CCM wagawa pombe, ubwabwa na Nyama katika kijiji cha Tano wilayani Bagamoyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wagawa pombe, ubwabwa na Nyama katika kijiji cha Tano wilayani Bagamoyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanakidagu, Oct 26, 2012.

 1. m

  mwanakidagu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 208
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakati kampeni zikendelea mjini bagamoyo!kwa kutembelewa na naibu katibu mkuu wa cdm,hali ya mambo ni tofauti kijijini Tano. Pombe, ubwabwa na nyama vilitawala kwenye maeneo karibu na ofisi ya CCM. Gari ya matangazo ilisikika ikiwajulisha wananchi hao kuwa vituo ni vilevile vya kura. Kijiji hk kinaonekana si rasmi kwani kimefanyizwa na wahaibifu wa mazingira wakata mkaa.

  Kila kibanda kinapepea bendera ya CCM nimeziona pia bendera ya cuf moja na cdm moja.nimejiuliza sana huku porin kote mbona inaelekea hakuna serikal, wala shule.

  Ni watu wanaoish ndani ya mbuga ya wanyama kinyume cha sheria!tena wameleweshwa na kulishwa ubwabwa. CDM fuatilieni eneo hili huenda ndiko kura hewa zitatoka.

  Eneo lenyewe kuanzia kijiji cha makurunge-kisauke kuelekea mbuga ya saadani. Mimi nilikuwa kikaz .kupitia maeneo hayo kwa masuala ya utalii.
   
 2. mathcom

  mathcom JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 1,402
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Huko kusiko fikika ndiko ambako CCM inafika na huko watu hawapangi uzazi!
  sasa vyama pinzani mara nyingi hung'ang'ania mijini tuuu! Dar, mwanza, arusha, n.k.
   
 3. n

  nemasisi JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 1,881
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huko hata ccm hawafikî, wanafaidika na umaarufu tu wa chama chao, viongozi wa vyama vya upinzani hata wangependa bado hawataweza kufika kila kona ya nchi hii jambo la muhimu ni kwa wapenda mabadiliko kusaidia kueneza fikra hizi popote walipo ili na hao wengine wapeleke vijijini ziwe kama mbio za kupokezana vijiti vinginevyo tutaishia tu kuwalaumu viongozi..
   
 4. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Siku si nyingi watagawa bangi na cocaine kama watataka kura za wavuta bangi na mateja. Kesho kutwa watagawa tunguli kwa majambazi ukiachia mbali kondomu kwa wazinzi.
   
 5. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ccm wapo tayari kufanya chochote ili wapate kura,iwe hata kwa kuwahonga watu kwa kanga,vyakula na vinywaji.ni kudhalilisha watanzania.
   
 6. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Natoa wito kwa wananchi wote wa maeneo hayo wale,wanywe na hata wapokee pesa maana hizo ni ela zao lakini KULALA chadeni.
   
 7. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Kumbe wanaouwezo wa kugawa chakula bure..si wagawe nchi nzima sasa tuwaone
   
 8. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kwa wakazi wa huko kwa Ubwabwa ndo wenyewe. Hao ni vigumu kuwabadilisha kama wameshalishwa Ubwabwa na Mnazi
   
 9. C

  Concrete JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  *Hizo ni Propaganda za CCM za muda mrefu, eti kuwa CCM inapendwa vijijini na wapinzani mijini!!

  Ungejua huko vijijini walivyoichoka CCM wala usingesema hayo.

  *Ukweli ni kwamba vijijini ndiko CCM inawalaghai kirahisi sana wananchi kwa rushwa na pia ndiko uchakachuaji mkubwa wa kura unafanyika kirahisi zaidi.
  Kwa mfano, kijiji(Pori) chenye idadi ya wakazi 100 utashangaa kuna vituo vitatu vya kupigia kura, na matokeo yatakuwa CCM imeongoza kwa zaidi ya kura 200. Haya mambo tuliyaona vizuri Igunga na Arumeru mashariki.
   
 10. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wangekuwa hao CCM wanafika nadhani pangekuwa na maendeleo angalau kidogo tu. Labda kama unamaanisha huwa wanafika nyakati za uchaguzi tu na kutoa ahadi na kuondoka kwani ndio tabia yao ningekuelewa zaidi.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  mkuu uko nchi gani? maana kwenye sensa ccm imegawa bangi na nyama pori kwa wasonjo..hukusikia kama hujui fahamu serikali yako iliwa sonjo wakubali kuhesabiwa walitaka pombe, bangi na nyama..na mbunguni waliwahi kugawa bangi kwa apolo ili wawasaidie polisi kutoa maiti walio kuwa wamenasa migodini..
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mtaji wa CCM ni rushwa za pesa,khanga,T-shirt,ubwabwa! naambiwa siku hizi wanaonga mpaka under wear! CCM kwishney kabisa!
   
 13. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kwani kuna uchaguzi wa udiwani huko??
   
 14. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Crashwise mwanangu nakushukuru. Kwani sikuwa najua hivyo ingawa huo ulikuwa mwanzo. Kesho watagawa bwimbwi kwa mateja ili wawafichie siri hasa vigogo wa CCM wanaowauzia bwimbwi.
   
Loading...