pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,636
- 6,261
Kwa mwenendo ambao unaonekana CCM wanajilazimisha kuwa wapo wamoja jambo ambalo siyo kweli. Na hii inatokea kwa sababu mwenyekiti anaonekana Kama mungu ndani ya chama na hakosei kwa sababu katiba ya CCM inampa mamlaka ya kuwa mungu mtu.
Pia katiba hii iliyopo imepitwa na wakati imempa Rais mamlaka kiasi kwamba Hakuna mhimili mwenye mamlaka kuhoji hata akifanya ujinga.
Bunge linaweza kumwondoa Rais madarakani, Rais anaweza kulivunja Bunge, sasa basi Bunge likimuondoa Rais madarakani anabaki na cheo cha mwenyekiti wa chama hao wabunge waliomuondoa madarakani mwenyekiti ataitisha kikao na atawafukuza wote chamani na wao ubunge wao utaishia hapo.
Rais anaweza kulivunja Bunge na akateua watu wake kuwa wabunge kupitia uenyekiti wake.
Watanzania siyo madikteta lakini CCM wametengeneza udikteta wenyewe na haifiki 2025 hawajaanza kutwangana wao kwa wao.
Kwa sasa wana Vita ya maneno hii Vita itahamia kwenye vita kamili.