CCM wajiandaa kujibu kauli ya Anne Kilango kuhusu kuogopa mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wajiandaa kujibu kauli ya Anne Kilango kuhusu kuogopa mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Black Jesus, Apr 12, 2009.

 1. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wajiandaa kujibu kauli ya Anne Kilango kuhusu kuogopa mafisadi

  Na Kizitto Noya

  KAULI ya Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaogopa kupambana na ufisadi kwa kuwa mafisadi ni viongozi wenzao, inaonekana kukikera chama hicho na sasa kinaandaa taarifa maalum kujibu mapigo.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Katibnu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alisema ingawa suala la ufisadi limejadiliwa vya kutosha katika jamii, atalazimika kuandaa taarifa kujibu kauli ya Kilango na kuikabidhi kwa katibu mwenezi wa CCM ili aitoe kwa vyombo vya habari.

  "Haya mambo yanaandaliwa, hatukurupuki tu na kujibizana magazetini. Ninaandaa taarifa na baada ya Sikukuu ya Pasaka mtafute katibu mwenezi akupe ufafanuzi wangu," alisema Makamba.

  Makamba alitoa kauli hiyo baada ya kusita kwa muda kuzungumzia suala hilo akidai kuwa yaliyosemwa kuhusu ufisadi, yametosha na jamii sasa inapaswa kujadili mambo mengine ya maendeleo.

  "Niache, mimi niko likizo ya sikukuu na najiandaa kwa uchaguzi wa jimbo la Busanda. Ukitaka tuzungumzie uchaguzi huo kwa kuwa ndiyo suala jipya," alisema Makamba na kuongeza:

  "Suala la ufisadi limepitwa na wakati, kwani limejadiliwa sana na mengi yamezungumzwa, na hata CCM imejitahidi kueleza," alisema.

  Makamba alieleza hayo alipotakiwa kueleza msimamo wake akiwa Katibu Mkuu wa CCM kuhusu kauli ya Kilango kwamba viongozi wa CCM wanashindwa kuwafichua mafisadi, kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa wamo wabunge, viongozi na wanachama wenzao.

  Kilango alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi’, kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni cha Star na kueleza kuwa ugumu wa viongozi wa CCM kupambana na mafisadi, upo katika ukweli kwamba, wanaopambana nao ni viongozi wenzao.

  Bila ya kutoa mifano bayana, Kilango alisema ni wabunge wachache wanaoweza kusimama kidete kutetea sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM inayozungumzia vita dhidi ya ufisadi na hii inatokana na mahusiano yaliyopo kati ya watuhumiwa na viongozi hao.

  "Ugumu wa sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni kwamba, unapambana na mwanachama mwenzako, mbunge na hata kiongozi. Na hii ndio inawafanya watu wengi kushindwa isipokuwa wachache kama mimi," alisema Kilango na kuongeza.

  "Unaposimama imara kutaka kufanya mabadiliko kutetea haki na kupinga ubatili, unapaswa kutegemea mengi na mimi niliyategemea na ndio maana sipati tabu katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi".

  Alisema viongozi wa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuwa wakweli na wawazi katika kupinga rushwa kama wanavyofanya watu wa Marekani.

  "Nchini Marekani mtu aliyetaka kurithi nafasi ya useneta wa Obama alitanguliza rushwa ili kuwashawishi wajumbe, jambo ambalo liliwafanya Wamarekani kusimama imara na kuzungumza ukweli kuhusu kashfa hiyo," alisema Kilango ambaye alipata tuzo ya ‘Mwanamke Jasiri’ aliyopewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni.

  Alisema jamii inapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote wachache waliothubutu kuikemea rushwa nchini.

  Katika kashfa nyingi za ufisadi, viongozi na wabunge wa CCM ndio wamekuwa wakituhumiwa kuhusika na miongoni mwa waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa zamani katika serikali ya CCM, huku moto dhidi ya wabunge wa sasa ukizidi kuwaka katika kashfa za miradi mikubwa.

