CCM wabanwa vijijini; wamuongezea mzigo JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wabanwa vijijini; wamuongezea mzigo JK

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  (Mwananchi) CHAMA cha Mapinduzi(CCM), kimebadili ratiba za kampeni kwa mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete na sasa atafanya kampeni bila kupumzika tofauti na awali alipopangiwa siku za kupumzika.Agosti 20 mwaka huu, meneja wa kampeni wa CCM Abdulrahman Kinana katika mkutano wake na wahariri wa vyombo vya habari, alitangaza kuwa mgombea huyo wa urais atakuwa na siku 16 za kupumzika kati ya siku 68 za kampeni.

  Kwa mujibu wa Kinana, Kikwete alipangiwa kufanya kampeni kwa siku 52 badala ya 68 na pia kupunguziwa uchovu wa safari kwa kuondolewa kilometa 58,000 ambazo angetumia kusafiri kwa barabara. CCM iliamua atumie pia helkopta kwa kampeni zake.

  Katika kampeni zake kuwania urais mwaka 2005 kumbukumbu zinaonyesha kuwa Kikwete alisafiri kilometa 96,000 kwa barabara, na mwaka huu alipangiwa kusafiri kilometa 38,000 kwa barabara huku umbali uliosalia akipangiwa kutumia helkopta ili kumpunguzia uchovu.
  Lakini habari kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya CCM zinasema kuwa hatua ya chama hicho kuondoa siku za mapumziko kwa mgombea wake huyo wa urais, imekuja ili kukabiliana na upepo wa kisiasa ulivyo kwa sasa.

  Vyanzo hivyo vimefafanua kwamba CCM imepokea taarifa za kiupelelezi zinazoonyesha kuwa iwapo Kikwete ataendelea na mfumo wa kampeni anaoutumia sasa wa kujipa siku za mapumziko, anaweza kupunguza kiwango cha kura anazotarajia kupata kumwezesha kuwa tena rais katika uchaguzi mkuu ujao, Oktoba 31.

  "CCM imeamua kubadili mfumo wa kampeni za Kikwete... sasa hatapumzika kama alivyopangiwa awali, atafanya kampeni kila siku kwa siku zilizosalia," alieleza mpashaji wetuo.

  Wapashaji habari hao walilidokeza gazeti hili kuwa taarifa ilizonazo zinaonyesha kuwa kuna wagombea urais wawili wa vyama tofauti ambao hadi sasa wameonyesha ushindani dhidi ya CCM, hali ambayo imekishtua chama hicho tawala na kuamua kuongeza nguvu katika kampeni zake kwa lengo la kulinda "ushindi wa kishindo".

  Wagombea hao wametajwa kuwa ni Dk Willbrod Slaa wa Chadema na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF wanaoelezewa kufikisha kampeni zao hadi vijijini hivyo kuwa na uwezekano wa kupata idadi kubwa ya kura.

  Katibu mkuu wa CCM, Yusuph Makamba hakupatikana jana kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo, lakini katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, John Chiligati hakutaka kuzungumzia suala hilo.

  Badala yake alisema: " Sasaa, ahh, hilo muulize mheshimiwa Kinana , mimi nipo jimboni Manyoni natafuta kura za CCM; napambana; anayetoa taarifa zote kitaifa kuhusu kampeni za uchaguzi za CCM ni Kinana."

  Lakini Kinana alisema: " Si kweli, kuna siku chache ambazo ni lazima apumzike."

  Alipoelezwa zaidi kuhusu lengo la kumwondolea Kikwete mapumziko, meneja huyo wa kampeni wa CCM alisema: "Haiwezekani akafanya kampeni siku zote bila mapumziko. Kama binadamu Kikwete lazima apumzike, bila kusahau huyu bwana (Kikwete) pia ni rais, lazima apumzike siku chache awepo pia ofisini, lazima arudi Dar kwa ajili ya kazi za ofisi."

  Bila kufafanua zaidi Kinana aliongeza kuwa hata ikiwa wagombea wa upinzani wanafanya kampeni zao kwa nguvu kubwa sasa, siku zijazo watakwama na hawataifikia CCM hivyo kutoitia hofu ya kukosa ushindi wa kishindo.

  Kikwete alipata ushindi wa kishindo mwaka 2005 wakati alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza baada ya kunyakua zaidi ya asilimia 90 ya kura zote, lakini mwamko wa wananchi katika miaka ya karibuni na kuzidi kuimarika kwa vyama vya upinzani kunaonekana kunaweza kuondoa uwezo wa CCM kurudia rekodi hiyo.

  My Take:

  Kwanza, si kweli JK alishinda kwa zaidi ya kura asilimia 90!.. ilikuwa a little over 80 percent..

