume na ilivyopendekezwa na tume ya uundaji wa katiba mpya chini ya Mzee Sinde J.Warioba.
Mara kadhaa viongozi wa CCM akiwemo Mzee Abdallah Bulendo wamemkashifu Mzee Warioba kwa kukubali muungano wa serikali tatu ikiwamo Tanganyika.
Hoja ipo wazi, bajeti ya sherehe ya uhuru iligharamiwa na nani hali Tanganyika haina serikali?