CCM Wajiingiza Mkenge: Chadema Wawasilisha List of Shame NEC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Wajiingiza Mkenge: Chadema Wawasilisha List of Shame NEC

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kulikoni Ughaibuni, Sep 5, 2010.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 234
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Pasipo kutarajia,CCM inaweza kulazimika kuuambia umma kwanini mafisadi waliotajwa kwenye List Of Shame (orodha ya mafisadi sugu iliyowekwa wazi na Chadema viwanja vya Mwembeyanga) hawajachukuliwa hatua hadi leo.Kama ambavyo chama hicho tawala kilivyokosa umakini katika kuongoza nchi ndivyo walivyokurupuka na kuwasilisha malalamiko yao NEC wakidai "wametukanwa kwa kuitwa mafisadi".Sijui ni ulevi wa madaraka au ubabaishaji tu kiasi kwamba walisahau kuwa wote waliotajwa katika List of Shame hawajathubutu kwenda mahakamani kama walivyotishia kwa kuogopa "kuwekwa uchi zaidi".Sasa wamejipeleka mahakamani wenyewe kwa kudai tuhuma hizo ni kashfa.Utamu wa stori hii uko kwenye ukweli kwamba ukidai nimekukashifu basi unawajibika kuthibitisha tuhuma nilizotoa dhidi yako sio za kweli.Kibaya zaidi kwa mafisadi waliotajwa,CHADEMA wana ushahidi mzito dhidi ya watajwa.Patamu hapo!

  Hebu soma habari husika

  Hatimaye watajwa kwenye List of Shame wanaweza kulazimika kuuthibitishia umma kwanini wasiwe jela muda huu wanaopita huku na kule kuomba wachaguliwe tena.


  Patamu hapo!!!

  KULIKONI UGHAIBUNI: CCM Wajiingiza Mkenge: Chadema Wawasilisha List of Shame NEC
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewasilisha ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) majibu ya utetezi wake kuhusu malalamiko ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeikashifu viongozi wake waandamizi wakati wa uzinduzi wa kampeni huku kikitoa orodha ya mafisadi kama moja ushahidi kwake.

  Katika majibu hayo imo orodha ya majina 12 ya watuhumiwa wa ufisadi ambayo iliwahi kutangazwa na Chadema mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembeyenga.

  Naibu katibu wa Chadema John Mnyika jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamechukua hatua hiyo ili kuthibitisha kauli zao walizozitoa kwenye uzinduzi wa kampeni zao wiki moja iliyopita katika viwanja vya Jangwani.

  “Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chadema inaeleza wazi kuwa viongozi wote ambao walishabainisha kuhusika na tuhuma za ufiasadi na ubadhilifu wa mali ya umma ambao serikali imeshindwa kuwafikisha mahakamani, watafiishwa mahakamani ndani ya siku 180, iwapo tutaingia madarakani,” alisema Mnyika.

  Alisema watuhumiwa hao wakiwamo marais wastaafu ambao wataondolewa kinga yao na Bunge ili wafikishwe mahakamani.

  Mnyika alifafanua kuwa hatua hiyo imelenga katika kujenga uongozi bora na kuimarisha utawala wa sheria hapa nchini.

  Kuhusu kutaja orodha ya majina ya mafiasadi kwenye mkutanio huo chama hicho kilisema huo si ukiukaji wa maadili ya uchaguzi kwakuwa tuhuma hizo zipo na wahusika hadi sasa hawajachukuliwa hatua na baadhi yao wanagombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

  Alisema madai yote waliyoyatoa kwenye viwanja hivyo wana ushahidi nayo na mengi ni yale ambayo tayari waliwahi kuyaweka wazi siku za nyuma.

  Kwa sababu hiyo, Chadema iliitaka Nec kutupilia mbali malalmiko ya CCM kwa sababu waliwasilisha bila kusoma sheria za maadili.

  Source: Mwananchi
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri ingekuwa bora zaidi CCM wangeenda Mahakamani ili hati zote za ushahidi wa Marando zitoke hadharani! Hawa NEC ni CCM tu hawawezi kuanika hati hizo -- watakaa kimya tu.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,427
  Trophy Points: 280
  WaMESHAWASHIKA PABAYA TAYARI, SASA HIVI CCM WANAENDA ENDA TU. ILA JAMANI INABIDI CHADEMA IWE MAKINI ISIJE BADAE MKULU AKATUMIA KIBAKI STYLE. YAANI NINA DOUBT KUBWA SANA KUHUSU HILI.
   
 5. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo ambapo CHADEMA huwa wanakosea.

  Kuna kitu kimoja ambacho binafsi nampenda Mtikila: Anaweza kuwa yeye na chama chake hawana popularity kama CHADEMA, lakini ni maarufu sana kwa kutafuta haki yake tena bila kukoma.

  Kama CHADEMA wana ushahidi, kwa nini wasifungue kesi mahakamani? Hata kama watashindwa lakini by the time kesi inaamuliwa watakuwa wameanika uozo wote na wananchi wamejua zaidi. Wasisubiri wao ndiyo waitwe mahakamani au mpaka waingie madarakani.

