Elections 2010 CCM wabanwa vijijini; wamuongezea mzigo JK

Usipoangalia vizuri unaweza ukachanganya udhaifu wa uongozi na kutojiamini.

Ninachokiona mimi ni tofauti tu ya sirka na uwezo wa watendaji wakuu wa CCM wa sasa ukilinganisha na wale wa waliokuwepo kwenye chaguzi zilizopita, ila kimsingi ile hofu na panic ya CCM kama chama ya mwaka 1995 sijaiona kwenye uchaguzi huu.

Uchaguzi wa mwaka 1995 hofu ilikuwepo kwa CCM sababu ya mazoea wa chama kimmoja bila hata mpinzani kutoka chama hicho,kura ya ndio au hapana. Kumbuka ilikuwa ni shindikizo kutoka kwa wafadhili wa nchi za magharibu na wala haikuwa mapenzi ya watawala.Pili njia zilizotumika kumpata mgombea uraisi ziliwakera baadhi ya vigogo waliokuwa wameenguliwa nafasi hiyo,hawakumuunga mkono mgombea uraisi,lakini hawakuwa na wasiwasi na viti vya ubunge Tanzania Bara.Tatu Wasiwasi ya kunyanganywa uongozi wa Zanzibar kwa nyanja zote na chama cha CUF ilikuwa kubwa. Mwaka 2010 mchezo umebadirika, huko Zanzibar watakuwa na serikali ya mseto,wasiwasi umepungua,Huku bara mwanzoni CCM haikuwa na wasiwasi sababu ushindi mkubwa iliokuwa imeupata chaguzi 3 mfululizo kwa muda wa miaka 15. Lakini Bara ya leo imegeuka kuwa Zanzibar ya 1995.Na upeo wa kuelewa mambo wa wapiga kura umeongezeka.
 
Jipeni moyo. Lakini baada ya October 31, kutakuwa na vilio vya kura kuibiwa. Hakuna chama kitakachoshinda uchaguzi kwenye Internet. Nchi ambayo 75% ya wananchi wake hawana umeme, unafikiri kelele za kwenye Internet zinawafikia?

Kwa hiyo mwenzetu you are happy kwa wananchi kukosa umeme, it works for CCM.
 
Unajua huwa najiuliza come october CHADEMA wameshinda,kuna watu watahama nchi seriously.

Ingawa uwezekano wa kuchakachua kura upo kwa sana,ila wasimamizi wa vyama wawe macho tuu bse twataka kama mtu ameshinda ashinde kihalali not otherwise.
 
Haya ni matatizo ya kujua masuala ya kompyuta ukubwani ama kuyajua hivi karibuni. Wengine tulikuwa kwenye stage zenu miaka 15 iliyopita hivyo tunajua vizuri wapi mnaelekea.
Ni mjinga pekee anayefurahia kujua komputa miaka 15 iliyopita wakati bado ni mtumwa wa akili na mwili kwa kuendelea kulamba miguu ya mabwana zake. Kama mtu unafurahia vijijini kukosa umeme hizo zitakuwa akili zako kweli.
 
Nilishasema kuwa wengi wenu mlioingia upinzani uchaguzi huu mpaka majuzi mlikuwa CCM na hii inadhihirisha ninachokisema. You guys are newbies kwenye upinzani hivyo kuwa na fikra za kushinda uchaguzi kwa mbwembwe za kufurika kwenye Internet forum ni normal trend. Mwakani utatoka WARAKA mwengine halafu mtarudi huko huko mlikotokea.

Unaongelea kampeni za kwenye internet wakati watu wanakata mawingu na kuwapa dozi wananchi jinsi wanavyoibiwa na baba zako mafisadi. Ingekuwa ni kampeni za kwenye net usingesikia Kinana analia kuwa CHADEMA wameanza kampeni chafu au TBC wasingekata matangazo Jangwani. Hapa ni JF kaka.
 