  Pili, mkakati wa chadema kutengeneza dent vijijini unaanza kuzaa matunda..

  Tatu, Chadema wanaonekana kutumia mbinu za kumdhoofisha adui at his strongest point (vijijini).. Kwa hiyo tuangalie adjustment ya CCM itakuwaje.. maana baada ya madongo ya uchafu kuisha itabidi warudi kwenye hoja tu ambazo bado zinawasubiri.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hivi mwandishi alikuwa na lengo gani kuandika JK alishinda 2005 zaidi ya asilimia 90 wakati ukweli ni kwamba alishinda kwa asilimia 82?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nadhani na yeye (mwandishi) ni miongoni mwa watu wanaoamini bila kuchukua muda kuangalia kilichofanyika.
   
 4. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  the ccm, the conspiracy group in the world, so take care everyone when you meet them, true is so dangerous pipo
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Juzi juzi nilimuuliza rafiki yangu mmoja hivi ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi, "Mbona mmnaonekana kama mmenunuliwa na CCM"
  akajibu kwa kifupi tu "CCM wamejipanga bwana".
  Haiwezekani kwa mwandishi makini wa nchi hii kusahau (kutujua) kama Kikwete hakushinda kwa asilimia 90 mwaka 2005.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  lakini kitu kingine ni kuwa.. kwanini inaonekana kama CCM hawajiamini sana mwaka huu kuliko wakati mwingine wowote ule. Hivi wakipoteza viti vingi na urais ukawa matatani wataelezea ni kwa sababu ya kampeni chafu ya chadema au watajua ni kuwa wananchi wametuma ujumbe?
   
 7. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mkuu CCM walikuwa wanajiamini sana, hasa kabla ya Slaa kutangaza nia, Ukiangalia zile mbwembwe za Dodoma utaona kabisa hawa jamaa walikuwa wanashangilia Ushindi wa Kishindo, JK alikuwa ni mwenye kujiamini sana, sasa hili la Slaa limekuja kama Vile Bondia ambaye Ulikuwa unakaribia kumtwanga kwa knock out halafu dakika za Mwisho akakupiga Ngumi ya Pua au Korodani ghafla
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mzee na wewe unaamini kabisa kwamba CHADEMA wanafanya kampeni chafu?

  Nina uhakika kwamba CCM wanajua madudu yao, kwa hiyo itakuwa ujumbe kwao kwamba sasa wananchi wameamka. Lakini hilo somo haliwezi kueleweka kirahisi kwa kuwa Top Brass wote wako pale kulinda maslahi yao na kuendeleza ufisadi.

  Kama CCM itapoteza viti vingi vya ubunge inaweza kuwa mwanzo kusambaratika kwa CCM kuwa nina uhakika wapo ambao watapoteza ubunge kwa sababu chama chake ni kichafu na uongozi haufanyi lolote kukemea huo uozo.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  ninapozungumzia kampeni chafu nazungumzia kile ambacho CCM wataona kuwa chadema imeng'ang'ania kuihusisha CCM na kashfa za ufisadi n.k kwa CCM hiyo inaonekana ni kampeni chafu.
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Ndege ya economy, sidhani kama CCM hawakujua kuwa mwaka huu watasimama na Dr.Slaa.
  Hilo lilikuwa linajulikana mapema sana.
  Mfano humu JF tulikuwa tunajuwa tangu awali sembuse CCM wasiwe na taharifa!
   
 11. Y

  Yasebhase Member

  #11
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Saa hizi Jamaa (JK) yuko zake Serengeti- BililaH anapumzika.
   
 12. Zungu la Unga

  Zungu la Unga Member

  #12
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jipeni moyo. Lakini baada ya October 31, kutakuwa na vilio vya kura kuibiwa. Hakuna chama kitakachoshinda uchaguzi kwenye Internet. Nchi ambayo 75% ya wananchi wake hawana umeme, unafikiri kelele za kwenye Internet zinawafikia?
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  ni kweli kelele za internet haziwafikii but kelele za mafisadi zinawaingia moyoni!!!!! Subiria 31 October
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Sep 8, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji ni kweli CCM hawajiamini si kwa sababu watapoteza nafasi ya kutawala la, hili haliwapi shida wasiwasi wao upo kwenye mambo yafuatayo

  1. Wajua wazi kuwa wamekuwa wakibadili matokeo ya uchaguzi kwa nguvu pale ambapo walishindwa. Sasa kwa jinsi Dr Slaa et al wanavyoweza kuwafikia watu wengi zaidi inawajengea potential ya kuwa na peoples' power na kukabiliana na uhuni CCM iliyozoea kuufanya kuwa kuzima will of the people.

  2. Kilichotokea Kenya baada ya uchaguzi wanajua fika kuwa kuna high potential ya kutokea hapa Tanzania kama tu wapinzani watawaelimisha wananchi vya kutosha juu ya kuhakikisha sauti zao katika kutaka nani awaongoze hazizimwi kwa kisingizio chochote.

  3. CCM wanajua kuwa ili uchaguzi uwe wa amani wanatakiwa kuonekana wanatenda haki katika kutangaza matokeo halali ya kura za wananchi, na kama ni hivyo basi ni lazima waongeze juhudi katika kuzipigania kura halali, vinginevyo watapata tabu katika kutawala.

  Kwa ujumla wasiwasi wao ni kuamka kwa watanzania baada ya kudanganywa uchaguzi baada ya uchaguzi baada ya uchaguzi na wasio walichoahidiwa na watu wale wale wa chama kilekile kwa sera zilezile. Mwamko huu haujulikana kama utapeleka kwenye wananchi kuingia mitaani au la baada ya matarajio yao waliowachagua kuwekwa kapuni na kupewa wasiowachagua kuwa viongozi wao.
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu jingine kubwa is just an EGO of Kikwete, mgombea aliyeshinda by 80% in 2005 and just after 5 yrs anaogelea almost chini ya 50%
   
 16. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #16
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Asije aka-colapse tena........
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Potential ipo na tena ni kubwa sana. CCM wameishajionea wenyewe wakati wa kura za maoni. Action za wapiga kura zilikuwa ziko loud and clear, na pale haki ilipofinywa, wapiga wameonyesha hasira zao kwa uwazi. Sehemu zote ambazo CC na NEC walichakachua matokeo, moto una wawakia CCM na hawajui watauzima vipi. Maana wapiga kura wao wamehamia upinzani na huko ndiko wataenda kuongeza mwamko.

  Siku Mwakalebela anapelekwa mahakamani, sina hakika kama mtu alienda kuwaita watu waliofurika mahakamani kusikiliza kesi. Huo mwamko nina hakika kwamba utaendelea na tuombe Mungu wananchi wawe na ujasiri wa kulinda kura zao mpaka dakika ya mwisho hata kama watatishwa na polisi.

  Sasa hivi UWT wanakusanya data kuona ni majimbo gani kuna upinzani mkali ili kuona namna ya kutumia polisi ili ku-suppress upinzani na ikiwezekana kuongeza idadi ya polisi wengi kwenye hayo majimbo ili kufanikisha uchakachuaji wa matokeo.
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe hapa kwenye internet unatafuta nini? toka hapa nenda wacha sisi tukae hapa na mikakati yetu uone kama sisi m mtaona kitu.
   
 19. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #19
  Sep 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe ndiyo endelea kujidanganya kuwa wananchi 75% hawana umeme, endelea kujidanganya kuwa wananchi wa 1995 ni sawa na wa leo, endelea kujidanganya kuwa aliko huko Slaa vijijini anahubiri kwa internet. WanaCCM walio makini wanalielewa hilo hata M/kiti wao amesema wasilale wasiwadharau wapinzani ni wewe tu umebaki kulielewa hilo.

  Kuna viashiria vingi tu vinavyoonyesha kuna changes. Leo hii kampeni ya Chadema haina kikundi kimoja cha kampeni kama ilivyokuwa 1995 walivyokuwa wanafuatana wote na Mrema wakiondoka kwenye kijiji hakuna tena chama.

  Slaa ana kundi lake Zitto ana kundi lake M/kiti Mbowe ana kundi lake, Makamu m/kiti Said Arfi leo yuko Mpanda anakundi lake, Kamati ya kampeni inayoongozwa na Prof. Baregu ina kundi lake haifuatani na timu ya Slaa. Vile vile Chadema kimeweka wagombea ubunge karibu 80% ya majimbo hiyo yote ni mtaji tosha, unawaweka wananchama jimboni kuwa active wakati wote wa uchaguzi.

  Mbali ya makundi hayo kuna vikundi vidogo vidogo kama FOS navyo vina mikakati hiyo hiyo na tayari viko vijijini kwa kazi maalum ya kulinda kura. Sasa unavyosema ni kelele za internet haueleki, ila sisi tupo hapa kukujulisha wewe na mafisadi yanayojiri huko vijijini.
   
 20. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #20
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Unachokiandika ni habari njema kwa watanzania kwani inaonyesha kuwa jamii imekuwa na mwamko ila mkuu nakushauri usiweke hapa sana mikakati ya chama chenu maana kuna mamluki wa sisiem wanakuja huku kuchota data na kusaidia chama chao kupanga mikakati. Aliyelala usimwambushe!
   
Loading...