CCM vipande vipande Mara

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225

headline_bullet.jpg
Diwani, mwenyekiti wilaya wajiuzulu
headline_bullet.jpg
Sasa wafikia watatu, kisa uenyekiti

Mchakato wa kuwapata mameya, manaibu mameya na wenyeviti wa halmashauri nchini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeendelea kukipasua chama hicho baada ya diwani mwingine wa chama hicho kujiuzulu wadhifa huo.
Aliyejiuzulu jana ni diwani wa kata ya Nyamkinga, Okea Ogigo, wilayani Rorya mkoani Mara akiungana na wengine wawili waliojiuzulu juzi, Ongujo Wakibara wa kata ya Mkoma, Shirati na Lukio Ambago wa kata ya Nyahongo.
Pamoja na madiwani hao, wanaopinga uamuzi ya kuenguliwa kwa baadhi ya majina kuwania uenyekiti wa halmashauri, uliofanywa na vikao vya juu vya chama hicho dhidi ya msimamo wa wilaya, pia yumo Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Rorya, Leonard Yoda.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Yoda alisema kuwa haoni sababu ya kuendelea kukiongoza chama wakati maamuzi ya vikao hayazingatiwi na uongozi wa juu wa chama.
Alisema katika mchakato unaoendelea sasa wa kumpata Mwenyekiti wa Halmashauri ya

Rorya maamuzi yao yamekuwa yakidharauliwa.
Katika mchakato huo, wagombea watano walijitokeza ambao ni madiwani kupitia CCM, Charles Ochele, Yamo Odemba, Ongujo Wakibara, Lukio Ambogo na Okea Ogigo.
Mwenyekiti huyo anayeachia ngazi, Yoda alisema kuwa uongozi wa Mkoa na Kamati ya Siasa chini ya Mwenyekiti wake, Makongoro Nyerere na Katibu wake, Ndekubali Ndengaso, walipitisha majina mawili ya Lukio Ambogo na Okea Ogigo ambao hawakuwa na makundi wala malumbano.
Alisema wapenda amani na wanaotaka kukinusuru chama waliunga mkono maamuzi ya kamati ya mkoa kwa kuyarudisha majina hayo ya wagombea ambao hawakuwa na malumbano.
Alisema kuwa baada ya kukatwa majina ya Ochele, Wakibara na Odemba, mgogoro ulioanza siku za nyuma za kugombea makao makuu ya wilaya kati miji ya Shirati, Utegi na Randa, uliibuka tena kiasi cha kuleta mvutano mkubwa na kusababisha baadhi ya madiwani kutishiana maisha na kutoleana silaha. Alisema hali hiyo ilizidi kuleta mgawanyiko kati ya jamii ya wakazi wa tarafa za Nyancha, Suba na wakazi wa Girango na Luo Imbo.
Alisema kuwa matatizo hayo yote yalitokana na madiwani, Mwenyekiti Ochele na Ongujo, pia kulikuwa na madonda ya mgogoro wa Hospitali ya Rufaa uliosababisha serikali kuipeleka Shirati, nayo bado yangalipo miongoni mwa jamii.
“Sasa hili la uenyekiti tena limeleta vurugu kubwa kutokana na hali hiyo mbali na kutoa malalamiko yetu ngazi za juu bila mafanikio naona sina sababu ya kuendelea kuongoza chama wilaya huku kukiwa na mpasuko mkubwa naachia ngazi na kuungana na wenzangu walioachia ngazi za udiwani, Wakibara, Ambogo na Ogigo, alisema.
Katibu wa Kata ya Mkoma CCM, Juma Ombata naye ametangaza kujiuzulu wadhifa wake na nafasi hizo kuachwa wazi. Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Ndekubali Ndaengaso, alipoulizwa kuhusiana na suala hilo alisema: “Sisi uongozi wa Mkoa tunasikitishwa na hatua ya wanachama wenzetu hao kuchukua maamuzi ya haraka ya kuachia ngazi bila kufuata taratibu za chama tunafuatilia sakata hilo na sisi ili tuone kama tunaweza kukinusuru chama ,” alisema. Hayo yakitokea Rorya, CCM mkoani Mbeya na Arusha kinadiwa kuwafunda madiwani wake ili kuepuka hasira za kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea wa nafasi za umeya na unaibu meya.
CCM imekuwa majeruhi mkubwa wa mchakato wa uchaguzi, kila maamuzi yanayochukuliwa yanakumbana na upinzani hasa inapotokea waliopitishwa na wanachama ngazi za chini kuenguliwa na vikao vya juu.
 
Sihitaji kujua source ya hiyo habari.

Japo Malaria Sugu anaweza kusema huo ni Udaku taslimu, lakini hali hali halisi ndiyo hiyo.

Watagawanyika mpaka ikulu kudadadadeki!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom