CCM - Wagombea wenye 3yrs of age - A joke or wht?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM - Wagombea wenye 3yrs of age - A joke or wht??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyambala, Dec 29, 2009.

 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu,

  Chama kile kikongwe naona kiko desperate mpaka inachekesha.......... Jisomee hapa chini for details.


  Mtoto wa Makalla kuwania Uenyekiti chipukizi

  na Nasra Abdallah

  MTOTO wa Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, Gabriel Makalla, amejitokeza kuwania nafasi ya uenyekiti wa chipukizi taifa ndani ya chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara.
  Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Desemba 29 katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe mkoani Morogoro, ambapo nafasi hiyo wamejitokeza jumla ya wagombea tisa - watano kutoka Tanzania Bara na wanne Visiwani.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja wa Vijana, Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Esther Bulaya, aliwataja wagombea wengine waliojitokeza na mikoa wanayotokea kwenye mabano kuwa ni Ally Mbaraka (Kagera), Asnail King (Dar es Salaam), Hayani Mkambuga (Kagera) na Paulina Lucas Kasonso (Mtwara).
  Kwa upande wa Tanzania Visiwani waliojitokeza ni Abdallah Ali Abdallah, Harith Juma Mwinyi, Harith Mohamed Mohamed na Mohamed Gharib Mohamed, wote kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi.
  Kwa mujibu wa Bulaya, vigezo ambavyo vinazingatiwa katika kugombea nafasi hizo ni kwa mgombea kuwa na umri kati ya miaka mitatu hadi 13 na awe na kadi ya uanachama.
  Aidha, alisema mbali na nafasi ya uenyekiti, nafasi nyingine zinazogombewa katika uchaguzi huo ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa atakayewakilisha chipukizi (nafasi mbili - moja Tanzania Bara nyingine Tanzania Visiwani).
  Nafasi nyingine ni ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Taifa ambapo nafasi zinazogombewa ni tatu - mbili Tanzania Bara na moja Zanzibar, huku nafasi za wajumbe wa Kamati ya Uendeshaji Taifa ni tatu - moja kutoka Tanzania Bara na mbili Zanzibar. "Ni kawaida na taratibu za uongozi wa chipukizi kufanya uchaguzi mkuu kila baada ya miaka mitatu, ambapo mkutano huu ni wa tano tangu kuanzishwa kwa chipukizi. "Hata hivyo mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa chipukizi ngazi ya matawi, kata, wilaya, mikoa hadi taifa na katika ngazi ya matawi hadi mkoa tayari wamekwishakamilisha chaguzi hizo," alisema Bulaya.

  source: freemedia.co.tz

  My take:

  1. Ina maana hao wanachama wa CCM tunaoaminishwa ni 4 million includes babies born in 2006???????


  2. What is the significance ya kuwa na mwenyekiti wa chipukizi nchi nzima? What are their roles?

  3. Hivi hii chipukizi iliffufuka lini? Na hizi taratitibu zilianza lini, enzi zile sikuwahi kusikia haya mambo.

  4. Is this not indoctrination of babies into the green party??????
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  Sisiem wametuchoka...
  Hivi ni vigezo gani vitatumika kumchagua mtoto wa miaka mitatu, je ni sera zake, je ni uwezo wake wa kuongea, au ni uzuri wa sura yake?
   
 3. TingTing

  TingTing Member

  #3
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Ingawaji kuna uhuru wa kila kitu lakini sasa tukienda kwa watoto ama ndugu zetu wenye umri chini a 18 sasa tunakuwa tunakosea kabisa. Hawa watoto badala ya kukaa shule kusoma wanakuwa wanawaza CCM tu kwa sababu kutakuwa na mijitu hapo pembeni inayowaongoza nini cha kufanya kwa kuwa bado hawana uwezo wa kuchambua na kupambanua mambo yanayohusu vyama na siasa. Hii Chil-Labor ni illegal jameni.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani mkuu inachosha kabisa, and these guys are serious. Na usijeshangaa ukaambiwa bilioni 2 zimetumika katika maandaliozi ya uchaguzi huo!
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hii ni abuse of human rights.

  Ninaposema ni abuse of human rights, I really mean it. Nakumbuka nikiwa na miaka nane tulikuwa tunapigishwa gwaride pale uwanja wa golf Morogoro kwenye jua mpaka watoto wanaaguka. Personally nilishapata kizunguzungu lakini nikaa chini kabla ya kuanguka. Lakini makamanda walinijia juu wakidhani nimefeki.

  Inakuwaje katika dunia ya leo wanawatumia watoto (under age) kuhakikisha kuwa wanaendelea kutawala?? Wanawapotezea muda wa shule na michezo inayowasaidia for their mental development na kuwafanyisha kazi za SISIM!!! Hii chipukizi nilifikiri ilikufa baada ya multparty kuingia kumbe wameiendeleza??
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Me too mkuu, nilijua chipukizi imekufa............ And it seems hii chipukizi ya sasa si kama ile ya wakati ule, hii inaonekana ni ya kisirisiri na ajenda yake sijui kama inajulikana
   
 7. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni njia ya kurithisha uadui watoto.Inatumika sana isreal kumpa mtoto hali ya kujua mpalestina ni adui yake na hivyohivyo kwa wapalestina kutambua Israel ni adui zao.Mtoto kadri anavyokuwa tayari anakuwa na hamasa ya kujua mpinzani wake ni nani na afanye nini kumdhibiti.Nenda hata Cuba watoto wadogo wanafundishwa kujua adui yao ni Amerika.Hivyo hawa sisieeem wamechukua mfumo huo kuwarithisha watoto wao wajue kabisa kuwa kadri wanavyokuwa wapo wapinzani wao ktk siasa ambao ni wasio kuwa sisieeem.Kuhusu suala la watoto kutosoma hilo sahau kwakuwa watoto wote wanaogombea nafasi hizo ni wanaotoka katika migongo ya vigogo,yaani wote hao wanasomeshwa shule zinazoitwa za kimataifa,sasa wewe ndugu yangu iga mpeleke mtoto wako akagombee utaona hasara yake.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Can this be justified in our society as of current???????? Well the Israelites and Palestinians indoctrinate kids for what they biliv is a national interest!!!!!!!!!

  But this of CCM is for whose interest, how do we skew kids minds at such a young age?????
   
 9. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sisieem and Mafias are of the same nature!
   
 10. a

  asif JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 28, 2009
  Messages: 335
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  hawapo sirius....... WE ARE GOING THROUGH A BAD PHRASE.... WE HAVE CHOOSEN THEM... inamaana sisi lazima tuwe pamoja ili tuwaamshe hawa...
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kinachotuumiza sana sisi ni hizi shortcuts; transforming from one party system to multiparty system without dismantling the old sole party and creating the new parties under same level ground.
   
 12. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yea mkuu, it is so funny and is like ccm wanaona the current system is ok as long as it works for them
   
Loading...