CCM vurugu tupu - Katibu CCM Mwanza ataka Nape na wenzake wapigwe stop | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM vurugu tupu - Katibu CCM Mwanza ataka Nape na wenzake wapigwe stop

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 29, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kundya ataka Nape,wenzake wapigwe 'stop'
  KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza,Rajabu Kundya, amesema ziara zinazofanywa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nape Nnauye na wenzake katika mikoa mbalimbali nchini, zinapingana na taratibu za CCM.

  Kundya pia amesema kitendo cha viongozi hao kuwataja majina baadhi ya wanachama wanaotuhumiwa kwa mambo mbalimbali kinaleta mgawanyiko mkubwa ndani ya chama hicho kinachotawala.

  Katika zira hizo mikoani, Nape amekuwa akifuatana na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na wengine kadhaa.Akizungumza katika mahojiano maalum jana katibu huyo wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, alisema ingawa ziara kama hizo zingeweza kusaidia kuimarisha chama, lakini kutaja majina ya watu na kuwashutumu si sehemu ya kuimarisha chama bali kukibomoa.

  "Kama kuna mtu ambaye wanadhani ana tatizo kubwa ndani ya chama, utaratibu upo na wala si busara kumtaja katika mikutano ya hadhara, hili ni la kulisemea ndani ya vikao," alisema Kundya.Alisema taratibu za kusema zipo na zinatoa nafasi kwa mwananchama yeyote kuzungumza na hata kuwasema wenzake kupitia njia za vika ndani ya chama.

  Mtendaji huyo alisema kinachokifanywa na Nape na wenzake hasa kuwasema hadharani viongozi wanaotakiwa kujivua magamba, ni kukiuka taratibu. Alisema hata hiyo jambo hilo analiacha mikononi mwa chama, ili kiangalie namna ya kuwazuia viongozi hao ili wasiendelee kuvunja taratibu.

  Kwa kauli hiyo katibu huyo atakuwa anaungana na wenyeviti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja na Mkoa wa Dar es salaam John Guninita waliojitokeza kuwakosoa makada hao wa CCM.

  Mwananchi
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haya, hehehehe la kuvunda halina ubani
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Lukuvi yuko wapi - aombe mwongozo haraka maana inaelekea Nape analeta uchochezi!!!
   
 4. M

  MPG JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha magamba CCM hakina tena ridhaa ya kuongoza watanzania,kimepoteza sifa,badala ya kutatua matatizo ya wananchi kipo kulumbana
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Lukuvi mwongozo ni kwa wapinzani
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Warioba alishasema, badala ya kujenga nchi baada ya uchaguzi magamba yapo kwenye kampeni za urai 215, sasa ni ushindani kati ya CCM na CCJ
   
 7. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wanatumia pesa nyingi sana, badala ya kutumia hizo pesa kuanzisha miradi ya maana! utakuta miradi mingine haina pesa. Anyway, acha waendelee hivo hivyo ili kazi iendelee kuwa rahisi hapo mbeleni.
   
 8. r

  raffiki Senior Member

  #8
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He....watani zangu awa wasukuma bwana taabu kweli.......!Shinyanga mwenyekiti anapinga inayoitwa CCM-CCJ, mwanza nako tena..-mh mhhh....wenzao wa nyanda za juu wanaunda mtandao kumuingiza mtu ikulu 2015, wa kaskazini nao wako busy kutafuta upenyo wa kuweka mtu round ya 2015, watu wa pwani nao hawapo nyuma vivyo hivyo hadi mtwara lindi huko...sasaaa hawa watani zangu wa kanda ya ziwa ambao ndio wapo wengiii wanabakia kuwa washabiki tu wa kambi hizo au kuzipinga pasipo faida wala lengo lolote ambao....labda ndio maana Mhe. wao mmoja ameamua kukumbilia kwenye kambi ya nyanda za juu, watu wako busy kutafuta maisha ya baada ya 2015..sahivi ndo ishotoka hiyo...ohh ohhh watani wangu kanda ya ziwa changamkeni mjinjengee na nyie msingi wa utawala mtabakia kuwa wasindikizaji tuuu...-tena mna kifaa kinaweza kuwatoa kipo mabarabarani juzi nimekuta kinataka kubomoa nyumba pembezoni mwa barabara.......2015 inakuja ohhh ohhhh
   
 9. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  CCM imepoteza dira.
  Viongozi wake wamebaki kuviziana na kuropokeana.
  R.I.P CCM.
   
 10. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  njoo cdm tupige kazi, acha kupiga kelele huko huko
   
 11. V

  Vonix JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,987
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Teh-teh-teh-teh ukiona ndugu wanagombana chukua jembe ukalime naenda chanikaaaaa kuvuna machungwa karibuni.
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Wewe usicheze na siasa za shinyanga na mwanza acha kabisa.Kinachoeleweka shinyanga na Mwanza ni kwamba DR.slaa ndiyo rais ajaye, wasukuma hawana haja na siasa uchwara walishaamua 2015 ni Dr.slaa wabunge wote watakuwa wa CDM.Hili liko wazi hata kwa CCM mkoa SHY-MWZ.CCM hawana chao lake zone hata wana-CCM walioko huko hawako tayari kukiunga mkono chama chao CCM, wataishia kunawa
   
 13. r

  raffiki Senior Member

  #13
  Jul 29, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukimanisha wananchi nakubaliana na wewe ndugu yangu..lakini nilicho judge mie ni CCM kanda ya ziwa wao ka bado wapo CCM kwanini walumbane juu ya matayarisho ya kanda zingine???????????wakati wao wako wengi na wana watu safi pia...pengine ndio imefanya wananchi wa mikoa hiyo wamezamia CDM maana wanaona viongozi wao wazuri hawatendewi haki.......!HAPA tusidanganyane kwa siasa ooh sio za ukanda wala udini, upuuzi mtupu kusimbua wananchi tu..ukanda na ukabila upo sana tu....tena huwa nacheka sanaaaaa pale watu wanavyo mnukuu baba wa taifa kwa udini na ukabila tu...tena wengine wanaenda mbali nakuchangia au kunena kama sio kujenga hoja.... oohh.. baba wa taifa alikataa makabila makubwa kama wanavyoyaita kuwa ni wachaga, wanyakusa na wasukuma...hayapaswi kushika dola....HUWA NAJIULIZA BABA HUYO HOYO WA TAIFA ALIKATAA RUSHWA NA AKASISITIZWA VIONGOZI WATOKANE NA UWEZO WAO WA KUWATUMIKIA WANANCHI....sasa mbona hilo halitekelezwi zaidi ujanja ujanja tuu unatumiwa na wajanja wachache kutumia baadhi ya matamshi ya BABA wa TAIFa kujitafutia uongozi....Kanda ya ziwa nao wachangamkie huu ujanja ujanja hoja yangu ndo hiyo kakaaaa siasa mtajiiii ohooooo hata chadema huoni wanavyochangamka bungeni ni mtaji tu huo kakakakakakakaaaaa
   
 14. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  R.I.P Magamba.....
   
 15. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #15
  Jul 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mizunguko ya Nape kwa nchi nzima haina tija zaidi ya kuchezea pesa ambazo wangeweza hata kununua madawati. Nape si mtu makini zaidi ya kufanya ushabiki na kueneza propaganda za chuki dhidi ya wapenda maendeleo.
   
Loading...