CCM wacharuana bunge live

kaking81

New Member
Feb 12, 2019
2
7
WANARUDISHA BUNGE LIVE KWA MBINDE

CHAMA cha Mapinduzi na Serikali yao hivi sasa wako kwenye Mvutano mkali kwa kipindi cha Wiki nzima na zaidi, kuhusiana na uamuzi wa kurejesha "Bunge Live" kwa Wananchi.

Viongozi wa CCM wanatoa hoja Vikaoni kwamba; Wabunge wake hawaonekani kwa Wananchi na wanaenda mbali zaidi wanaitetea hoja yao wakisema, Mitaani hakukaliki kutokana na hasira walizonazo Wananchi maana huko Mitaani Wananchi wanaamini kuwa, Serikali ya CCM ndio imewanyima haki hiyo na sasa hivi Nchi nzima Wananchi wanaijadili vibaya sana CCM kuhusiana na suala hili la Bunge kutokuwa Mubashara.

Hao Viongozi wa CCM wanaohudhuria Vikao hivi vizito vinavyofanyikia kwenye lile Jengo lenu wanazitetea hoja hizi kwa kueleza wazi kuwa, hoja ya gharama za uendeshaji" wa Bunge Live kuwa kubwa kama ilivyotolewa wakati wa kufuta utaratibu huo, imewaelemea katika kuitolea ufafanuzi mbele za Wananchi na wanaisihi Serikali iurejeshe ule utaratibu wa mwanzo kwa kile wanachosema kuwa, itakuwa ni ahueni nyingine kwa CCM kuelekea Chaguzi zijazo.

Kwa sasa, hoja ya Bunge Live ni miongoni mwa hoja nzito zinazowasumbua sana CCM na Serikali yao juu ya namna gani wataweza kujinasua, ukiliachilia mbali suala la Tundu Lissu aliyeumizwa vibaya na ameamua kuieleza Dunia 'jinsi' alivyokosa Ushirikiano wa Serikali ya Chama hicho pamoja na kwamba ni Mbunge mwenye Stahiki za Kibunge na alikuwa Rais wa Chama cha Mawakili TLS.

Kuhusiana na hoja hii ya Bunge Live, Serikali kwa upande wao, wanapata kigugumizi sana kuwa wazi juu ya nini wafanye kutokana na kwamba, "Mkuu" wenu bado haridhiki maana shida yake kubwa, hataki Wabunge wa Upinzani waonekane kwa Wananchi, anahisi Wananchi wakiona hoja zao (akina Lema, Bulaya, Heche, Msigwa, Zitto, Mdee, Mnyika na wengine) zitakuwa sumu ya kumharibia Kura za 2020 maana akili yake yote ni jinsi gani ataweza kurudi tena humo Magogoni 2020.

Baadhi ya Watu wa Serikali wanaohudhuria Vikao hivyo wanasema, baadhi ya Wabunge wa Chama chao wanahoji vitu vya ajabu wakiwa Bungeni, hivyo inaweza kuendelea kuwa fedheha kwa Chama hicho kama Wananchi wakiwatazama Mubashara. Mmoja wa Maofisa wa Serikali alitolea Mfano wa Mbunge mmoja Mwanamke kupitia CCM aliyehoji kwa nini Wanaume wasianze kukaguliwa getini kama wametaahiriwa kabla hawajaingia ndani ya Bunge.

Kinachopangwa sasa kuhusiana na suala hili la Bunge Live, ni kuanza kuratibu Propaganda ya kuonyesha kwamba, kuna Watu wanamuomba Rais aingilie kati suala hilo (subirini muone kama hawataahirisha) kisha utaitishwa Mkutano wa wadau wa habari pamoja na Wananchi kama ilivyofanyika kwenye suala la Kikokotoo cha 25% ili Rais akatoe kauli ya kuliomba Bunge kurejesha Bunge Live kwa niaba ya Wananchi.

Baada ya hapo; wadau wote pamoja na Wananchi, imepangwa kuwa; yafanyike Maandamano kila kona ya Nchi kwa ajili ya kumpongeza "Rais" kwa kuliomba Bunge kurejesha Bunge Live la Wananchi na Movie iishie hapo, tusubiri nyingine.

Hizi ndizo Siasa za Matukio. Yaani ni zile Siasa za kutengeneza tatizo mbele za Watu unaowaongoza kisha unarudi tena wewe huyo huyo kulitatua kwa mbinu zile zile ulizopita wakati wa kulianzisha na hao Watu wapige Makofi na kukushangilia tena huku wakikuita Shujaa, Jembe, Mpiganaji ama hata Mtetezi wa Wanyonge.

Kwa mujibu wa taarifa za Vikao hivyo, mambo mengine yanayowasumbulia CCM na Serikali yao akili kuelekea Chaguzi zinazofuata ni pamoja na haya; Mauaji ya Raia wasio na hatia kila wakati na kusiwepo na upelelezi wa kueleweka, kupotea ama kupotezwa kwa Raia, Wanaharakati, Wanahabari, Wanasiasa, Wafanyabiashara n.k. Uchumi wa Nchi kuendelea kudorora Siku hadi Siku.

Suala la Korosho za Watu wa kusini, Kunyimwa Misaada na Mataifa makubwa ya Dunia. Deni la Taifa kuongezeka kwa Kasi ya ajabu kutoka Trillioni 30 hadi Trillioni 60 na zaidi zinazodaiwa sasa.

Mambo mengine ambayo ni tatizo la sasa kwa CCM ni haya; Huduma hovyo ya Maji Vijijini na Mijini, Ahadi ya Millioni 50 kila Kijiji na Kukosekana kwa Ajira.

Francis M. Garatwa,
Diwani na Mwenyekiti wa Chadema Serengeti.
 
Kumbe bunge sio dhaifu tena.....
Na kumbe wabunge wa CCM sio wa kusema ndio tu ila kuhoji na kukataa mabaya
Umeelezea kitu kizuri kwa taifa letu..
 
CCM kuna wazima kiakili wachache sana. Ndio maana tunamwona Nape akianza kukana kuwa siye mhusika wa hoja hiyo wala haikuwa hoja ya bunge. Bunge live yalikuwa maagizo ya moja kwa moja kutokea ikulu.

BUNGE KWA LUGHA RAHISI LILIBAKWA
 
Bunge live litapunguza wakina mama wabunge wa ccm kuomba wabunge wanaume wafanyiwe tohara na kukaguliwa sehemu za siri kuona wenye magovi
 
HATA CCM IFANYE NINI JIWE 2020 ANARUDI KUCHUNGA NGOMBE CHATO
Nani atashindana na ccm? Ikiwa sheria ya vyama vya siasa atai-sign jua hakuna chama kitashiriki uchaguzi wowote, na ikiwa kuna chama kitashiriki najua watakuwa UDP na TLP au CUF ya Lipumba. Nje ya hivyo nitawaona hao watu hawana akili na watakuwa wamelipwa kuhalalisha CCM kuingia madarakani.
Ni ujinga kushiriki uchaguzi wakati lolote wagombea wako watakalo lisema kuhusu CCM na Serikali yao watakuwa wametenda kosa la jinai. wamekatazwa kuisema serikali vibaya, na Hakuna kusema jambo bila kupata taarifa za kitakwimu kutoka NBS, mnafahamu hao ni vibaraka wa CCM. Sasa mtafanyaje siasa bila kuisema Serikali iliyopo madarakani?! Vyama vyote vinahitaji vibali kufanya mikutano isipokuwa CCM wao wanatiririka popote na vyovyote. Majeshi yamepewa mamlaka kulinda serikali iliyopo madarakani, maana viongozi wake wakubwa huteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM. Sasa hivyo vyama vinavyoota uchaguzi kwa mazingira hayo hayo vitakuwa vimehongwa na ccm ili kutoa Baraka kwa ushindi wa asilimia 99.99 utakao patikana.
Unaposema Hatorudi baada ya 2020 niakushangaa sana, Umeisharekebisha malalamiko ya tume ya uchaguzi? Umesharekebisha katiba kuhusu kutangazwa bila kupingwa? Sasa kwanini asirudi?!
 
Nani atashindana na ccm? Ikiwa sharia ya vya,ma vya siasa atai-sign jua hakuna chama kitashiriki uchaguzi wowote, na ikiwa kuna chama kitashiriki najua watakuwa UDP na TLP au CUF ya Lipumba. Nje ya hivyo nitawaona hao watu hawana akili na watakuwa wamelipwa kuhalalisha CCM kuingia madarakani.
Ni ujinga kushiriki uchaguzi wakati lolote wagombea wako watakalo lisema kuhusu CCM na Serikali yao watakuwa wametenda kosa la jinai. wamekatazwa kuisema serikali vibaya, na Hakuna kusema jambo bila kupata taarifa za kitakwimu kutoka NBS, mnafahamu hao ni vibaraka wa CCM. Sasa mtafanyaje siasa bila kuisema Serikali iliyopo madarakani?! Vyama vyote vinahitaji vibali kufanya mikutano isipokuwa CCM wao wantiririka popote na vyovyote. Majeshi yamepewa mamlaka kulinda serikali iliyopo madarakani, maana viongozi wake wakubwa huteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa CCM. Sasa hivyo vyama vinavyoota uchaguzi kwa mazingira hayo hayo vitakuwa vimehongwa na ccm ili kutoa Baraka kwa ushindi wa asilimia 99.99 utakao patikana.
Unaposema Hatorudi baada ya 2020 niakushangaa sana, Umeisharekebisha malalamiko ya tume ya uchaguzi? Umesharekebisha katiba kuhusu kutangazwa bila kupingwa? Sasa kwanini asirudi?!
Mkuu ya mungu ni mengi, hakuna ajuae kesho, kaa hii sheria ya vyama jiwe ataweka signature then hakuna haja ya kushiriki katika uchanguzi, lakini jiwe ataondolewa na mungu pengine kabla ya 2020
 
Back
Top Bottom