CCM vs CHADEMA: Ali Mufuruki amaliza kabisa

Jamar Said

Member
Sep 2, 2015
19
35
Ningependa kutoa wito kwa watu wote wenye nia njema na wazalendo kuacha kukaa pembeni na kulalamika na badala yake kujihusisha moja kwa moja katika kuibadili CCM na uongozi wake, kuweza kutoa uongozi thabiti na wa kuwajibika kwa nchi yetu. Ujenzi wa taifa huwa ni jambo gumu na kazi hii inaweza kushindwa kutekelezwa licha ya nia njema na jitihada za nyuvu. Inahitaji bidii na subira.

Kizazi chetu kitaweza kuchangia kiasi fulani katika kazi hii njema na vizazi vijavyo labda vitaendeleza kujenga juu ya tuliyoacha nyuma.

Nina mitazamo miwili ya mustakbali wa nchi yetu baada ya uchaguzi wa Jumapili na yote inahitaji ushiriki wetu sote kikamilifu na kwa ufanisi katika kuipeleka nchi yetu mbele.

Mtizamo wa kwanza ni ule wa Magufuli kuibuka mshindi baada ya uchaguzi wa uraisi na kuchukua uongozi wa chama ndani ya miezi 6.

Magufuli ameshatangaza nia ya kukigeuza Chama cha Mapinduzi na kukirudisha katika misingi yake ya kiitikadi na kukijenga upya. Hataweza kufanya haya yote peke yake na ndio hapo sote tunahitajika kuwa tayari kumsaidia.

Mtazamo wa pili ni ule wa Lowassa kuibuka mshindi baada ya uchaguzi, jambo ambalo litatupelekea kama nchi katika wakati mgumu na usiotabirika kwa sababu nyingi.

Kwanza kabisa CHADEMA imepoteza misingi yake ya kiitikadi na hasa msimamo wake wa kupinga ufisadi, inaongozwa na kundi la watu wasio na maadili wala uzalendo, ambao nia yao ni kujitajirisha binafsi na kukwepa mkondo wa haki na sheria kwa madhambi yao ya nyuma.-

Na endapo CCM itashindwa, itakabiliwa na tishio la sintofahamu kuhusu kuwepo kwake kama tulivyoona kwa vyama vya uhuru vilivyotawala muda mrefu ( kama KANU, UNIP, MPC n.k) vilipopoteza madaraka.
Ukweli usiokwepeka ni kwamba kuiacha CHADEMA ikatawala peke yake kwa zaidi ya miaka mitano itaashiria maafa makubwa yasiyosemeka kwa nchi hii na watu wake.

Hivyo basi itabidi Watanzania wazalendo wenye nia njema wakunje mikono ya shati na kushiriki kikamilifu katika kukijenga upya na kukiimarisha chama cha CCM ili kiwe tayari kutawala wakati tukuiingia tena katika mchakato wa uchaguzi-- mwaka 2020.

Ushindi wa CHADEMA unatia wasi wasi zaidi kwa sababu ya idadi na ukubwa wa madhara yanayoambatana na ushindi huu.

Moja ni kwamba Lowassa ameahidi kuunda mfumo wa serikali 3 ndani ya siku 100 na sidhani kama uelewa wake kuhusu serikali hizi 3 ni kama ulioainishwa na Kamisheni ya Warioba.

Sote tunajua umuhimu wa muungano wetu na Zanzibar katika kuwepo kwa amani na utulivu katika sehemu hii ya bara letu la Afrika na tunafahamu fika athari za kutengua muungano bila kufuata taratibu za kikatiba.

Mwenyezi Mungu atunusuru na matokeo haya, Amina.

Madhara mengine- yanaweza kutokea iwapo afya ya Lowassa itaporomoka kufikia kiasi cha yeye kushindwa kutawala nchi. Hayo yakitokea, chini ya Katiba iliyopo, urais- utashikwa na Makamu wa Rais Duni Haji Duni, mwanachama mamluki wa CHADEMA, mwanachama mwanzilishi wa CUF na mhafidhina wa siasa za kupinga muungano.

Na hata Lowassa akiweza kustahimili uongozi wa miaka mitano ya kwanza, athari za mitandao ya kihalifu ambayo imedhamini umaarufu wa CHADEMA zinaweza kupelekea nchi yetu kuvurugika kiuchumi na kisiasa kwa muda mrefu ujao.

Hiyo ndiyo sababu CCM mpya na imara inayoongozwa vizuri na kwa uadilifu itahitajika kutoa mwelekeo kwa watu wa nchi hii.

Kwa kumalizia, vyovyote matokeo ya uchaguzi yatakavyokuwa, tuwe tayari kusimama kidete na kusaidia nchi yetu kusonga mbele.

