johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,614
- 141,439
Juzi kati nilikuwa nafuatilia habari kupitia BBC Dira ya Dunia nikashangaa kusikia kuwa huko Uchina chama cha Kikomunisti humsaidia Papa wa Vatican kuteua maaskofu wa katoliki nchini humo. Nilishangazwa zaidi kusikia kuwa papa amekubaliana na hali hiyo na kwamba yule mteule wake aliyemteua awali bila kuhusisha chama anastaafu. Chonde chonde CCM pamoja na urafiki wetu uliotukuka na chama cha kikomunisti tunaweza kuiga mengine yote lakini siyo hili. Ni ushauri tu, ahsante!