  Miongoni mwa miradi hiyo ni ununuzi wa rada, ambao umeelezwa kuwa ulifanywa kwa kuongeza bei ili iwe juu kwa lengo la kujipatia kamisheni nzuri. Miradi mingine ni wa uzalishaji umeme wa dharura wa Richmond uliosababisha mawaziri kujiuzulu baada ya kutajwa kwenye ripoti ya kamati teule ya bunge na wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira.

  Kashfa nyingine iliyohusisha wanachama na viongozi wa CCM ni wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), katika benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo inahusisha majina ya vigogo wanaohusishwa na kampuni zilizochota fedha nyingine, lakini imekuwa ni vigumu kuwataja.

  Hata hivyo Kilango hakutaja majina ya watu wanaojaribu kuwazuia au kuwamaliza, bali aliapa kuendelea na vita hiyo kwa kuwa hayo ni maumbile na hulka yake.

  "Mimi ndivyo nilivyozaliwa na ni maumbile yangu kuzungumza ukweli. Rangi nyekundu nitasema kuwa ni nyekundu na bluu pia, wala hakuna mtu atakayeweza kuninyamazisha ili niseme kuwa ni nyeupe, kibaiolojia siku zote naweza," alisema na kuongeza:

  "Wapo wapole, waoga ambao hata chumbani kulala peke yao wanaogopa, lakini pia wako majasiri wanaothubutu".

  Alisema Watanzania walishachoshwa na rushwa na kufikia hatua ya kujenga imani kuwa wabunge wa CCM wapo kwa ajili ya kuilinda serikali yao na wanaoweza kuikosoa ni wabunge wa upinzani tu.

  "Sasa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuondoa imani hiyo na sisi tupo kwa ajili ya wananchi na msimamo wangu, chama hakiwezi kupendwa kama hakikosolewi. Tukikosoa ndio tunakipa afya na si kukidhoofisha kama wanavyodhani baadhi ya watu," ailsema.

  Alifafanua kuwa vita dhidi ya rushwa ni kama mashindano ya riadha kwani kuna wanaoanza wanaoshindwa katikati, wanaomaliza na pia kuna wasiothubutu kuanza.
   
  Last edited: Apr 12, 2009
 2. p

  p53 JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  sasa mzee hiyo heading hapo umeitowa wewe au ndiyo tayari iko kwenye ripoti ya Makamba?Kwahiyo kwavile mmempa nafasi hiyo asiseme mnavyokwiba mabilioni ya wadanganyika?
  Mafisadi wanamtishia nyau mama Kilango!
   
 3. p

  p53 JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  safi mods manake heading ilikuwa inatisha!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,910
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::4/11/2009

  CCM wajiandaa kujibu kauli ya Anne Kilango kuhusu kuogopa mafisadi

  Na Kizitto Noya

  Mwananchi

  KAULI ya Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango kuwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaogopa kupambana na ufisadi kwa kuwa mafisadi ni viongozi wenzao, inaonekana kukikera chama hicho na sasa kinaandaa taarifa maalum kujibu mapigo.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alisema ingawa suala la ufisadi limejadiliwa vya kutosha katika jamii, atalazimika kuandaa taarifa kujibu kauli ya Kilango na kuikabidhi kwa katibu mwenezi wa CCM ili aitoe kwa vyombo vya habari.

  "Haya mambo yanaandaliwa, hatukurupuki tu na kujibizana magazetini. Ninaandaa taarifa na baada ya Sikukuu ya Pasaka mtafute katibu mwenezi akupe ufafanuzi wangu," alisema Makamba.

  Makamba alitoa kauli hiyo baada ya kusita kwa muda kuzungumzia suala hilo akidai kuwa yaliyosemwa kuhusu ufisadi, yametosha na jamii sasa inapaswa kujadili mambo mengine ya maendeleo.

