Elections 2010 CCM Vipande Vipande Rorya,Diwani , M/Nyekiti CCM Wilaya Wajiuzulu,Sasa Wafikia Watatu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
428
Mchakato wa kuwapata mameya,manaibu mameya na wenyeviti wa Halmashauri nchini kupitia CCM ,Unaendelea kukipasua chama hicho baada ya diwani mwingine wa chama hicho kujiuzulu wadhifa huo

Aliyejiuzulu jana ni diwani wa kata ya nyamtinga ,Okea Ogigo ,wilaya ya Rorya Mkoani Mara akiungana na wengine wawili waliojiuzulu juzi ,Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma ,na Lukio Ambogo wa kata ya Nyaongo

Pamoja na madiwani hao,wanaopinga uamuzi ya kuenguliwa kwa baadhi ya majina kuwania uenyekiti wa halmashauri uliofanywa na fisadi Yusuph Makamba na Pius Msekwa dhidi ya msimamo wa wilaya ,pia yumo mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Rorya ,Leonard Yoda

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkoma Shirati Yoda alisema kuwa haoni sababu ya kuendelea kukiongoza chama wakati maamuzi ya vikao havizingatiwi na uongozi wa juu wa chama ,Mwenyekiti huyo anayeachia ngazi ,Yoda alisema kuwa uongozi wa mkoa na kamati ya siasa chini ya uenyekiti wa makongoro nyerere na katibu wake Ndekubali Ndengaso,walipitisha majina mawili Lukio Ambogo na Okea Ogigo ambao hawakuwa na Makundi na hawakuwa na kashfa ya Rushwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2010

Katibu wa kata ya Mkoma Juma Ombata naye Ametangaza Kujiuzulu
 
mbona makamba hajiuzuru tu..hivi anakumbuka alivosemaga atashangaa sana kama mtoto wake hatopewa unaibu waziri?
 
Safi sana ccm, endeleeni kujipasua...sisi tu najiaanda kuja kuziba hayo mapengo...vita ya kunguru furaha ya nzige..
 
Hii ni vita ya UTEGI NA SHIRATI sasa kichwa maji makamba bila ya kujua ame-aside na Genge la wahalifu la UTEGI (Lameck Airo, Ochelle na Obeto) lakini anashindwa kujua kwamba ndio anaizika CCM huko Rorya. Kwanza kuwarudisha hao jamaa ni kwamba kamvunjia sana heshima Makongoro Nyerere.
MAKAMBA=KIBONDE=SOPHIA SIMBA=CELINE KOMBANI=DR BENSON BANNA=KIKWETE=MEGHJI
 
mkuu kwenye hii vita obeto yupo na watu wa shirati maana mkiti wa wilaya aliyejiuzulu ni mdogo wake kabisa. hapa waliomhonga makamba na msekwa ni lameck airo, ochele na yule mganga wa kienyeji odembaambaye ni diwani wa buturi. habari za kuaminika wanasema imetumika millioni 75
 
nje ya chama wacheze faulo mpaka na ndani ya chama wanachezeana faulo?! Yaliyowakuta ni madogo the worst is yet to come.
 
CCM wanaonyeshana UFUNDI WA KUCHAKACHUA. Hivi ni wao kwa wao wanaibiana hivyo je wanapokutana na vyama vingine
 
Mchakato wa kuwapata mameya,manaibu mameya na wenyeviti wa Halmashauri nchini kupitia CCM ,Unaendelea kukipasua chama hicho baada ya diwani mwingine wa chama hicho kujiuzulu wadhifa huo

Aliyejiuzulu jana ni diwani wa kata ya nyamtinga ,Okea Ogigo ,wilaya ya Rorya Mkoani Mara akiungana na wengine wawili waliojiuzulu juzi ,Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma ,na Lukio Ambogo wa kata ya Nyaongo

Pamoja na madiwani hao,wanaopinga uamuzi ya kuenguliwa kwa baadhi ya majina kuwania uenyekiti wa halmashauri uliofanywa na fisadi Yusuph Makamba na Pius Msekwa dhidi ya msimamo wa wilaya ,pia yumo mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Rorya ,Leonard Yoda

Akizungumza na wananchi wa kata ya Mkoma Shirati Yoda alisema kuwa haoni sababu ya kuendelea kukiongoza chama wakati maamuzi ya vikao havizingatiwi na uongozi wa juu wa chama ,Mwenyekiti huyo anayeachia ngazi ,Yoda alisema kuwa uongozi wa mkoa na kamati ya siasa chini ya uenyekiti wa makongoro nyerere na katibu wake Ndekubali Ndengaso,walipitisha majina mawili Lukio Ambogo na Okea Ogigo ambao hawakuwa na Makundi na hawakuwa na kashfa ya Rushwa kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2010

Katibu wa kata ya Mkoma Juma Ombata naye Ametangaza Kujiuzulu

Nakubaliana na msimamo wao wa kutetea kile wanachoamini kuwa ni sahihi. Ila nina mashaka na ufahamu hawa jamaa. Hivi ina maana walikuwa hawaijui CCM mpaka wakati huu wa uchaguzi wa meya? Hivi ni kweli rushwa na uchakachuaji wa matokeo vimeanza wakati huu wa uchaguzi wa meya peke yake? vipi kuhusu rushwa na uchakachuaji mkubwa uliofanyika wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu? ina maana hawakuona kweli?

Hata hivyo nawaunga mkono kwani kama sikosei wahenga walisema "kufanya kosa siyo kosa bali kurudia kosa"
 
Nilitegemea MP std VII angemaliza mambo kama alivyoahidi

Nadhani yeye kwa uelewa wake alidhani kayamaliza kwa kupitisha rupia kwa Makamba ili kuhakikisha chaguo lake linapita. Alisahau kuwa kuna mambo mwngine hayatatuliwi kwa rupia peke yake.
 
Hao mafisadi ni NOMA unaweza kuongoza ktk kura halafu unaambiwa kura zako hazikutosha ila aliyekufuatia kura zake zimetosha.
 
Issue kama hii ingetokea Chadema, Uhuru na Habari leo wangeishikia bango kweli kuonyesha kuwa Chadema ina ukabila na imeanza kufa. Lakini kwa kuwa ni CCM husikii hata wakiiongelea.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom