CCM usinge vunja Azimio la Arusha yasingekukuta haya yanayokuta hivi sasa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM usinge vunja Azimio la Arusha yasingekukuta haya yanayokuta hivi sasa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kitero, Sep 7, 2012.

 1. k

  kitero JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ufisadi,mgawanyiko wa chama,kilio cha walala hoi,uhaba wa madarasa na madawati,huduma mbovu za Hospitalini,migomo ya wafanyakazi wa idara mambimbali,mauwaji ya raiya wasio na hatia,migomo na maandamano ya waislamu,kugomea sensa na kutumia nguvu kubwa kuhamasisha wananchi kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha kwenye zoezi la sensa,udini yote haya yanatokana na sera na uwajibikaji mbovu wa CCM.CCM iliyopo si ile aliyoiacha mwalimu.Kwahiyo kutumia nguvu ya mihimili ya dola kama mahakama na polisi ni ishara tosha kabisa ya kuwa CCM haina tena mvuto wala ushawishi.Jitafakari chukua hatua bado unaonyesha kama unauhai kiasi fulani kwa wale ambao bado hujawatenda.
   
 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Wasingekuwa madarakani hivi sasa. Pesa za EPA za Kifisadi zilisaidia kuiingiza madarakani. Mafisadi walitumia nguvu ya Pesa kuvuruga uchaguzi 2010. Kama Azimio la Arusha linekuwepo, hakuna angekuwa na Jeuri ya pesa kuvuruga matokeo ya uchaguzi
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  NENDA KAMWAMBIE ALI HASSAN MWINYI --- KAMPA KAZI HUSSEIN MWINYI; NENDA KAMWAMBIE JOHN SAMWEL

  MALECELA PIA KALETA WILLIAM MALECELA

  - Hatukuwa na MIGOMO
  -Hatukuwa na Maandamano
  -Hatukiwa na Mabepari Wabunge na Mawaziri
  -Hatukuwa na Vifisadi Ridhwani
  -Hatukuwa na Makabwela hawana kazi lakini wanapata pesa William Malecela

  *NA BADO... MLIDHANI SASA NYERERE ALITUNYIMA UHURU; UKIANGALIA KATIBA YA MAREKANI INA NGUZO 27 zote ni

  za kuwamiliki Wamarekani; Unajua

  Hakuna Mfanyakazi Kugoma Kazini Marekani? Unajua Hawasheherekei MEI MOSI? States zingine hazina UNIONS unafukuzwa kazi

  basi umepoteza kila kitu siku Hiyo Hiyo... hata kama umafanya kazi Miaka 20... Very Strict... WAO WAKAONDOA kuwaingiza

  watoto wao wawe Marais...
   
 4. k

  kitero JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa mkuu namaanisha tangia kipindi kile cha awamu yapili wangekuwa wanafuata ile misingi ya awali ya mwalimu kama azimio la arusha na ahadi zile kumi za mwana TANU wangekuwa bado wanamvuto mkubwa na tungekuwa mbali sana kimaendeleo.kusingekuwa na madhaifu kama haya yaliyopo hivi sasa,ambayo wapinzani wanayatumia.Ungekuta tunafanya kampeni kama wanazofanya Marekani hivi sasa,badala ya hizi za sasa za udini,uchinjaji,kupigana mabomu,ukabila,mambo ya ndoa sijui ufisadi,maji na barabara.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Hii huwa naiona kuwa ni convinience mean/solution kwenye matatizo ya msingi. Huwa inaambatana na misconceptions fulani ndani yake ambazo hutuacha kwenye vicious circle fulani; kwamba ni vipi na ufanisi kiasi gani Azimio la Arusha lingekuwa dawa ya matatizo tuliyonayo leo?

  Rafiki chagua upande mmojawapo tujadiliane: kwa mfano kisiasa au kiuchumi kisha tuone lile Azimio lingekuwa na mchango gani. Tusitafute majawabu rahisi, mbona lilikuwepo na uhujumu uchumi ukazaliwa kwa kasi wakati wa Mwalimu Nyerere? Na kama sio juhudi binafsi za makusudi za hayati Moringe Sokoine hali ilishanuka.

  Kwa kawaida tunahitaji vitu zaidi ya kimoja ili kuwa na hali bora. Sote tunaviahamu kuwa ni:
  a) Unahitaji watu
  b) ardhi
  c) siasa safi
  d) sera nzuri na
  e) uongozi/usimamizi bora.
  Sio kimojawapo bali vyote na tena vifanye kazi pamoja (click functionally).

  Hii dhana ya Azimio la Arusha kana kwamba lingekuwa mwarobaini wa matatizo yetu, ni wazi lilikuwapo kwa takriban miaka 25, je how good were we then? Tunaweza kufikiri vizuri zaidi na kuja na better solutions to our current challenges and problems.
   
 6. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Hiyo nayo ina mashiko.

  Sio kwamba CCM ilikuwa na mvuto au kupendwa kivile hata wakati wa Mwalimu Nyerere. Taarifa zilikuwa zinatolewa hazikuwa sahihi (were one sided); ndio maana ya kuzaliwa kwa dhana potofu kuwa CCM ilikuwa na nguvu vijijini. Nakataa kwa sababu kama CCM ilikuwa na nguvu au kujulikana vijijini CHADEMA wasingepenya na kuwa na mwitikio tunaouona sasa. Lakini wananchi walipopelekwa mbadala tu ili wachague tumeona mwitikio tofauti na taarifa zilizokuwepo.

  Nina swali la uchokozi; je ni kwa vipi bado kuna wananchi ktk baadhi ya vijiji walikuwa wanajua kuwa (bado) Mwalimu Nyerere ni Rais wakati alishastaafu na kufariki kitambo? It's lead to a path that it was a political machination at work.
   
 7. Z

  Zinjathropus JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2012
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbona AA la arusha kama njia ya kutuletea maendeleo lilishakufa zamani. Hila bado AA la arusha ndio linalo tutesa leo kwenye uongozi sio kwa minajili ya ufanisi wa AA bali kwa namna ya upatikaniji wa viongozi wa chama tawala kpitia mfumo wa AA uliojengwa na nani vile?
   
 8. Mtanzania1

  Mtanzania1 JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 1,169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Ni kweli mkuu..... kama azimio la Arusha lingekuwepo tusingekuwa na madokta na maprofesa bungeni.......wataalam wote wangekuwa wanahudumia wananchi.........lakini kutokana na msukumo wa tamaa ya mali pamoja na mgao usio wa haki wa keki ya taifa ndiyo maana wakaamua kuwa wanasiasa....
   
 9. S

  SUNGA FILS Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka unanikumbusha LUKA 19:41-44
   
 10. k

  kisimani JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kitero,

  Very Good analysis. Nimeipenda nadhani Nnauye ataipata hii.
   
Loading...