Wewe ndiyo endelea kujidanganya kuwa wananchi 75% hawana umeme, endelea kujidanganya kuwa wananchi wa 1995 ni sawa na wa leo, endelea kujidanganya kuwa aliko huko Slaa vijijini anahubiri kwa internet. WanaCCM walio makini wanalielewa hilo hata M/kiti wao amesema wasilale wasiwadharau wapinzani ni wewe tu umebaki kulielewa hilo.

Kuna viashiria vingi tu vinavyoonyesha kuna changes. Leo hii kampeni ya Chadema haina kikundi kimoja cha kampeni kama ilivyokuwa 1995 walivyokuwa wanafuatana wote na Mrema wakiondoka kwenye kijiji hakuna tena chama.

Slaa ana kundi lake Zitto ana kundi lake M/kiti Mbowe ana kundi lake, Makamu m/kiti Said Arfi leo yuko Mpanda anakundi lake, Kamati ya kampeni inayoongozwa na Prof. Baregu ina kundi lake haifuatani na timu ya Slaa. Vile vile Chadema kimeweka wagombea ubunge karibu 80% ya majimbo hiyo yote ni mtaji tosha, unawaweka wananchama jimboni kuwa active wakati wote wa uchaguzi.

Mbali ya makundi hayo kuna vikundi vidogo vidogo kama FOS navyo vina mikakati hiyo hiyo na tayari viko vijijini kwa kazi maalum ya kulinda kura. Sasa unavyosema ni kelele za internet haueleki, ila sisi tupo hapa kukujulisha wewe na mafisadi yanayojiri huko vijijini.

Mkuu asante sana, kwa nyongeza pia tupo hapa kupashana habari tuchangie chama mbadala hata kwa msg kwa kutuma neno CHADEMA kwenda 15710, ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
 
ccm kinaenda kufa, huitaji kuwa na darubini ama uchawi wa shehe Yahya kujua hilo.
ccm watawatumia UWT kwenye mikakati yao, watawatumia wafanya kazi wa serikali kama kinga yao, wanawatumia wanavijiji kama ngome yao.
sasa hao woote wameng'amua kua ccm inawatumia kwa faida yao, wameachia ngazi, wameondoa mapenzi yao kwa Kikwete plus ccm , sasa ccm wanawayawaya, hawajui nani mchawi na mganga.
ccm haina miaka 20 ikiwa madarakani, hawawezi vuka salama wakiwa chama chenye nguvu, hekaheka zao zinaenda kugonga mwamba.
kila aliendani ya ccm hana raha , hana amani, kila mtu kaamua kuishi apendavyo.
wewe watu kama makamba Y, TAMBWE HIZA NDIO VIONGOZI WAO KITAIFA, hiki chama kinaugua Kansa, lazima kitakufa, hakina kinga, miguu imeisha katika , mikono imeoza, shingo tayari imeshambuliwa .
mgonjwa huyu anaishi kwa cocain ili kumpunguzia maumivi.
cccm tutaizika kitambo kifupi, haitaonekana, bora KANU , inaishi , lakini ccm itabaki kwenye mabuku ya historia.
 
lakini kitu kingine ni kuwa.. kwanini inaonekana kama CCM hawajiamini sana mwaka huu kuliko wakati mwingine wowote ule. Hivi wakipoteza viti vingi na urais ukawa matatani wataelezea ni kwa sababu ya kampeni chafu ya chadema au watajua ni kuwa wananchi wametuma ujumbe?
Mkuu, CCM walikuwa wakijiamini sana kabla ya Dr. Slaa hajaamua/kuombwa na chama chake kugombea urais. Walijiamini kwakuwa walikuwa wameshaweka sawa vyama vingine vya upinzani ambavyo huwa vinajitokeza na kusababisha ushindani mkubwa kwa CCM.

Kama unavyoona, vyama vilivyoamua kugombea nafasi ya urais na ambavyo vimekuwa vikigombea mara nyingine zote ni viwili tu hadi sasa. Hivyo alijua tu kuwa hakuwa na haja ya kampeni kubwa. Na ndio maana aliwekewa makisio madogo tu ya siku na umbali wa kampeni zake.

