CCM: Uchaguzi wa Zambia ni ushindi kwa Demokrasia ya Afrika

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
SHAKA: UCHAGUZI WA ZAMBIA NI USHINDI KWA DEMOKRASIA YA AFRIKA

"Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawapongeza wananchi wa Zambia kwa kukamilisha uchaguzi mkuu wao kwa amani na utulivu" Shaka Mwenezi Taifa

"Na kumpongeza kwa ushindi Rais Mteule Hakainde Hichilema aliyetangazwa kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika 12 Agosti, 2021 pamoja na Rais Edgar Lungu aliyekubali kukabidhi madaraka" Shaka Mwenezi Taifa

"Wameipa heshima Afrika kuwa inawezekana demokrasia ikatekelezwa na kuheshimiwa bila kuiacha nchi vipande vipande au kuingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe" Shaka Mwenezi Taifa

"Wanaotaka kufananisha siasa za Zambia na Tanzania wanakosea kwani haziwezi kufananishwa, Zambia chama cha ukombozi UNIP kiliongoza nchi hiyo kwa miaka 27 (1964-1991) kikaondolewa madarakani na Frederick Chiluba wa MMPD (1991-2002), ambaye naye aliondolewa na Levy Mwanawasa (2002-2008) akaja Rupiah Banda (2008-2011), kisha Michael Satta (2011-2014) halafu Edgar Lungu (2015-2021) mpaka leo Hakainde Hichilema wa chama cha UPND" Shaka Mwenezi Taifa

"Siasa za nchi hiyo ni wazi kuwa upinzani wametoana madarakani wenyewe kwa wenyewe hivyo wanaofananisha siasa hizo na za Tanzania wamekosa uelewa mpana na ufuatiliaji wa siasa za kiafrika na kidunia" Shaka Mwenezi Taifa

"Ukitazama mwenendo wao utagundua ukiondoa chama cha UNIP kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi hakuna chama cha upinzani kilichokaa zaidi ya kipindi kimoja ikiwa ni ushahidi kuwa upinzani hauaminiki" Shaka Mwenezi Taifa

" Uchaguzi wa Zambia umetoa somo kwa vyama vya siasa hapa nchini hususani upinzani kuwa mgombea aliyeshinda Zambia wa chama UPND alifanya siasa safi na zaidi wakati wote wa kampeni alikuwa Balozi wa amani na kuhimiza umoja miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo akijua tunu hizo ni chachu ya maendeleo" Shaka Mwenezi Taifa

"Hichilema ametoa somo kwa vyama vya upinzani Afrika na hapa nchini kuwa demokrasia sio fujo wala vurugu bali ni mchakato wa kueleza namna unavyoweza kuwaletea wananchi maendeleo" Shaka Mwenezi Taifa

" CCM imeendelea kuaminika kwa wananchi kwa sababu kimekuwa kikiyaishi mahitaji ya umma na kuyatekeleza kikamilifu jambo ambalo daima tutaliendeleza na tunaamini watanzania wataendelea kuzidi kutuamini" Shaka Mwenezi Taifa
 
Je ni lini Tanzania tutaingia katika,ulimwengu uliostaarabika kama wenzetu mfano Wazambia,Wamalawi na ulimwengu unaothamini demokrasia ya kweli na sii democrasia ya CCM
 
Je ni lini Tanzania tutaingia katika,ulimwengu uliostaarabika kama wenzetu mfano Wazambia,Wamalawi na ulimwengu unaothamini democrasia ya kweli na sii democrasia ya ccm.

Mkuu chama gani kinaishi Demokrasia Tanzania. Lala ukiamka kunywa kahawa. Akili ikutulia jibu.
 
Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawapongeza wananchi wa Zambia kwa kukamilisha uchaguzi mkuu wao kwa amani na utulivu, na kumpongeza kwa ushindi Rais Mteule Hakainde Hichilema aliyetangazwa mshindi kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika 12 Agosti, 2021 pamoja na Rais Edgar Lungu aliyekubali kukabidhi madaraka.