  It is time for action. watumie mbinu zote: Siasa, Sheria nk.
   
 6. K

  Keil JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba mfumo wa Mahakama nao una matatizo. Mfano, wakifungua kesi leo hii, kesi hiyo inaweza isisikilizwe mpaka baada ya uchaguzi, so haiwezi kusaidia chochote.

  Kibaya zaidi, maoni ya Jaji Mkuu kwamba majukwaa ya siasa yasitumike kuongelea kesi zilizo mahakamani, nayo inazidi kutia mashaka. Marando aliongelea kesi za EPA ambazo hazijafikishwa mahakamani. Mfano akina KAGODA, akina Malegesi Law Chambers, Akina Changanyikeni na wengineo. Kuna kampuni nyingi hazijafikishwa mahakamani na ili hali serikali ina ushahidi wote. Lakini ajabu Jaji Mkuu akasema watu wasiongelee kesi zilizo mahakamani. Kwani Kikwete, Lowassa, Rostam na Mkapa wamefikishwa mahakamani? Maana hao ndio waliotajwa kuhusiana na EPA.
   
 7. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #7
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Mimi naunga mkono strategy hii ya CHADEMA kwa sababu ukiamua kufungua kesi, kuna vitu viwili utakumbana navyo, kwanza kesi dhidi ya hao vigogo itacheleweshwa na usikute ikaanza kusikilizwa in 2011, hapo uchaguzi mkuu umeshapita na pili ni kwamba kabla ya kusomwa hiyo kesi mahakama inabidi iamue endapo hao unaowashtaki wanayo kesi ya kujibu.....and we all know kwamba mahakama haiwezi kusema Kikwete au Mkapa wana kesi ya kujibu.

  Kwa hiyo kwa kuchukua hatua hii ya kujibu hoja za CCM, CHADEMA inakuwa imewaachia CCM(mafisadi 12) na NEC ndio waamue. Endapo hao mafisadi waamua kuipeleka CHADEMA (or Marando) mahakamani, then ushahidi wote utatolewa pale. Endapo NEC itaamua kum-censor Marando, again Marando+Chadema wanaweza kufikisha malalamiko yao Mahakamani ambapo Marando ataelezea kwa undani madai yake, which is something that CCM doesn't want to happen. Na endapo NEC watamwachia Marando aendelee kuhubiri kuhusu kashfa ya EPA, Kikwete na CCM yake wataendela kuwa kwenye wakati mgumu.

  All in all, CCM wameminywa pabaja.
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280

  Hapo dawa ni kuwasema hadi wawo wenyewe wajue walikula vya kuiba, wamewadanganya watz na wanawaibia watz. Hivyo ni vema kuwasema majukwaani kama wanaweza wajisafishe. wasiwasi wangu, ni mpangilio wa Chadema kupiga kampeni, ningependa wawe wanashambulia zaidi, na kujihami zaidi. Mfano wanaweza kuanza kutuma majeshi kabla ya Dr Slaa kuingia sehemu husika. Wanaotangulia wakatema cheche kwanza harafu ndo mkuu Mh. Rais mtarajiwa anaingia naye kumalizia kazi.
   
 9. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Keil na Texter;

  List of Shame haikutoka mwaka huu, ina miaka mingi toka itolewe pale Mwembeyanga. CHADEMA wangeanza nalo wakati huo, wangefika mbali.

  Mtikila alipoanza na hoja ya mgombea binafsi, ilikuwa kitambo, lakini haki ilitolewa ingawa baadaye Mahakama ya rufaa ilikuja kutengua. Kutengua kwa Mahakama ya rufaa kumeongeza moto mwingine wa madai ya katiba mpya kwani sasa watake wasitake mahakama imelirudisha suala hili bungeni.

  List of Shame ingefika mahakamani, si lazima CHADEMA wangeshinda, lakini jumuiya ya kimataifa ingeweza kuona uozo uliopo kulikoni sasa hivi ambapo suala hili linachukuliwa kisiasa zaidi.

  Ukimwambia Mtanzania leo hii JK ni fisadi, nani atakuelewa ukiacha wachache ambao wana access na information na kiu ya haki?

  Katika kipindi hiki, nakubaliana inaweza ikawa ni mbinu mwafaka.

  Ikiamua inaweza ikaanza kuchapisha tuhuma hizo kwa uzito katika vyombo vya habari moja baada ya nyingine. Hii itasaidia watanzania kukumbuka maana wengi husahau mapema.
   
 10. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Jamani naomba tusiwe mbumbumbu wa sheria. Mwenye mamlaka ya kisheria ya kufungua kesi za jinai ni fereshi na si chadema ndo maana chadema wanasema kwa wananchi wajue uozo huu. chadena kama chedema haiwezi kuzifungua kesi hizo mahakamani! au nimekusoa? huo ndo uelewa wangu.
   