  "Niache, mimi niko likizo ya sikukuu na najiandaa kwa uchaguzi wa jimbo la Busanda. Ukitaka tuzungumzie uchaguzi huo kwa kuwa ndiyo suala jipya," alisema Makamba na kuongeza:

  "Suala la ufisadi limepitwa na wakati, kwani limejadiliwa sana na mengi yamezungumzwa, na hata CCM imejitahidi kueleza," alisema.

  Makamba alieleza hayo alipotakiwa kueleza msimamo wake akiwa Katibu Mkuu wa CCM kuhusu kauli ya Kilango kwamba viongozi wa CCM wanashindwa kuwafichua mafisadi, kwa kuwa miongoni mwa wanaotuhumiwa wamo wabunge, viongozi na wanachama wenzao.

  Kilango alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza katika kipindi cha ‘Tuongee Asubuhi', kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni cha Star na kueleza kuwa ugumu wa viongozi wa CCM kupambana na mafisadi, upo katika ukweli kwamba, wanaopambana nao ni viongozi wenzao.

  Bila ya kutoa mifano bayana, Kilango alisema ni wabunge wachache wanaoweza kusimama kidete kutetea sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM inayozungumzia vita dhidi ya ufisadi na hii inatokana na mahusiano yaliyopo kati ya watuhumiwa na viongozi hao.

  "Ugumu wa sura ya nane ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ni kwamba, unapambana na mwanachama mwenzako, mbunge na hata kiongozi. Na hii ndio inawafanya watu wengi kushindwa isipokuwa wachache kama mimi," alisema Kilango na kuongeza.

  "Unaposimama imara kutaka kufanya mabadiliko kutetea haki na kupinga ubatili, unapaswa kutegemea mengi na mimi niliyategemea na ndio maana sipati tabu katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi".

  Alisema viongozi wa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuwa wakweli na wawazi katika kupinga rushwa kama wanavyofanya watu wa Marekani.

  "Nchini Marekani mtu aliyetaka kurithi nafasi ya useneta wa Obama alitanguliza rushwa ili kuwashawishi wajumbe, jambo ambalo liliwafanya Wamarekani kusimama imara na kuzungumza ukweli kuhusu kashfa hiyo," alisema Kilango ambaye alipata tuzo ya ‘Mwanamke Jasiri' aliyopewa na Serikali ya Marekani hivi karibuni.

  Alisema jamii inapaswa kuwaunga mkono kwa nguvu zote wachache waliothubutu kuikemea rushwa nchini.

  Katika kashfa nyingi za ufisadi, viongozi na wabunge wa CCM ndio wamekuwa wakituhumiwa kuhusika na miongoni mwa waliofikishwa mahakamani ni viongozi wa zamani katika serikali ya CCM, huku moto dhidi ya wabunge wa sasa ukizidi kuwaka katika kashfa za miradi mikubwa.

  Miongoni mwa miradi hiyo ni ununuzi wa rada, ambao umeelezwa kuwa ulifanywa kwa kuongeza bei ili iwe juu kwa lengo la kujipatia kamisheni nzuri. Miradi mingine ni wa uzalishaji umeme wa dharura wa Richmond uliosababisha mawaziri kujiuzulu baada ya kutajwa kwenye ripoti ya kamati teule ya bunge na wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe wa Kiwira.

  Kashfa nyingine iliyohusisha wanachama na viongozi wa CCM ni wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), katika benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambayo inahusisha majina ya vigogo wanaohusishwa na kampuni zilizochota fedha nyingine, lakini imekuwa ni vigumu kuwataja.

  Hata hivyo Kilango hakutaja majina ya watu wanaojaribu kuwazuia au kuwamaliza, bali aliapa kuendelea na vita hiyo kwa kuwa hayo ni maumbile na hulka yake.