Kimesema wameipa heshima Afrika kuwa inawezekana demokrasia ikatekelezwa na kuheshimiwa bila kuiacha nchi vipande vipande au kuingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe. Hayo yamesemwa na katibu wa Itikadi na uenezi wa chama hicho Shaka Hamdu Shaka alipotakiwa kuzungumzia uchaguzi huo wa Zambia.

"Wanaotaka kufananisha siasa za Zambia na Tanzania wanakosea kwani haziwezi kufananishwa, Zambia chama cha ukombozi UNIP kiliongoza nchi hiyo kwa miaka 27 (1964-1991) kikaondolewa madarakani na Frederick Chiluba wa chama cha Movement for MMPD (1991-2002), ambaye naye aliondolewa na Levy Mwanawasa (2002-2008) akaja Rupiah Banda (2008-2011), kisha Michael Satta (2011-2014) halafu Edgar Lungu (2015-2021) mpaka leo huyu Hakainde Hichilema wa chama cha UPND" Alisema Shaka.

Amefahamisha kuwa kwa siasa za nchi hiyo ni wazi kuwa upinzani wametoana madarakani wenyewe kwa wenyewe hivyo wanaofananisha siasa hizo na za Tanzania wamekosa uelewa mpana na ufuatiliaji wa siasa za kiafrika na kidunia.

"Ukitazama mwenendo wao utagundua ukiondoa chama cha UNIP kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi hakuna chama cha upinzani kilichokaa zaidi ya kipindi kimoja ikiwa ni ushahidi kuwa upinzani hauaminiki" Alisema Shaka

Hata hivyo Shaka amesema Uchaguzi wa Zambia umetoa somo kwa vyama vya siasa hapa nchini hususani upinzani kuwa Mgombea aliyeshinda Ndugu Hakainde Hichilema wa chama cha UPND alifanya siasa safi na zaidi wakati wote wa kampeni alikuwa Balozi wa amani na kuhimiza umoja miongoni mwa wananchi wa Zambia sababu alijua tunu hizo ni chachu ya maendeleo.

"Hichilema ametoa somo kwa vyama vya upinzani Afrika na hapa nchini kuwa demokrasia sio fujo wala vurugu bali ni mchakato wa kueleza namna unavyoweza kuwaletea wananchi maendeleo, CCM imeendelea kuaminika kwa wananchi kwa sababu kimekuwa kikiyaishi mahitaji ya umma na kuyatekeleza kikamilifu jambo ambalo daima tutaliendeleza" Alisema Shaka.​

IMG-20210629-WA0106.jpg
 
Huyu jamaa ni mwenezi wa CCM au Tanzania au UPND Zambia?
Kwanza ni vyama viwili visivyokaribiana wala kushabihiana kiitikadi. Hawa ni liberal wakati CCM ni wajamaa.

Hawa ni mlengo wa kati wakati huku ni mlengo wa kushoto kutokea kati.

Umoja wao na marafiki wao barani Afrika na Ulaya ni tofauti kabisa na CCM.

Sasa wapi na wapi? Na hawa ni wapinzani pure with liberal minds huku ni watawala waanzisha mifumo na nchi.

Shaka bila shaka nachelea kusema hajui madhira aliyoyapitia HH kuwa Rais wa Zambia, hajui manyanyaso, hajui mateso yake na familia yake, hajui alishaswekwa ndani kwa uhaini na akaachiwa kwa pressure ya wahisani na raia, hajui hadi akina KK11 walikua wanazuiwa kumuona gerezani wakati yeye ndio founding father wa Zambia.

Hajui kuwa ni wananchi kukaza na mifumo imara ndio imeisaidia Zambia kufika hapo kidemokrasia.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
RAIS MTEULE wa ZAMBIS kawachana Kikweli kweli ALIYOTENDEWA na RAIS LUNGU Ndio CCM Mnayo mtendea MBOWE na CHADEMA
Amesema Alikamatwa Mara 15 Tanzania Chadema Wamejaa Magerezani
TV ya Taifa ilikuwa haionyeshi Mikutano ya Upinzani na Tanzania Tunaona TBC nayo Haionyeshi Mikutano ya Upinzani
Anasema Alipigwa MABOMU na Tanzania Tunaona CHADEMA Wanapigwa MABOMU WANAKAMATWA mpaka MAKANISANI
 
Back
Top Bottom