CCM, tutawapuuza muda si mrefu, Hii kuwasema watu baada ya kuwakimbia si sawa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Nawaandikia viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Nawaandikia kuwaambia kuwa siku si nyingi tutawapuuza kwa kila mnalolisema au kulitenda. Hii tabia ya kukaa na mafisadi na majizi kwenye chama chenu hadi wahame au waachane na siasa ndiyo muwanyooshee vidole na kuwasema si sawa.

Uzuri wenu CCM ndiyo mnaounda Serikali. Mna kila uwezo, kama kuna nia pia, ya kuwachunguza, kuwabaini na kuwashughulikia mafisadi na majizi yote yaliyopo kwenye chama chenu. Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wenu wa Taifa wa CCM aliingia madarakani, pamoja na sera nyinginezo, na sera ya kupambana na kuyashughulikia mafisadi na majizi yote ya hapa Tanzania. Sera yake hiyo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Mahakama ya Mafisadi, iliwavutia watanzania waliokuwa wamechoshwa na ufisadi na kumchagua Magufuli kwa wingi wao.

CCM mnapaswa kumsaidia Rais Magufuli kwa matendo katika vita dhidi ya mafisadi na majizi ya mali za umma. Msaidieni Rais kuwabaini, kuwachunguza na kuwashughulikia mafisadi wote waliopo CCM hivi sasa ili kama usafi uanzie ndani ya CCM. Kungoja hadi mwanasiasa ahame CCM na nyinyi kuanza kumsema kuwa ni fisadi na mwizi ni utapeli wa hali ya juu.

CCM, kuweni serious na mambo yenu. Kuaminika kwenu kunategemea na mnayoyasimamia na kuyafanya sasa. Pia, mnapaswa kujibu kichama mapigo yote ya wanaohama bila ya kuwategemea wasomi makada na watawala kuwajibu wanaoibua maswala ya kichama zaidi. Nasema tena, mafisadi na majizi yote yaliyopo CCM yashughulikiwe sasa. Au mseme wazi sasa kuwa ndani ya CCM hakuna mafisadi au majizi.

Msipowashughulikia sasa mafisadi na majizi hadi msubiri wahame au wajiuzulu, tutawapuuza na kuwaona matapeli, walaghai na watu wa propaganda. Muda wa kuwashughulikia mafisadi na majizi ndani na nje ya CCM ni sasa katika kuunga mkono sera ya Rais wetu na mwenyekiti wenu Dr. John Pombe Magufuli.
 
Nawaandikia viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Nawaandikia kuwaambia kuwa siku si nyingi tutawapuuza kwa kila mnalolisema au kulitenda. Hii tabia ya kukaa na mafisadi na majizi kwenye chama chenu hadi wahame au waachane na siasa ndiyo muwanyooshee vidole na kuwasema si sawa.

Uzuri wenu CCM ndiyo mnaounda Serikali. Mna kila uwezo, kama kuna nia pia, ya kuwachunguza, kuwabaini na kuwashughulikia mafisadi na majizi yote yaliyopo kwenye chama chenu. Kwakuwa mmekuwa madarakani tangu kuanzishwa kwenu mwaka 1977, hamuwezi kusema kuna mahali kuna majizi mengi kuliko nyinyi kwakuwa mko wengi.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wenu wa Taifa wa CCM aliingia madarakani, pamoja na sera nyinginezo, na sera ya kupambana na kuyashughulikia mafisadi na majizi yote ya hapa Tanzania. Sera yake hiyo, ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Mahakama ya Mafisadi, iliwavutia watanzania waliokuwa wamechoshwa na ufisadi na kumchagua Magufuli kwa wingi wao.

CCM mnapaswa kumsaidia Rais Magufuli kwa matendo katika vita dhidi ya mafisadi na majizi ya mali za umma. Msaidieni Rais kuwabaini, kuwachunguza na kuwashughulikia mafisadi wote waliopo CCM hivi sasa ili kama usafi uanzie ndani ya CCM. Kungoja hadi mwanasiasa ahame CCM na nyinyi kuanza kumsema kuwa ni fisadi na mwizi ni utapeli wa hali ya juu.

