CCM: Vijana Wanatuhujumu, wanaiba kadi za wazee,akina mama! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Vijana Wanatuhujumu, wanaiba kadi za wazee,akina mama!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Mar 18, 2012.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hebu soma habari hii uone jinsi ambavyo CCM imechoka na kutegemea kundi la vikongwe na akina mama. Nadhani ndio maana wameshinikiza NEC isi-update daftari la wapiga kura.

  Endelea....

  Title: Mamluki wakodiwa kufanya fujo arumeru

  TUHUMA nzito zimetolewa dhidi ya moja ya vyama vya siasa vinavyoshiriki kampeni za ubunge wilayani Arumeru kwamba kimeanza kucheza rafu kwa kukodi mamluki kufanya fujo kwenye mikutano ya vyama vingine.


  Aidha, inadaiwa kuwa, chama hicho kinatumia vijana kuiba shahada za wazazi wao ili kuwahujumu wasipige kura.

  Tuhuma hizo nzito ambazo tayari zimewasilishwa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na viongozi wa vyama vya siasa, zilitolewa jana.

  Kwa mujibu wa tuhuma hizo, chama hicho kinakodi vijana ambao wanatambulika na wamekuwa wakifika katika mikutano ya kampeni za vyama vingine na kufanya vitendo vya kuzomea, kutoa ishara mbaya na hata kujibizana na viongozi wa vyama hivyo wanapokuwa wakielezea sera majukwaani.

  "Unakuta mkutano una watu 5,000 wakisikiliza kwa makini sera za CCM, lakini tunapomaliza na kuondoka vijana watatu au watano wanajitenga pembeni na kufanya vitendo visivyo vya kistaarabu, jambo ambalo ni la hatari.

  "Katika hili hatuna hata sababu ya kuwaeleza polisi tutalishughulikia wenyewe kwa njia tutakazoona zinafaa," alisema na Meneja wa Kampeni za CCM katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM na kutaja kuwa vijana hao ni wa Chadema.

  Nchemba alisema matukio ya dhahiri ni katika kijiji cha Songolo ambako akiwa anaendesha kikao cha mabalozi, ghafla waliingia vijana watatu wasiofahamika, wakijifanya mabalozi na wenyeji wakawashitukia na kuwakagua na simu zao kukutwa na mawasiliano ya ujumbe mfupi na mgombea wa Chadema, Joshua Nassari, akiwaagiza kuingia katika kikao hicho kuchunguza kilichokuwa kinafanyika.

  "Tukio lingine lilitokea katika mkutano wa uzinduzi Jumatatu ambapo vijana wa kukodiwa walivamia mkutano wa CCM na kuweka bendera za Chadema na wengine kuja na gari la Chadema baada ya mkutano kumalizika, jambo ambalo ni la hatari maana mkutano ulikuwa na watu wengi wa CCM ambao wangeweza kufanya lolote," alisema.

  Alisema pia CCM imegundua mbinu chafu ya Chadema ya kutumia vijana wake kuiba shahada za kupigia kura za wazazi wao, wakiwa mashambani, ili kuzificha na kuwarejeshea baada ya uchaguzi, lengo likiwa ni kupunguza kura za CCM.

  "Wanaiba kadi za kupigia kura za wazazi wao.Kama inavyojulikana, wazee na akina mama ni wanachama wetu. Hili ni jambo baya sana la kuhujumu wanachama wetu wasipige kura. Tumewaeleza NEC na viongozi wengine wa vyama vya siasa, ili kukemea hili," alisema Nchemba.

  Katika hatua nyingine, CCM imevionya vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo, kuacha propaganda zinazodai kwamba mgombea wa CCM, Sioi si raia wa Tanzania.

  "Tunawaomba waache mara moja. Kwanza walimpinga kwa Msimamizi wa Uchaguzi lakini pingamizi lao likatupwa, wakaenda NEC nako rufani yao imetupwa. Kwa vile sasa vyombo vyote hivyo vimethibitisha kuwa ni raia wa Tanzania, tunawaomba waache propaganda kwa vile watakuwa wanavunja sheria za uchaguzi," alisema Nchemba.

  Alisema CCM ina uhakika wa kuibuka na ushindi katika kinyang'anyiro hicho, kutokana na tathimini waliyoifanya na pia kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wenye wanachama wengi jimboni humo, kuliko vyama vingine vyote. (Na..Gazeti la Walipakodi, Habari Leo)

  MASWALI YANGU

  1. Vitendo visivyo vya kistaarabu mjomba Nchemba ni vipi kwa tafsiri yako?? Watu watatu/watano wanaweza kuthubutu kujitoa mhanga mbele ya maelfu 5000?? Okay mjomba, vyema, kama wanafanya hivyo baada ya mkutano kwisha na watu kuondoka hatari yake nini hapo??,Hebu Mheshimiwa acha Udaku.

  2. Ni kwa kiasi gani CCM ina uhakika kuwa akina mama na wazee wote ni wa kwao?? Au ni mpango mchakachuo??
   
 2. t

  toxic JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hata wakiibiwa wana wasiwasi gani si kuna form no.17? Mwigulu kwa uongo nadhani hata shetani hamfikii,kimsingi hata ushauri ibilisi anachukua kwa huyu jamaa mchemba.P.U.MBA.V.U SANA.
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Taratibu mkuu sema naye kistaarabu atakuelewa tu!
   
 4. chitalula

  chitalula JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,307
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145


  kama ni kweli cdm hongereni sana kwani hakuna tofauti na ccm wanavyonunua shahada za watu, igunga nec ilisema hilo sio kosa baada ya yule balozi wa ccm kukutwa na shahada za watu
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aiseeeeee!!!Yaani kumbe CCM ni chama cha Wazee na akina Mama...Vijana hakutuhusu???!!!!!Ndiyo maana matatizo yetu vijana...ukosefu wa ajira,mikopo elimu ya juu nk.hayapatiwi ufumbuzi simply because yanakuwa adressed to the wrong chama siyo?Basi tunaomba tuelezwa chama chetu ni kipi...Na kwa hasira sasa hivi naenda kuiba shahada ya Mama,Baba,Bibi,Babu...hawakuti kitu wakitoka kanisani na kama fomu na 17 haitatumika kweli basi imekula kwao.
   
Loading...