  "Mimi ndivyo nilivyozaliwa na ni maumbile yangu kuzungumza ukweli. Rangi nyekundu nitasema kuwa ni nyekundu na bluu pia, wala hakuna mtu atakayeweza kuninyamazisha ili niseme kuwa ni nyeupe, kibaiolojia siku zote naweza," alisema na kuongeza:

  "Wapo wapole, waoga ambao hata chumbani kulala peke yao wanaogopa, lakini pia wako majasiri wanaothubutu".

  Alisema Watanzania walishachoshwa na rushwa na kufikia hatua ya kujenga imani kuwa wabunge wa CCM wapo kwa ajili ya kuilinda serikali yao na wanaoweza kuikosoa ni wabunge wa upinzani tu.

  "Sasa wananchi wa Tanzania wanapaswa kuondoa imani hiyo na sisi tupo kwa ajili ya wananchi na msimamo wangu, chama hakiwezi kupendwa kama hakikosolewi. Tukikosoa ndio tunakipa afya na si kukidhoofisha kama wanavyodhani baadhi ya watu," ailsema.

  Alifafanua kuwa vita dhidi ya rushwa ni kama mashindano ya riadha kwani kuna wanaoanza wanaoshindwa katikati, wanaomaliza na pia kuna wasiothubutu kuanza.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,910
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::4/11/2009
  CCM mafisadi,CCM safi wakabana makoo uchaguzi Busanda

  Waandishi wetu, Mwanza na Dar es Salaam

  Mwananchi

  PANDE mbili zinazohasimiana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinachuana vikali kupenyeza watu wao ili wateuliwe kuwa wagombea ubunge kupitia chama hicho, katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Busanda, wilayani Geita, mkoani Mwanza.

  Tayari pande zote zimehamasisha watu wake kuchukua fomu na kutokana na kutojiamini, wamejikuta wakihimiza watu wengi kuchukua fomu ili kuwa na uwanja mpana wa kuteua kukiwakilisha chama hicho katika uchaguzi huo unaotarajia kufanyika Mei 24, mwaka huu.

  Habari zilizolifikia Mwananchi Jumapili kutoka ndani ya CCM zilieleza kuwa pande hizo zinachuana vikali na hadi mwishoni mwa wiki hii, idadi ya walioomba nafasi hiyo ilikuwa imefikia 12.

  Pande hizi zinazochuana ni zilizozuka wakati wa fukuto la kuwaumbua mafisadi ndani ya serikali ya awamu ya nne na ndani yake lipo kundi la wanaojiona ni CCM safi na jingine linaloandamwa na tuhuma za kifisadi.

  Mgawanyiko huo unatokana na kundi la CCM mtandao ambalo ndilo liliwezesha serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani, lakini sasa wanaonekana kutofautiana baada ya upande mmoja kuonekana kuumbuliwa.

  Makundi yote yamekuwa yakijaribu kuweka mikakati ya kujijengea nguvu ndani ya chama hicho ingawa hili la CCM safi linaonekana kushikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya chama pamoja na serikali.

  Vita ya kuwania nafasi kati ya makundi haya mawili ndani ya CCM, imeanza muda mrefu na ilianza kujitokeza wazi wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na katika uchaguzi mdogo wa Busanda; mambo yanaonekana kuwa makali.

  Chanzo chetu ndani ya CCM kilieleza kuwa hadi sasa kundi linalotuhumiwa kwa ufisadi linaoongoza kwa kufanikiwa kupenyeza wagombea saba kwenye kinyang'anyiro hicho.

  Kwa mujibu wa katibu wa CCM Wilaya ya Geita, Rahel Ndegeleke zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu lilikuwa likienda vizuri na tayari 12 walikuwa wamekamilisha taratibu za chama kuomba kugombea.

  Aliwataja waliochukua fomu kuwa ni Sostenes Kurwa ambaye ni Mfamasia katika Mkoa wa Mwanza, Lolesia Bukwimba ambaye ni Meneja wa shirika linalojishughulisha na utoaji wa mikopo la Seda.