 11. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unaongea the other way. Wenye wajibu kupeleka mafisadi kahamakamani ni serikali ambayo inakata kodi aetu kwa ajili ya kazi hiyo; chadema wako sawa maana hiyo itakuwa sio siasa tena bali kujipima sheria kitu ambacho kina impact kisiasa;chadema haitaki kesi ila inataka serikali yoyote makini ipeleke watruhumiwa mahakamani haki itendeke kwa watanzania wote

  Mnyika kiboko anaweza kusimamia mambo kweli maana ni kama ofisi ipo tu kwa 100% wakati yuko pekee na anaendelea na kampeni; tunahitaji watu kama hawa; UBUNGO MSITUANGUSHE
   
 12. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #12
  Sep 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Utendaji wa Mnyika umenifurahisha sana..
  Keep it up budy, usichoke.
   
 13. k

  kiuno Member

  #13
  Sep 5, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naombeni hayo majina pliz,mimi nimepitwa sana
   
 14. Nachingwea

  Nachingwea Senior Member

  #14
  Sep 5, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 173
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  uhuu ni ujinga, narrow thinking capacity
   
 15. W

  We can JF-Expert Member

  #15
  Sep 5, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  This is real exciting and paining but above all, it is people's right to find their right. Time will tell.
   
 16. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #16
  Sep 5, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  haki ya kufaidi maziwa na asali ya nchi hii kwa watanzania ama kwa hakika ipo karibu
   
 17. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #17
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  what is that
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu Superman,

  Nakubaliana na wewe, (mimi si mtalaam sana wa sheria), lakini kesi ya Mgombea Binafsi iko tofauti kidogo na kesi ya List of Shame (mafisadi). Kesi ya Mgombea Binafsi ilifunguliwa na Mtikila ikiwa ni kesi ya kikatiba ya kutaka watu wasio na vyama waruhusiwe kugombea kwa kuwa ni swala linalogusa haki ya kikatiba kwamba kila mtu ana haki ya kuchagua ama kuchaguliwa bila kujali kwamba ana chama au hana chama.

  Kesi ya ufisadi ni criminal case ambayo nadhani procedure zake ziko tofauti. Kesi kama hizo zinatakiwa kushughulikiwa na Jamhuri, na kama Jamhuri ikionekana kuvuta miguu ndipo sasa mtu binafsi anaweza (kuomba/kuamua?) kufungua kesi dhidi ya hao ambao anawatuhumu lakini inakuwa chini ya Private Prosecutor, so DPP na vyombo vya dola like Polisi na PCCB wanakuwa hawahusiki. Ninadhani kuna complications za aina fulani katika kutekeleza hili.

  Labda wataalam wa sheria wanaweza kuja kutuambia kwa kina utaratibu wa Private Prosecution ukoje kwenye hizi kesi ambazo unakuta Jamhuri haina interest ya kushitaki watuhumiwa.
   
 19. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Chadema yajitetea Nec dhidi ya CCM Send to a friend Saturday, 04 September 2010 20:42

  Geofrey Nyang’oro
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewasilisha ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) majibu ya utetezi wake kuhusu malalamiko ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeikashifu viongozi wake waandamizi wakati wa uzinduzi wa kampeni huku kikitoa orodha ya mafisadi kama moja ushahidi kwake.

  Katika majibu hayo imo orodha ya majina 12 ya watuhumiwa wa ufisadi ambayo iliwahi kutangazwa na Chadema mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembeyenga.

  Naibu katibu wa Chadema John Mnyika jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamechukua hatua hiyo ili kuthibitisha kauli zao walizozitoa kwenye uzinduzi wa kampeni zao wiki moja iliyopita katika viwanja vya Jangwani.

  “Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chadema inaeleza wazi kuwa viongozi wote ambao walishabainisha kuhusika na tuhuma za ufiasadi na ubadhilifu wa mali ya umma ambao serikali imeshindwa kuwafikisha mahakamani, watafiishwa mahakamani ndani ya siku 180, iwapo tutaingia madarakani,” alisema Mnyika.

  Alisema watuhumiwa hao wakiwamo marais wastaafu ambao wataondolewa kinga yao na Bunge ili wafikishwe mahakamani.

  Mnyika alifafanua kuwa hatua hiyo imelenga katika kujenga uongozi bora na kuimarisha utawala wa sheria hapa nchini.
  Kuhusu kutaja orodha ya majina ya mafiasadi kwenye mkutanio huo chama hicho kilisema huo si ukiukaji wa maadili ya uchaguzi kwakuwa tuhuma hizo zipo na wahusika hadi sasa hawajachukuliwa hatua na baadhi yao wanagombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
  Alisema madai yote waliyoyatoa kwenye viwanja hivyo wana ushahidi nayo na mengi ni yale ambayo tayari waliwahi kuyaweka wazi siku za nyuma.

  Kwa sababu hiyo, Chadema iliitaka Nec kutupilia mbali malalmiko ya CCM kwa sababu waliwasilisha bila kusoma sheria za maadili.
  Source:Mwananchi
   
 20. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,617
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Hivi hapa JF hakuna lawyer awatoe watu matongotongo???
   
Loading...