Alipojitokeza Dr. Slaa, wakajua mambo yameharibika kabisa. Na walijua jinsi ambavyo Dr. Slaa anavyokubalika hata kwa baadhi yao na pia katika kundi kubwa la CCM ambao hawapendi ujinga unaofanywa na serikali na au wametengwa katika keki inayopatikana ndani ya CCM hadi sasa. Hivyo wakajua kuna urahisi wa kuumbuka.

Mikakati mingi inaundwa ili kudhoofisha umaarufu wa Dr. Slaa. Ila wananchi wanasema waziwazi kuwa sasa CCM basi.

CCM waliamini kuwa, kama mgombea wa urais hatakuwa na wakati mgumu kuchauliwa, angesaidia kufanya wagombea ubunge wa chama chake kupita bila kupingwa kwa wingi zaidi na au kuchaguliwa hata kama kwa shida. Ila alijua kuwa ataendelea kupata viti vingi bungeni. Sasa hata kujitafutia yeye mwenyewe kura inakuwa shida sana.
 
Nilishasema kuwa wengi wenu mlioingia upinzani uchaguzi huu mpaka majuzi mlikuwa CCM na hii inadhihirisha ninachokisema. You guys are newbies kwenye upinzani hivyo kuwa na fikra za kushinda uchaguzi kwa mbwembwe za kufurika kwenye Internet forum ni normal trend. Mwakani utatoka WARAKA mwengine halafu mtarudi huko huko mlikotokea.
Mkuu, kuna kitu kimoja cha ajabu sana kinachotokea mwaka huu. Kitu hicho ni mageuzi ya kimtazamo ambayo watu wengi wamekuwa nayo. Hakuna mtu anaezungumzia uCCM wake au wa mtu mwingine. Kuna wengi tu hapa ambao wameamua kutoipigia CCM kura kwenye uchaguzi huu bila kuwa wapinzani. Na vile vile, kuna wanaCCM wengi tu ambao wameamua kumpigia Dr. Slaa kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Kwa bahati mbaya CCM inahesabu kura za wote walio na kadi za CCM, bila kujua kuwa hawana mapenzi na wagombea wao. Subiri uone maajabu mwaka huu.
 
Uchaguzi wa mwaka 1995 hofu ilikuwepo kwa CCM sababu ya mazoea wa chama kimmoja bila hata mpinzani kutoka chama hicho,lakini hawakuwa na wasiwasi na viti vya ubunge Tanzania Bara.Tatu Wasiwasi ya kunyanganywa uongozi wa Zanzibar kwa nyanja zote na chama cha CUF ilikuwa kubwa. Mwaka 2010 mchezo umebadirika, huko Zanzibar watakuwa na serikali ya mseto,wasiwasi umepungua,Huku bara mwanzoni CCM haikuwa na wasiwasi sababu ushindi mkubwa iliokuwa imeupata chaguzi 3 mfululizo kwa muda wa miaka 15. Lakini Bara ya leo imegeuka kuwa Zanzibar ya 1995.Na upeo wa kuelewa mambo wa wapiga kura umeongezeka.

Sijajua basis ya hii analysis mnaitoa wapi.

Mwaka 1995 CCM ilikuwa na hofu kubwa ya kupoteza kiti cha uraisi na theruthi mbili ya wabunge na reality on ground ilikuwa ni ya kukatisha tamaa sana kutokana na uungwaji mkono mkubwa aliokuwa nao mgombea wa NCCR- Mageuzi.

Katika uchaguzi wa mwaka huu bado sijaona ata nusu ya uungwaji mkono ule wa NCCR mwaka 1995, mwaka huu CCM haina hofu ya kushindwa uraisi wala haina hofu ya kukosa theruthi mbili ya viti vya ubunge, sasa hiyo hofu mnaiona wapi wakuu? let's be realistic!!
 
Muulize bosi wako kwa nini ameongeza siku za kampeni kwanini anaruhusu siasa za maji taka bila kukemea, otherwise endelea kulala mwambie na bosi wako arudi dar alale akione cha mtema kuni.
 
Muulize bosi wako kwa nini ameongeza siku za kampeni kwanini anaruhusu siasa za maji taka bila kukemea, otherwise endelea kulala mwambie na bosi wako arudi dar alale akione cha mtema kuni.