CCM, kuweni serious na mambo yenu. Kuaminika kwenu kunategemea na mnayoyasimamia na kuyafanya sasa. Pia, mnapaswa kujibu kichama mapigo yote ya wanaohama bila ya kuwategemea wasomi makada na watawala kuwajibu wanaoibua maswala ya kichama zaidi. Nasema tena, mafisadi na majizi yote yaliyopo CCM yashughulikiwe sasa. Au mseme wazi sasa kuwa ndani ya CCM hakuna mafisadi au majizi.

Msipowashughulikia sasa mafisadi na majizi hadi msubiri wahame au wajiuzulu, tutawapuuza na kuwaona matapeli, walaghai na watu wa propaganda. Muda wa kuwashughulikia mafisadi ma majizi ndani na nje ya CCM ni sasa katika kuunga mkono sera ya Rais wetu na mwenyekiti wenu Dr. John Pombe Magufuli.
Leo umeandika kweli, kweli daima. Nakupongeza.
Mnamtuhumu Nyalandu wakati Mmemkumbatia Chenge??
 
Serikali inapowashughulikia mafisadi mnakuja na sound za issues za visasi!!
 
Jilulize anaetajwatajwa kuhusika katika kuagiza vichwa vya treni vyenye utata ana wadhifa gani leo hii?

Leo wako kimya siujui wanasubiri siku ahame chama ndio waanze kumsimanga?

Mawaziri waliotajwa katika ripoti za kamati za madini kuna hata mmoja ameshatakiwa?

Leo hii Chenge ana wadhifa gani Bungeni?

Jiulize ni kweli mahakama ya mafisadi imekosa watu au ni watu wameinyama kazi mahakama hii?

Poleni sana wenye imani na hiki chama!
 
Waliisha puzwa na kukataliwa na watz ndo maana wanaongoza kwa mabavu....ZENJI wamepoka ushindi wa wazi mchana kweupe km walivyotaka kumuua LISSU.
Bara huku wamepiga bao la mkono kwa kuahidi kwa uwazi kabisa....
ccm IIISHACHOKWA IMECHOKWA NA ITACHOKWA TUUUUU
Kwa miaka 50 ijayo CCM bado itaendelea kuongoza Tanzania...huku ikiendelea kuwa Chama adui kwa mafisadi na majangili ambao wanapata hifadhi chadema
 
Jilulize aliehusika kuagiza vichwa vya treni vyenye utata ana wadhifa gani leo hii?
Aliyehusika na wizi wa Richmond mlipa wadhifa gani huko chadema?
Chadema ya leo ijiweke mbali kuongelea ufisadi kwa kuwa imegeuka kuwa chaka kuu la ufisadi na ujangili
 
Nyani haoni kundule japo akimuona nyani mwenzie humcheka na kumnyooshea vidole!
 
Msiwabomolee watu wa Mwanza maana wamenipa urais.

Hii tosha inaonesha maombi mabaya yamefanya kazi,

Mwanza sasa anaiona kama Tanzania nzima.
 
Siasa za hii nchi ndivyo zilivyo, zimeathiri hata maisha yetu ya kawaida.

Mfano, unakua na mwanamke miaka kadhaa, unamlisha, unamvisha na kila kitu, siku mkiachana utasikia oooh, kwanza ana kibamia, mara alikua ananipiga, mara alikua ananitesa na kuninyanyasa

Sasa miaka yote hiyo ungekua unateseka na kupigwa si ungekua umeondoka, vinginevyo ni kua ulikja unafurahia kipigo.
 
Kwa miaka 50 ijayo CCM bado itaendelea kuongoza Tanzania...huku ikiendelea kuwa Chama adui kwa mafisadi na majangili ambao wanapata hifadhi chadema

Dogo hivi bado hata hawajakupa U-DC? Mbona wanaoingia kwenye chama wanateuliwa ... au nyinyi
wakubwa wanaona buku saba zinawatosha??? (by the way najua JPM anataka wasomi..kama vipi kamata diploma pale Open University). Otherwise utaua watoto kwa njaa...
Maana naona JPM anateua wanaoingia tuu..akina mama Mghwira, Kitila Mkumbo, Shonza..na nyinyi wapiga ramli mkiishia mitandaoni tuu....

Pambanane mkumbukwe!
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom