CCM waitana kumalizana; Mikoa yote kukutana Dar kujadili 'gamba lao' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM waitana kumalizana; Mikoa yote kukutana Dar kujadili 'gamba lao'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngalikihinja, Oct 31, 2011.

 1. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  UONGOZI wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), umelazimika kuitisha kikao cha dharura cha wenyeviti wote wa mikoa ili kupoza joto la upinzani mkali lililoibuka baina ya makundi mawili yenye nguvu ndani ya chama hicho.

  Habari za kuaminika zilizolifikia Tanzania Daima zimeeleza kuwa kikao hicho kitakachofanyika kuanzia leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee, kitakuwa chini ya uenyekiti wa Pius Msekwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, kutokana na kutokuwapo nchini kwa mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete.

  Taarifa zimebainisha kuwa katika kikao hicho, ajenda kuu zitakazojadiliwa ni hali ya kisiasa nchini na suala zima la kupanda kwa gharama za maisha.
  Habari zinasema kuwa ajenda itakayokuwa ya moto ni ya hali ya siasa nchini, lakini zaidi ndani ya chama hicho kuhusiana hasa na falsafa ya kujivua gamba ambayo imesababisha mpasuko mkubwa ndani ya CCM.

  Wenyeviti hao watajadili njia zitakazofaa kuchukuliwa ili kupoza joto lililoibuka ndani ya chama hicho na ambalo limewagawa viongozi wa juu katika makundi mawili yenye nguvu ambayo yamekuwa yakipingana kwa siri na hata waziwazi kwa miezi kadhaa sasa kuhusiana na dhana hiyo ya gamba.

  Kwa upande mmoja, baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho, hawakubaliani na namna ya utekelezaji wa dhana hiyo, wakidai kuwa haikuwalenga wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu, Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz, kama inavyokuzwa na kundi jingine na kupigiwa chapuo kubwa na Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

  Katika maelezo yake siku anatangaza kujiuzulu ubunge na ujumbe wa NEC, aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam, alisema waziwazi kuwa anajivua nafasi hizo za uongozi baada ya kuchoshwa na kile alichokiita ‘siasa uchwara' zinazofanywa na Nape na kundi lake.

  Kwa upande mwingine, kundi linalompinga Nape na wenzake limechukua sura mpya baada ya kuungwa mkono kwa kiwango kikubwa na baadhi ya viongozi waandamizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), ambao msimamo wao ulizidisha msuguano mkubwa baina ya makundi hayo.

  Kuhusiana na ajenda ya uchumi, wenyeviti hao watazungumzia kupanda kwa gharama za maisha kwa Watanzania na kuangalia njia gani zitafanywa na serikali ili kupunguza ukali wa maisha.

  Tanzania Daima, lilipowasiliana na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kujua sababu za kikao hicho kufanywa siri, alikuwa mkali na kukata simu, akidai kwamba hawezi kuzungumza na mwandishi yeyote wa gazeti hili.

  Hata alipopigiwa mara ya pili, alifoka tena na kusema, "Hamna aibu nyie, mnanitafuta nini? Sitaki kuongea na ninyi," alisema na kukata simu.


  Source: Tanzania Daima ya leo
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Sio rahisi kufanikiwa. ikumbukwe kinachowasumbua CCM ni usaliti waliofanyiana, na makundi hayawezi kuisha kwani bado kila mtu anaona ana haki ya kuwa mtawala wa nchi. unadhani manywele meupe atawasamehe waliomuita gamba? undahani ataacha kutafuta uungwaji mkono tunapoelekekea general election?
   
 3. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  hivi baba riz hajarudi!!??kweli hii balaa.
   
 4. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,407
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  Labda wameshapata shoka la kulivulia gamba lillilokwamia sehemu fulani ya mwili.............
   
 5. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 1,523
  Trophy Points: 280
  ...........wanaowaona wenzao magamba waanze wenyewe kujivua, haiyumniki wao ndo hovyoo kuliko akina Lowassa waliowalenga, haingii akilini kabisa eti gamba linalenga kuwatoa watu kwenye vikao vya maamuzi tu, ili nini, muwatete uraisi..... hawakumsaidia mwenyekiti wao mawazo juu ya hili kama walimsaidia, basi walipa kile ambacho alipenda akisikie.
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Things fall apart. Tulivyowazoesha wanachama kupokea rushwa za kanga, fulana, kofia, pilau, sukari, na vibahasha sasa nani atamnyooshea mwenzake kidole. Rushwa imekua kama kansa iliyoenea CCM nzima.

  Dawa ni kuvunja hiki chama na kuunda kingine. Labda kile cha CCJ.
   
 7. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  acha wafu wazikane!
   
 8. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  La kuvunda halina ubani. Hivi kuna gamba kubwa kuliko Jakaya Mrisho Kikwete?
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hivi kuna gamba kubwa kuliko kama rushwa ya khanga, kofia na elfu tano tano. Wako taabani. wanakutana wafu wa siasa.
   
 10. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nawaomba maamuzi ya fikra sahihi za mwenyekiti yatawale
   
 11. kalukamise

  kalukamise JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 688
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Yees Mku Shoka ndio dawa, maana nyoka anaweza kujivua ngozi.. siamini kama kobe anaweza kujivua gamba...ni shoka tuuuuu
   
 12. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hakuna lolote litakalofikiwa juu ya wanayoyajadili labda waridhishane kwa muda mrefu au wawavue yale magamba sugu akina RACHEL kitu ambacho kundi jingine hawatakubali kamwe aaah! hii tamu wache waendelee kumalizana mie napenda iende hvyohvyo
   
Loading...