Ukishazoea upambe sikuzote utadhani kila mtu nae ni mpambe, kaazi kwelikweli!!

Ushauri wa bure...jitahidi kuyasoma mazingira ya kisiasa yaliyopo na uungwaji mkono wa wagombea waliopo sehemu mbalimbali nchini kisha toa tathmini kutokana na reality unayoiona on ground bila kuingiza ushabiki wako binafsi.

Kwa kuanzia nitajie mikoa 5 tu kati ya 32 ambayo mgombea wa urasi wa Chadema anauhakika wa kushinda? na mikoa ambayo ana uhakika wakutoa wabunge wengi kuliko CCM?

Utoaji wa tathmini za kishabiki na kisha kuziamini ndiko kunakofanya kila baada ya uchaguzi tuanze kusingizia uchakachuaji ata pasipopaswa.
 
ccm haina miaka 20 ikiwa madarakani, hawawezi vuka salama wakiwa chama chenye nguvu, hekaheka zao zinaenda kugonga mwamba.

wewe watu kama makamba Y, TAMBWE HIZA NDIO VIONGOZI WAO KITAIFA, hiki chama kinaugua Kansa, lazima kitakufa, hakina kinga, miguu imeisha katika , mikono imeoza, shingo tayari imeshambuliwa .
mgonjwa huyu anaishi kwa cocain ili kumpunguzia maumivi.
cccm tutaizika kitambo kifupi

Nakubaliana na wewe katika haya.
 
Ukishazoea upambe sikuzote utadhani kila mtu nae ni mpambe, kaazi kwelikweli!!

Ushauri wa bure...jitahidi kuyasoma mazingira ya kisiasa yaliyopo na uungwaji mkono wa wagombea waliopo sehemu mbalimbali nchini kisha toa tathmini kutokana na reality unayoiona on ground bila kuingiza ushabiki wako binafsi.

Kwa kuanzia nitajie mikoa 5 tu kati ya 32 ambayo mgombea wa urasi wa Chadema anauhakika wa kushinda? na mikoa ambayo ana uhakika wakutoa wabunge wengi kuliko CCM?

Utoaji wa tathmini za kishabiki na kisha kuziamini ndiko kunakofanya kila baada ya uchaguzi tuanze kusingizia uchakachuaji ata pasipopaswa.

All in all, CCM itaendelea kubaki madarakani Unless mimi na wewe tuna uhakika wa Kupiga Kura, kwa sababu nimegundua watu wengi huwa wanashabikia sana mageuzi, ukipita huko maofisini people are talking about Slaa, lakini kati ya wafanyakazi saba inawezekana mmoja tu ndiye atakayepiga kura. Hatuwezi tukatarajia Mabadiliko ambayo mimi na wewe hatuko tayari kushiri kuyaleta
 
"Kutaraji, Kutamani, Kuzungumzia, Kupenda Mabadiliko pasipo kupenda kushiriki katika kuyaleta ni Unafiki Mkubwa" NyU 2010
 
Ukishazoea upambe sikuzote utadhani kila mtu nae ni mpambe, kaazi kwelikweli!!

Ushauri wa bure...jitahidi kuyasoma mazingira ya kisiasa yaliyopo na uungwaji mkono wa wagombea waliopo sehemu mbalimbali nchini kisha toa tathmini kutokana na reality unayoiona on ground bila kuingiza ushabiki wako binafsi.

Kwa kuanzia nitajie mikoa 5 tu kati ya 32 ambayo mgombea wa urasi wa Chadema anauhakika wa kushinda? na mikoa ambayo ana uhakika wakutoa wabunge wengi kuliko CCM?

Utoaji wa tathmini za kishabiki na kisha kuziamini ndiko kunakofanya kila baada ya uchaguzi tuanze kusingizia uchakachuaji ata pasipopaswa.
Ndiyo maana nimekwambia kama CCM wanauhakika wa kushinda mwambie Kikwete akapumzike dar si anaumwa kwanini ahangaike hivyo. Kwa hali ilivyo sasa ni tofauti na chaguzi zilizopita hakuna chama chenye uhakika 100%.
 