  Wengine ni aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 1995 hadi 2000, Ernest Kahindi ambaye alishindwa mwaka 2000 na Rwilomba ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo.

  Yumo pia, Donald Max ambaye ni Mweka Hazina wa CCM wilayani Geita na pia aliwahi kuwania ubunge katika jimbo la Geita Mjini na kuangushwa na mbunge wa sasa, Ernest Mabina.

  Wengine ni Lucas Bilie, Tumaini Magesa, Francis Misana, Sambili Mlingwa, Nicholaus Kasendamila, Abdallah Musa, Robert Kiganga na Jonathan Mpuya.

  Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Busanda utafanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Faustine Rwilomba aliyefariki dunia Machi 12, mwaka huu nchini India, ambako alikuwa amelazwa akitibiwa maradhi ya moyo.

  Wakati ndani ya CCM wanavutana mashati, upande wa vyama vya upinzani nako wanajaribu kuweka mikakati ya namna ya kulinyakua jimbo hilo ambalo lilikuwa chini ya chama hicho tawala.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) tayari kimeanza kupima nguvu ya operesheni sangara katika jimbo hilo.

  Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa aliliambia Mwananchi Jumapili kwamba, mpaka sasa waliochukua fomu kuwania kiti hicho ni watano.

  Huku akitamba kuwa safari hii lazima wachukue jimbo hilo, Mtemelwa aliwataja waliokwishachukua fomu kuwa ni Fineas Magesa, Nazir Mneka, Oscar Ndalawa, Meshack Opurukwa na Baltazar Madaha.

  Licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kuthibitisha kugombea bado hakuna taarifa za kuanza kujitokeza kwa wagombea wao, ingawa kumekuwa na tetesi kuwa wanasubiri watu wenye ushawishi watakaotemwa na CCM au Chadema.

  Picha halisi ya vita ya kuwania kiti hicho itaonekana Aprili 16 baada ya kumalizika kwa kura za maoni ndani ya CCM, japokuwa pia kitimutimu cha baadhi ya wawaniaji hao kuhama, kitajitokeza baada ya CCM kutangaza mgombea wake.

  Tayari vyama vimeanza kutambiana ambapo katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Rajabu Kundya alijigamba kuwa chama chake kinaingia katika uchaguzi kurejesha kiti chake kwa vile wanao wanachama wengi ndani ya jimbo hilo kuliko vyama vya upinzani.

  Kwa upande wa Chadema, Mtemelwa ameeleza kuwa iwapo hawatahujumiwa kama ilivyokuwa Mbeya kwa kuenguliwa mapema basi CCM itarajie kupoteza kiti hicho.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chama hicho, Msafiri Mtemelwa alisema uamuzi huo umefikiwa baada ya Sekretarieti ya Kamati Kuu kukutana Machi 31, mwaka huu pamoja na Tume ya Uchaguzi (NEC) kutangaza tarehe ya uchaguzi katika jimbo hilo ambayo ni Mei 24, mwaka huu.

  Chadema ilitangaza uchukuaji wa fomu Aprili 6, mwaka huu na mwisho wa kurudisha itakuwa Aprili 15. Aprili 18, mwaka huu Kamati ya Utendaji ya Chama hicho itakutana kufanya uteuzi na taarifa yake itawasilishwa kwa Kamati Kuu ambayo itafanya uamuzi wa mwisho kwa kupitisha jina la mgombea atakaye kiwakilisha chama hicho.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Yote haya ya akina Makamba na wenzake hayashangazi, kinachoshangaza ni kwa nini Mkuu wa Kaya (JK) ambaye ndiye pia mkuu wa chama chao anawavumiliwa watu hawa ambao ni dhahiri wanakwenda kinyume kabisa na dhamira ya umma mzima wa kuwapiga vita mafisadi?

