Ccm ushindi kwenda mbele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm ushindi kwenda mbele

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by zeeth, Sep 8, 2010.

 1. z

  zeeth Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha mapinduzi ni chama amabacho kimejipanga vizuri kuweza kuhakikisha kinapata ushindi wa kishindo, kwani ndio chama chenye Sura nzuri ukilinganisha na cha ma kingine chochote kinachoshiriki uchaguzi wa mwaka huu 2010.

  Sera za chama cha mapinduzi zimejikita vizuri katika kuhakikisha zinamkomboa mtazania wa aina yoyote katika kila mkoa.

  Elimu - sera ya elimu ya chama cha mapinduzi imeonyesha kuwa kweli inalengo la kumkomboa mtazania kutoka katika tatizo la kutojua kusoma na wala kuandika wanaosema elimu bure hawaitakii mema nchi yetu ya tanzania, kwani hata nchi tajiri za Mafuta kama U A E - KUWEITI, JORDAN, IRAN, ete, Wananchi wao Wanachangia swala la Elimu, miaka ya 1970 Mpaka 1980 shule za kata zilikuwa zimeanzishwa zimeanzishwa katika nchi za BRAZIL , CUBA, SDNGAPORE, Walichofanya wenzetu ni kuziboresha tu baada ya kuwa wamezijenga katika kila kata, ambacho ndio leo Serikali ya C C M IMEFANYA ndio maana kwa kufanya Hivyo leo hii cuba . ndio maana wana wataalam wakutosha katika sector Karibia zote ni imani isiyopingika katika miaka mitano mpaka kumi ijayo shule zetu za awali mpaka vyuo vikuuvitakuwa vimepiga hatua itakayoleta tija katika nchi yetu.


  Dira ya ccm pia inaelekeza serikali yake iweke mkazo katika Swala la Afya, leo zahanati KILA KIJIJI , Mpaka tarafa e t e , serikali imesha anza kupunguza Swala la watanzania kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa kuanzisha kitengo cha AFYA,Cha matibabu ya Moyo pale muhimbili Bugando Mwanza , na Hospital ya Rufaa mbeya na Tatizo la Figo pia naro mkakati wake na kwa upande wa swala la saratani ndio ndio Maana nasema Ushindi ni kwenda mbele kwa C C M.

  - SERA pia ya miundo mbinu ya barabara inaimarishwa , barabara za Rami , Madaraja sehemu mbali mbali yameanaza kujengwa , nasema tu kwamba c c m ndiyo yenye sera Madhubuti ukirnganisha na vyama vingine.

  NITAENDELEA KUELEZA KWANINI C C M USHINDI KWENDA MBELE KATIKA AWAMU YA PILI.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Unaweza usitume makala ya pili. Tumeshaamua mwaka huu tunampa kura nani hata tusikie kamnyanganya Nge mke wake.
   
 3. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zeeth soma hapo chini
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Hii ni kwa augustee mwingine - zeeth
   
 5. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Zeeth umekuzwa kwa hela ya ufisadi, maana naona uko kigiza zaidi.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Asante kwa kuonesha upeo wako katika kufikiri na kupambanua mambo.
  Ningependa kukusaidia kwa faida yako na watoto wako, wajukuu zako na vizazi vyako vijavyo kwa kukueleza yafuatayo:
  Tanzania haipaswi kuitwa nchi masikini katika dunia ya leo, lakini inaitwa masikini na sababu kubwa ni CCM. Mapato ya Taifa yanaliwa na watu wachache sana (familia 11 tu ndani ya Tanzania) ambao wamewekeza nje ya nchi.
  CCM haiwajali wananchi wake hata chembe bali CCM ni mkusanyiko wa kundi la mafisadi, wezi na waporaji. Na ndiyo sababu kubwa mafisadi wanalindwa na kupendelewa na CCM. Ni nani aliyeshikwa na kufungwa katika kesi ya EPA, RICHMOND, DEEP GREEN, MEREMETA, KAGODA?. Uchafu wote huo umefanywa na CCM na bado unalindwa na serikali ya CCM.
  Kwa akili yako finyu unadanganywa kama mtoto mdogo wa miaka 4 eti CCM wamejenga shule na zahanati na barabara, shule zilizopo watoto wanakaa chini kwenye vumbi, zahanati zilizopo hakuna dawa na wazazi wanalala chini, barabara hazipitiki. Nashindwa kukuelewa wewe ni mtanzania wa wapi na una ubongo wa namna gani.
  Mwaka huu CCM lazima ipigwe chini tena kwa staili ya kifo cha mende. Dharau zimewajaa CCM, mnafikiri mmepewa hati miliki na mungu ya kutawala Tanzania milele huku mkiendeleza madhambi yenu. Tanzania inanuka mabaya na machafu yote, ni lazima tuibadilishe na tutaweza kufanikiwa kwa kuindoa CCM madarakani.
   
 7. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  2010 hatudanganyiki!
   
Loading...