Mkuu hivi upo kweli hapa nchini? unajua sometimes upenzi ukizidi inakuwa ni vigumu sana kuiona hali halisi, ukiona chama cha upinzani hakina mikoa ambayo ni ngome yake, ujue kazi bado ni mbichi kabisa...

Kwa kuanzia nitajie mikoa 5 tu kati ya 32 ambayo mgombea wa urasi wa Chadema anauhakika wa kushinda? na mikoa ambayo ana uhakika wakutoa wabunge wengi kuliko CCM?a.
 
Mkuu hivi upo kweli hapa nchini? unajua sometimes upenzi ukizidi inakuwa ni vigumu sana kuiona hali halisi, ukiona chama cha upinzani hakina mikoa ambayo ni ngome yake, ujue kazi bado ni mbichi kabisa...
Kwa hiyo CCM haina kazi.
 
Wewe ndiyo endelea kujidanganya kuwa wananchi 75% hawana umeme, endelea kujidanganya kuwa wananchi wa 1995 ni sawa na wa leo, endelea kujidanganya kuwa aliko huko Slaa vijijini anahubiri kwa internet. WanaCCM walio makini wanalielewa hilo hata M/kiti wao amesema wasilale wasiwadharau wapinzani ni wewe tu umebaki kulielewa hilo.

Kuna viashiria vingi tu vinavyoonyesha kuna changes. Leo hii kampeni ya Chadema haina kikundi kimoja cha kampeni kama ilivyokuwa 1995 walivyokuwa wanafuatana wote na Mrema wakiondoka kwenye kijiji hakuna tena chama.

Slaa ana kundi lake Zitto ana kundi lake M/kiti Mbowe ana kundi lake, Makamu m/kiti Said Arfi leo yuko Mpanda anakundi lake, Kamati ya kampeni inayoongozwa na Prof. Baregu ina kundi lake haifuatani na timu ya Slaa. Vile vile Chadema kimeweka wagombea ubunge karibu 80% ya majimbo hiyo yote ni mtaji tosha, unawaweka wananchama jimboni kuwa active wakati wote wa uchaguzi.

Mbali ya makundi hayo kuna vikundi vidogo vidogo kama FOS navyo vina mikakati hiyo hiyo na tayari viko vijijini kwa kazi maalum ya kulinda kura. Sasa unavyosema ni kelele za internet haueleki, ila sisi tupo hapa kukujulisha wewe na mafisadi yanayojiri huko vijijini.
achilia mbali sms zinavyosambazwa.............
 
mtaji mkubwa wa ccm upo vijijini kama upinzani wanataka kura za ccm labda wajaribu mjini ,vijijini wataumbuka ningewashauri ule mkakati wa kuwarudisha vijana shuleni kwa wapangia vyumba mijini uwe endelevu kwa sababu wanafunzi wengi saa hizi mpunga umepungua hivi kutuleta hapa mjini tutafurahi sana na siku ikifika tutachukua tutaweka waa!!! JK apewe ushindi kwanini ?

1. Yote aliyoagiza Baba wa Taifa ametekeleza

2.Ilani ya Chama cha Mapinduzi imetelelezwa kama: barabara, maji, umeme, shule, hospitali, uwekezaji , hapo ndugu zangu wa Kigoma mpo!!!

3. Nchi imendelea kuwa yenye amani na utulivu na kuwawezesha watu wengi nje na ndani ya Afrika kuja kuwekeza Tanzania.

4. Ni katika kipindi cha JK vyombo vya habari vimepewa uhuru wote ndio maana hata wewe unaweza kusema chochote kile.

5. Ni katika kipindi cha JK hajawaonea hajawaonea haya mafisadi na vyombo vya sheria vinaendelea na kazi yake katika kulinda mihimili mitatu ya uongozi - tuwaachie mahakama .

JK ENDELEA NA KAZI TUPO PAMOJA ASIKUTISHE MTU ccm juu!!!
 
Back
Top Bottom