Uchaguzi 2020 CCM tuwe wakweli, mpaka mwisho wa kampeni tunaweza tukashindwa vibaya sana

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Kitu ambacho narudia mara ya pili kikisisitiza, ni kwanini Mzee baba anafanya kazi ya kujibu hoja za Tundu ambaye ana akili nyingi sana na sasa ameshamjuia anacheza na milio ya midundo yake. Mimi nilisema mzee ajikite zaidi kuelezea anayotaka kuyafanya badala ya kuhangaika kumjibu Tundu, hii kazi ifanywe na kina Polepole. Hivi CCM mpya tuna shida gani tunakosa ubunifu sisi?

Tuelekeako mbele ya safari tutajikuta tunajibu hoja za Tundu tukasahau yaliyoko mbeleni. Huyu jamaa ana taarifa zote za mahali tunakoteleza, wapo watumishi wa umma wasio waaminifu wanatoa haya.Sasa tinavyozidi kumjibu ndivyo anavyozidi kuyatoa mengi ya ndani na sisi tutaendelea kumjibu.

Hawa jamaa ni wa ajabu sana, wameficha silaha zao pembeni za kampeni kama vile katibu mkuu na naibu wake, mwenyekiti wao pia wamemtangulizia Mgombea na mgombea mwenza na viongozi wa kikanda. Wanataka mwishoni watumalize sisi ambao kila safari tunaambatana timu yote.
 
Hivi kwa chama kilicho tawala 60 yrs, kina stahili kufanya kampeni au kilistahili kurudi kwa wananchi kuelezea kilivyo simamia maendeleo ya nchi? Hivyo kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza?

Maana kwa sasa tuna ona CCM wana fanya kampeni kuliko hata vyama vya upinzani. Hii ni kuonyesha CCM kwenye muda wote wa utawala wamekuwa walaghai na hawastahili tena kuongoza hii nchi. Ifike mahali sasa Watanzania tuseme Sasaaa! Baaaaasiii!!
 
Wewe hujawahi kuwa CC M!

Siku hizi wapinzani wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!

Kwani hutaki CCM ishindwe uchaguzi!

Yaani kuna wajinga wanaamini CCM itashindwa katika Uchaguzi huu!
 
KWA akili zangu timamu upinzani unge waachia KILA kitu CCM. Serikali za mitaa,udiwani, Ubunge na urais Ingenoga sanaa.
Inafikirisha.

Ifikapo 2025 tuwapime.
 
Wewe hujawahi kuwa CC M!

Siku hizi wapinzani wamekuwa watoa ushauri kwa CCM!...
Mkuu nakuona kama umebaki pekeako unaeamini hivyo! Hebu tazama mwenyewe na ulinganishe hoja za mgombea wenu na zile za mgombea wa CHADEMA,

Yeye tu mgombea wenu kaamua aziache na sasa kaanza kuhangaika na hoja za Lissu! Yaani CCM wamejikuta wanafanya kile anachofanya Lissu wakati walishasema walishafunga mitambo je mitambo imezimwa na nini?
 
KWA akili zangu timamu upinzani unge waachia KILA kitu CCM
Serikali za mitaa,udiwani, Ubunge na urais Ingenoga sanaa.
Inafikirisha....
Ifikapo 2025 tuwapime.
Tuwe wakweli tuache unafki, mzee baba kuna mahali anachemka sanaa
 
wajinga wajinga wakisoma nyuzi kama hizi wananunua maji wanakaa chini wanakunywa na kufurahi.

nyie mwaka huu kuna mtu anapata ushindi 96% hamtaki subirini.
 
Mimi ni Chadema ila Ilani yetu hailewek i ya ubabaishaji mno.suala la majimbo limetuvua nguo
 
Back
Top Bottom