Ccm waja juu mbeya, wajitapa kushinda uchaguzi wa udiwani.

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
CCM waja juu Mbeya


na Christopher Nyenyembe



VIONGOZI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) jana waliibuka kutoka mafichoni na kudai kuwa kambi iliyowekwa kwa ajili ya kuwafua vijana wao, haiendeshi mazoezi ya kijeshi kama wanavyodai viongozi wa CHADEMA.


Kuibuka kwa viongozi hao, kumekuja siku moja baada ya gazeti hili kutoa taarifa kwamba CCM inaendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana hao kwa lengo la kuvuruga uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Iyela, mjini hapa.


Licha ya viongozi hao wa CCM kukiri kuwapo kwa kambi za vijana wanaopatiwa mafunzo maalumu, walikataa kutaja idadi yao na kwamba huo ni utaratibu wa chama chao na hawajatumwa na Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Nchemba kwa lengo la kuvuruga uchaguzi.


Mwenyekiti wa Vijana CCM Wilaya ya Mbeya, Malanyingi Matukuta akiwa ameongozana na viongozi wenzake hadi katika ofisi za gazeti hili mjini hapa alisema kuwa chama hicho hakijifui kijeshi kama inavyodaiwa na CHADEMA.


“Si kweli, sisi ndio haswa walinzi wa chama, walinzi wa viongozi wetu na ndiyo maana tuna kitu kinaitwa ‘Green Guard’. Ni wazi kuwa hatuwezi kuwa na Green Guard bila mazoezi, huu ni utaratibu wetu, hatuwezi kuuacha, tutaendelea na mazoezi ya ukakamavu ambayo si hatarishi,” alisema Matukuta.


Alisema kwa kuwa chama hicho kimeweka utaratibu wa kuwaweka vijana wao kambini kwa ajili ya mafunzo na wataendelea kujifunza ukakamavu, ujasiriamali, masomo ya itikadi, itifaki, uzalendo kwa chama chao.


“Sijaelewa wenzetu wanakwenda kwenye vyombo vya usalama kufanya nini, kweli askari kanzu walikuja kwenye kambi yetu wakawapiga picha vijana waliokuwa wakifanya mazoezi kisha waliondoka bila kusema lolote, hizi zote ni propaganda za CHADEMA,” alisema mwenyekiti huyo.


Akizungumzia uchaguzi wa udiwani Kata ya Iyela, Malanyingi alisema kuwa wao wamejipanga vizuri na wana uhakika na ushindi ndiyo maana CHADEMA wanahaha baada ya kumuona mgombea wao, Richard Shanghvi anakubalika kwenye kata hiyo.


Viongozi wa CHADEMA juzi waliitisha kikao na vyombo vya habari wakielezea kuwepo kwa hofu iliyotanda ya kuwepo kwa kambi tatu za mafunzo ya kijeshi yanayotolewa kwenye shule za sekondari, Itende, Igawilo na Ivumwe zinazomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi CCM.
 
Enhee ! Wewe Mwenyewe ndugu Bungeni una maoni gani ? Ikiwa raia wanafundishwa kutumia mitutu ( mafunzo ya kijeshi )?
 
Ccm ni wahuni tu, wanasubiri muda tu wakiona mwelekeo hauko upande wao utasikia tu mambo ya tindikali, mtu kupigwa shoka nk na yote yanafanya na hao greenguard wa ccm kisha watasingizia chadema
 
Back
Top Bottom