Nawatakia nyote siku njema
 
Mmetuchosha mafisadi ambao tokea utotoni mwenu hamjawai kushika jembe kulima,Kura yangu mabadiliko tu
 
Hii ndo tunaita selective myopia!...Kwamba Mufuruki ameona matatizo yanayoweza kujitokeza kama tu CHADEMA itachukua nchi,bila kuchambua athari ambazo CCM imezileta na kuacha uozo mwingi in its trail,kama mauaji ya tembo,uhujumu uchumi on record levels(ESCROW!),Mikataba mibovu na debilitating national debt ambalo sasa linafikia matrilioni ya shilingi!...na kuanza kuongelea cheap politics!
 
biased.hakuna kitu.vyama viko 8 kwa nini unawaongelea ccm tu na chadema katika ushindi?alfu unaona mabaya tu kwa cdm.
 
Huyu ali mafuruki lazima aitete ccm maana amefanya biashara zake kwa fadhila za ccm
 
Tulishafanya maamuzi asubirie tena kipindi kingine. Kwa sasa tunataka mfumo kandamizi wa CCM uondoke then 2020 Mungu akipenda, tutaanza upya.
 
Watanzania hatuwezi kuchaguliwa Rais na Mufuruki ambaye anafaidika na mfumo wa CCM uliopo sasa.
 
Kaka Ali biashara eti ccm nzuri kwasbbu kodi zile unazosamehewa na ccm au nini
 
Kwani huyo Mufuruki watoto wake wanahitaji mkopo wa vyuo, anahitaji matibabu Amana au Sekou Toure, anajua vipele vya kuumwa na mbu vinafananaje!?

Japokuwa JK kashindwa kuvunja bunge na baraza la mawaziri, lakini kumbuka funzo lake kuwa 'changanya na zako'.
 
Da wakati mwingine unaeza kuwa popular ukajikuta unadhani kila utakachokisema kina make sense. Kwa uchambuzi wake sijaona alichokisema zaidi ya kueleza historia. Maana serikali inayoondoka ndo yenye sifa hizo alizozieleza na kwamba uchumi wetu umeharibika pakubwa for the past ten years.
 
Hii ndo tunaita selective myopia!...Kwamba Mufuruki ameona matatizo yanayoweza kujitokeza kama tu CHADEMA itachukua nchi,bila kuchambua athari ambazo CCM imezileta na kuacha uozo mwingi in its trail,jkama mauaji ya tembo,uhujumu uchumi on record levels(ESCROW!),Mikataba mibovu na debilitating national debt ambalo sasa linafikia matrilioni ya shilingi!...na kuanza kuongelea cheap politics!
Ni mara mia ya kuirudisha ccm kuliko kumpa au kulipa uongozi kundi la mafisadi na mafanya biashara ambayo yanasubiri kuitafuna nchi yetu inayoelekea kwenhe uchumi wa kati uchumi wa gesi. Wananchi hatudanganyiki janja yenu ya kutaka kukwapua gesi tumeshaing'amua. Nendeni mkaendelee na biashara zenu.
 
Ndio alitaka kusimamia mdahalo wa wagombea Urais huyo jamaa. Duh
 
Huyu Ali Mafuruki ndio Nani Hadi watu Wenye Uelewa Mpana Tumsikilize...kama Anafaidika na Tax holidays za Utawala wa

CCM basi Ajiandae Kulipa Kodi Kwa Usahihi.
 
Ni mara mia ya kuirudisha ccm kuliko kumpa au kulipa uongozi kundi la mafisadi na mafanya biashara ambayo yanasubiri kuitafuna nchi yetu inayoelekea kwenhe uchumi wa kati uchumi wa gesi. Wananchi hatudanganyiki janja yenu ya kutaka kukwapua gesi tumeshaing'amua. Nendeni mkaendelee na biashara zenu.

Acha kuendeshwa kwa hisia hasi. Ni kweli unaweza kutueleza sisiem wamefanikisha kipi katika nchi hii yenye kila neema za Rabuka? Hebu amka wewe!
 
Ningependa kutoa wito kwa watu wote wenye nia njema na wazalendo kuacha kukaa pembeni na kulalamika na badala yake kujihusisha moja kwa moja katika kuibadili CCM na uongozi wake, kuweza kutoa uongozi thabiti na wa kuwajibika kwa nchi yetu. Ujenzi wa taifa huwa ni jambo gumu na kazi hii inaweza kushindwa kutekelezwa licha ya nia njema na jitihada za nyuvu. Inahitaji bidii na subira.

