Siku hizi imekuwa kawaida karibu kila siku kwa viongozi wa CCM kukisema vibaya Chadema na hata vyombo mbalimbali vya habari vyenye mrengo wa CCM na serikali vimekuwa mara nyingi vikiandika habari mbaya kuhusu Chadema nyingi zikiwa zimetiwa chumvi na nyingine hata kupotoshwa. Naamini wanadhani wanakikomoa Chadema bila kujua kwamba ndiyo wanakipa umaarufu.
Unahitaji falsafa ya watoto kujua jambo hili, yaani ukitaka watoto wasiguse kitu fulani basi usiwakataze kwamba mtu asiguse hapa; lakini ukiwaambia msiguse au msifanye jambo fulani hapo ndiyo unawajengea udadisi wa kutaka kujua je kuna nini hapo kwa nini tukatezwe. Na kwa vyovyote vile lazima watagusa au kufanya. Kwa hiyo CCM kuikandia Chadema kila siku kinawajengea Watanzania udadisi wa kukifuatilia Chadema na kugundua kumbe sio kama wanavyoelezwa huenda ndiyo maana hata Igunga waliamua kupigia kura Chadema kwa sababu kilishambuliwa sana na CCM.