  Inawezekana kweli hata JK mwenyewe anasapoti hili? kama JK yupo makini na kuwa pamoja na umma, na kama ni jasiri kama anavyotaka tuamini, basi tunatarajia amkataze Makamba asimjibu Mama huyo shujaa aliyepewa tuzo ya heshima hivi karibuni. Itaonekana sasa CCM imekuwa genge la wahuni tu kila mtu anasema vyake -- hakuna heshima kabisa!

  VIVA Anne!!!!!!!!
   
 7. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Anne sasa ndio kafikishwa...hapo ataweweseka hapo hadi basi aanze kujiandaa maana wanaweza wakamtosa kabisa hata kura maoni....balaa sana jamani tungweza kupata nusu bunge wawe msimamo kama huu....basi bunge lingekuwa na meno kama msumeno...ila sasa ni kibogoyo bora liende
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  CCM wana utaratibu mpya ambao unaweza kuwa msaada kwa Kilango katika kura za maoni .Mwache ajimwage nasi tunampima tu .
   
 9. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mdau FMES Sauti ya umeme... uwanja ni wako...
   
 10. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi wabongo bado mtaendelea kuwa Naive for how long?hii yote ni mipango imepangwa na wenywe CCM huyo mama wamemtuma atowe kauli hizo wakiwa wanajuwa nini kitatokea na nini wanataka kukifanya, hapa nitakumbusha kiongozi mmoja wa upinzani Mr juma Duni akiwa katika moja ya mikowa ya Tz bara aliwambia wanachi ya kuwa CCM ni kama Ulevi (pombe)ukinywa kwenye glass utalewa (kupombeka)ukitumia jani la mgoma Gubi, kifuu chombo chochote kile utalewa tu (kupombeka) Tatizo kwa sasa ni sisi wananchi ishak,uwa mazowea kwetu kuhadaliwa na viongozi wetu ,CCM wakikupa miyadi tusubiri Dar wewe kawasubiri Mtwaza hawa watu wapo very advanced haitonishanga siku moja nikasikia wamekuwa na (WEB SITE )ya ulahai tuamkeni wananchi tunaishi katika (21mileniyam)
   
 11. M

  Magezi JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  wana JF mbona iko wazi kabisa JK anasapoti yanayoendeshwa na CCM mafisadi, jamani ni nani aliagiza Amina chifupa aondolewe uhai haraka?? Yule dada alikuwa na ushahidi ambao ulikuwa unamhusisha JK kwa namna fulani kwani rafiki zake na JK ambao ni magwiji wa mihadarati hapa TZ walimchangia fedha za campaign na najua deals zao. Sasa mdada alipeleka majina yale bila kujua kuwa jk anafahamiana na hao watuhumiwa.

  Kwa hiyo ulisukwa mpango kwa kutumia vijana wetu ambao ni mashuhuri kwa kukorimba then wakamkorimba mdada wa watu. Kwa hiyo Anna Kilango anajua haya kwani mzee samwel amekuwa jikoni atakuwa amemweleza kwamba ajihami mapema.
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama CCM ikishindwa kutupatia uongozi makini, nchi ipo hatarini. Kama wao kwa wao wanaanza kubishana kwa suala ambalo li wazi, wanaonyesha kuwa wanashindwa kutupatia yuongozi makini unaohitajika katika kipindi hiki. Tusubiri kauli ya makamba, labda itazidi kutupa mwanga zaidi kuwa nani yupo upande gani katika vita dhidi ya ufisadi
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani, vita dhidi ya ufisadi inaishia na kujadili suala hili tu au na kuchukuliwa hatua stahili kwa wahusika/watuhumiwa? Inashangaza kusikia kuwa KM wa CCM- Makamba akisema ati wananchi wamezungumizia ufisadi sana hadi ajenda hiyo sasa imepitwa na wakati! Ingepitwa na wakati kama serikali na vyombo vyake vingesimama kidete na kuchukua hatua kama wananchi wanavyotegemea.Huenda ikawa kuwa jamii bado inaendeleza kuzumgumzia ufisadi kwa vile hakuna hatua za kutosha zimechukuliwa.
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bi Mkubwa,

  Hata mimi nashangazwa sana na hili taifa especially hiki chama twawala. Kesi ya uwizi na ufisadi inafanyiwa majadiliano na vuta nikuvute na sarakasi kibao badala ya kupelekwa kortini ili sheria ichukue mkondo wake.

  Inasikitisha sana.
   
 15. F

  Fataki Senior Member

  #15
  Apr 12, 2009
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hivi Mkuu, Makamba ana ubavu wa kumjibu Mama Anne-Kilango Malecela? Atatoa wapi majibu wakati yeye mwenyewe ni mfadhiliwa wa mafisadi? Sana sana anachoweza kufanya ni kumwagiza Rostam ayatume magazeti yake kumshambulia mama huyo mfululizo kwa wiki mbili hivi kwa hoja za kijinga kama ilivyofanyika kwa Mwakyembe. Baada ya hapo wanaita Kamati ya Maadili "kusuluhisha". CCM, Usanii Mtupu!
   
 16. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Fisadi ni Fisadi hata umsugue kwa wire wa chuma hatakati!!!!!! Na kauli za Makamba naona zinazidi kumpeleka shimoni !! asipoangalia kuzimu kabisa!!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  "Hivi Mkuu, Makamba ana ubavu wa kumjibu Mama Anne-Kilango Malecela? Atatoa wapi majibu wakati yeye mwenyewe ni mfadhiliwa wa mafisadi? Sana sana anachoweza kufanya ni kumwagiza Rostam ayatume magazeti yake kumshambulia mama huyo mfululizo kwa wiki mbili hivi kwa hoja za kijinga kama ilivyofanyika kwa Mwakyembe. Baada ya hapo wanaita Kamati ya Maadili "kusuluhisha". CCM, Usanii Mtupu!"

  *************************
  FATAKI: Umenena haswa ndugu yangu. Ndivyo itakavyokuwa -- yaani RA kutumia magazeti uchwara kulumbana na Anne. Na badala ya kujibu hoja zake, magazeti hayo yatatafuta "madhambi" yake na kuyasokota yaonekane ukweli. Nafikiria vichwa vya habari: "Anne Kilango maji shingoni" au "Wananchi wa Same Mashariki kumtema AK 2010" ili muradi tu kumkashifu shujaa huyu.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,910
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Tusubiri kauli ya Makamba kujibu tuhuma nzito za Mama Kilango, lakini kwa maoni yangu tuhuma nzito kama hizi dhidi ya CCM zinatakiwa zijibiwe na kiongozi mkuu wa CCM ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho. labda kwa mara nyingine tena yeye hahusiki!!!!
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Je ni kweli sera ya kupambana na mafisadi ndio imeshatoka ? Kwa mujibu wa Makimba kuwa vita vya mafisadi vimeshapitwa na wakati..! Huo ni mwito kwa nionavyo mimi kuwaambia makada kuwa msijadili tena wala kujibu hoja zihusianazo na mafisadi ,ziwekeni kando na zaidi mseme zimeshapitwa na wakati . Tujadili mengine au tujipange kwa uchaguzi wa 2010 ndio maana yake.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,910
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli ya Makamba swala la ufisadi limeshapitwa na wakati, na kama sikosei wiki chache zilizopita katika mkutano wa IMF uliofanyika Dar, Kikwete alipoulizwqa swali kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi vimefikia wapi na mmoja wa wajumbe katika mkutano huo, alijibu kwamba vita hivyo bado ni mbichi kabisa lakini hakufafanua. Sasa utaona ni jinsi gani kauli za viongozi wa juu zinavyogongana katika swala hili la vita dhidi ya ufisadi.
   
Loading...