Kizazi chetu kitaweza kuchangia kiasi fulani katika kazi hii njema na vizazi vijavyo labda vitaendeleza kujenga juu ya tuliyoacha nyuma.

Nina mitazamo miwili ya mustakbali wa nchi yetu baada ya uchaguzi wa Jumapili na yote inahitaji ushiriki wetu sote kikamilifu na kwa ufanisi katika kuipeleka nchi yetu mbele.

Mtizamo wa kwanza ni ule wa Magufuli kuibuka mshindi baada ya uchaguzi wa uraisi na kuchukua uongozi wa chama ndani ya miezi 6.

Magufuli ameshatangaza nia ya kukigeuza Chama cha Mapinduzi na kukirudisha katika misingi yake ya kiitikadi na kukijenga upya. Hataweza kufanya haya yote peke yake na ndio hapo sote tunahitajika kuwa tayari kumsaidia.

Mtazamo wa pili ni ule wa Lowassa kuibuka mshindi baada ya uchaguzi, jambo ambalo litatupelekea kama nchi katika wakati mgumu na usiotabirika kwa sababu nyingi.

Kwanza kabisa CHADEMA imepoteza misingi yake ya kiitikadi na hasa msimamo wake wa kupinga ufisadi, inaongozwa na kundi la watu wasio na maadili wala uzalendo, ambao nia yao ni kujitajirisha binafsi na kukwepa mkondo wa haki na sheria kwa madhambi yao ya nyuma.-

Na endapo CCM itashindwa, itakabiliwa na tishio la sintofahamu kuhusu kuwepo kwake kama tulivyoona kwa vyama vya uhuru vilivyotawala muda mrefu ( kama KANU, UNIP, MPC n.k) vilipopoteza madaraka.
Ukweli usiokwepeka ni kwamba kuiacha CHADEMA ikatawala peke yake kwa zaidi ya miaka mitano itaashiria maafa makubwa yasiyosemeka kwa nchi hii na watu wake.

Hivyo basi itabidi Watanzania wazalendo wenye nia njema wakunje mikono ya shati na kushiriki kikamilifu katika kukijenga upya na kukiimarisha chama cha CCM ili kiwe tayari kutawala wakati tukuiingia tena katika mchakato wa uchaguzi-- mwaka 2020.

Ushindi wa CHADEMA unatia wasi wasi zaidi kwa sababu ya idadi na ukubwa wa madhara yanayoambatana na ushindi huu.

Moja ni kwamba Lowassa ameahidi kuunda mfumo wa serikali 3 ndani ya siku 100 na sidhani kama uelewa wake kuhusu serikali hizi 3 ni kama ulioainishwa na Kamisheni ya Warioba.

Sote tunajua umuhimu wa muungano wetu na Zanzibar katika kuwepo kwa amani na utulivu katika sehemu hii ya bara letu la Afrika na tunafahamu fika athari za kutengua muungano bila kufuata taratibu za kikatiba.

Mwenyezi Mungu atunusuru na matokeo haya, Amina.

Madhara mengine- yanaweza kutokea iwapo afya ya Lowassa itaporomoka kufikia kiasi cha yeye kushindwa kutawala nchi. Hayo yakitokea, chini ya Katiba iliyopo, urais- utashikwa na Makamu wa Rais Duni Haji Duni, mwanachama mamluki wa CHADEMA, mwanachama mwanzilishi wa CUF na mhafidhina wa siasa za kupinga muungano.

Na hata Lowassa akiweza kustahimili uongozi wa miaka mitano ya kwanza, athari za mitandao ya kihalifu ambayo imedhamini umaarufu wa CHADEMA zinaweza kupelekea nchi yetu kuvurugika kiuchumi na kisiasa kwa muda mrefu ujao.

Hiyo ndiyo sababu CCM mpya na imara inayoongozwa vizuri na kwa uadilifu itahitajika kutoa mwelekeo kwa watu wa nchi hii.

Kwa kumalizia, vyovyote matokeo ya uchaguzi yatakavyokuwa, tuwe tayari kusimama kidete na kusaidia nchi yetu kusonga mbele.

Nawatakia nyote siku njema

Uliua Air Tanzania (ATC) ili kujnufaisha...Huna jipya ni walewale
 
Ali Mufuriki ni kati ya wafanyabiashara ambao hawalipi kodi inavyotakiwa hapa Tanzania. Lazima ajipendekeze kwa CCM kulinda interest zake.
 
Bwana Ali Mufuruki wewe huwezi kusema neno lolote baya juu ya Makofuli maana nyie ni marafiki na ulisoma secondary moja na darasa moja. Kwa mtizamo wangu your really biased.
 
Back
Top Bottom