CCM wadai kuwa na wanachama hai milioni 12. Natamani kusikia kwenye database ya vyama vingine

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
754
1,000
Kama tujuavyo kuwa kwenye shughuli ya siasa mtaji ni wanachama, CCM wanadai kuwa wana wanachama hai wapatao milioni 12. Ningetamani kujua na vyama vingine waweke data za wanachama wao hadharani.

Hii itasaidia sana kuwahamasha makada kufanya mapitio ya mipango na mbinu mbalimbali za kuongeza idadi ya wanachama.

Jambo lingine la kufanyika, ni vyema vyama vingine vya siasa vikaja na reforms kubwa sana, zenye kukidhi uwezo sawia wa kuikabili CCM iliyojilimbikizia kila nguvu tajika.

Vinginevyo tutafanya siasa za maigizo mpaka siku ya kiyama.
 
Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,340
2,000
Ni kweli hizo data zipo. Nijuavyo wengi walilazimika kujiunga ndani ya miaka 5 iliyopita kutokana na hali halisi ilivyokuwa. Hasa wanachuo na wapiga deal kwa sababu kila kitu kilihitaji lazima uwe CCM ndipo ufikiriwe utendaji, ualimu, Tarafa nk. Hata sasa hakuna uwezekano wa kuwakwepa. Binafsi nimejiunga rasmi CCM lkn sina matokeo HD uchaguzi.
 
stakehigh

JF-Expert Member
Aug 9, 2019
5,027
2,000
Ni kweli hizo data zipo. Nijuavyo wengi walilazimika kujiunga ndani ya miaka 5 iliyopita kutokana na hali halisi ilivyokuwa. Hasa wanachuo na wapiga deal kwa sababu kila kitu kilihitaji lazima uwe CCM ndipo ufikiriwe utendaji, ualimu, Tarafa nk. Hata sasa hakuna uwezekano wa kuwakwepa. Binafsi nimejiunga rasmi ccm lkn sina matokeo HD uchaguzi.
Kabla hata ya magu CCM ilikua na wanachama wengi, kwanza saaahv ndo wamepungua! fuatilia kipindi cha kina mwinyi, Mkapa na mwanzoni wa Nyerere, kuna kipindi CCM inashinda mpaka kwa asilimia 94%
 
Bombabomba

JF-Expert Member
Dec 23, 2017
1,340
2,000
kabla hata ya magu CCM ilikua na wanachama wengi, kwanza saaahv ndo wamepungua! fuatilia kipindi cha kina mwinyi, mkapa na mwanzoni wa nyerere, kuna kipindi CCM inashinda mpaka kwa asilimia 94%
Kuwa na wanachama wengi sio kushinda uchaguzi ndg.
 
BIN BOR

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,006
1,500
Sasa polisi wa nini kama wanachama ni kweli wanafikia idadi hiyo?
 
peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
3,925
2,000
Kama kwenye data base hii, kuna nape, makamba JR, kinana na Bashiru, mnayo data base nzuri na ya kutegemewa.
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,459
2,000
Eeh bana, umuhimu wa hesabu ndo hapa unahitajika, wale waliosoma MAGAZIJUTO NA, MLINGANYO darasa LA SITA -B, wanaweza kudadavua hii hesabu, hata ukimuita Comrade Pole pole mtaalam wa MAGAZIJUTO anajua Vizuri hii hesabu!

Tanzania ina watu milioni 60, kati ya hao CCM ina wanachama milioni 10, Chadema itabakiwa na wanachama wangapi!

Wale wa darasa la sita B kujeni huku na msahihishiwe,🤣🤣🤣🤣🤣
 
M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,233
2,000
Am sure CCM wanawahesabu hata wale wataozaliwa baadaye kutoka miongoni mwao wenyewe (offsprings kutokana na mbio za mwenge, makongamano ya chama, vikao vya bunge (over 90% ni CCM, so offsprings wake watakuwa CCM), nk, nk).
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,061
2,000
Ni kweli hizo data zipo. Nijuavyo wengi walilazimika kujiunga ndani ya miaka 5 iliyopita kutokana na hali halisi ilivyokuwa. Hasa wanachuo na wapiga deal kwa sababu kila kitu kilihitaji lazima uwe CCM ndipo ufikiriwe utendaji, ualimu, Tarafa nk. Hata sasa hakuna uwezekano wa kuwakwepa. Binafsi nimejiunga rasmi ccm lkn sina matokeo HD uchaguzi
Dikteta aliharibu balaa mifumo yote.
 
Pac the Don

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
974
1,000
kabla hata ya magu ccm ilikua na wanachama wengi, kwanza saaahv ndo wamepungua! fuatilia kipindi cha kina mwinyi, mkapa na mwanzoni wa nyerere, kuna kipindi ccm inashinda mpaka kwa asilimia 94%
Mzee ushindi wa chaguzi nchi hii usiangalie percentage, ni kikundi flan kitaamua nan awe nan asiwe.
 
Fredwash

JF-Expert Member
Oct 27, 2009
856
1,000
Kama tujuavyo kuwa kwenye shughuli ya siasa mtaji ni wanachama, CCM wanadai kuwa wana wanachama hai wapatao milioni 12. Ningetamani kujua na vyama vingine waweke data za wanachama wao hadharani.

Hii itasaidia sana kuwahamasha makada kufanya mapitio ya mipango na mbinu mbalimbali za kuongeza idadi ya wanachama.

Jambo lingine la kufanyika, ni vyema vyama vingine vya siasa vikaja na reforms kubwa sana, zenye kukidhi uwezo sawia wa kuikabili CCM iliyojilimbikizia kila nguvu tajika.

Vinginevyo tutafanya siasa za maigizo mpaka siku ya kiyama.nafikiri kukiwa na tume huru ya kweli ndo tutajua uhalisia wa idadi ya wanachama na wapenz wa hivi vyama vyote kuanzia ccm na wengine..

wanaweza wakawa hai kwa mujibu wa katiba.. c unajua mtaka cha uvunguni.....
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,636
2,000
Sasa hofu ya kushindwa uchaguzi huwa inatoka wapi hadi waombe msaada wa TISS na Polisi?
 
Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
1,369
2,000
Kama tujuavyo kuwa kwenye shughuli ya siasa mtaji ni wanachama, CCM wanadai kuwa wana wanachama hai wapatao milioni 12. Ningetamani kujua na vyama vingine waweke data za wanachama wao hadharani.

Hii itasaidia sana kuwahamasha makada kufanya mapitio ya mipango na mbinu mbalimbali za kuongeza idadi ya wanachama.

Jambo lingine la kufanyika, ni vyema vyama vingine vya siasa vikaja na reforms kubwa sana, zenye kukidhi uwezo sawia wa kuikabili CCM iliyojilimbikizia kila nguvu tajika.

Vinginevyo tutafanya siasa za maigizo mpaka siku ya kiyama.
Hiyo million 12 hata Magufuli bado mwanachama
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom