CCM tusitegemee kufaulu kwa kutumia wanachama wa kukodi. Tahadhari kabla ya hatari

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,020
2,000
Habari za weekend mabibi na mabwana,

Kumezuka wimbi la wahamiaji kutoka upande wa wenzetu wakijinasibisha kuielewa sana itikadi ya chama chetu ni jambo zuri sana kwa chama chochote cha siasa kupata wanachama.

Lakini mimi kama mwana CCM kada ambaye sijayumba toka niipokee kadi yangu mwaka 1998 Julai makao makuu ya chama Dodoma nachelea kuwatahadharisha viongozi wangu kuwa makini sana na hawa wanaorudi CCM kwa kuridhishwa na sera na utendaji wa Rais Magufuli.

Itikadi au imani ya chama haijengwi kwa siku moja au mbili. Nina uhakika kati ya hawa waliotangaza kujiunga na CCM tukiamua kufanya hata msako wa kushtukiza katika majumba yao au ofisi wanazofanyia kazi hakuna hata mmoja tutakayemkuta na ilani ya Chama Chama Mapinduzi au documents yeyote inayomtambulisha kama mwana CCM.

Natoa tahadhari kuwa makini na hawa wanachama wa kukodi.

Jumapili Njema:
 

kilambalambila

JF-Expert Member
Nov 16, 2013
8,897
2,000
Kikubwa ni kwamba waje ika wakae tu bila cheo chochote hadi 2020. Atakayeweza kuvumilia mpaka hapo ndo ikitokea nafasi afikiriwe
 

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,020
2,000
Kikubwa ni kwamba waje ika wakae tu bila cheo chochote hadi 2020. Atakayeweza kuvumilia mpaka hapo ndo ikitokea nafasi afikiriwe
sasa nani mwenye moyo wa kusubiri? kama sisi wenyewe tumesota miaka yote hiyo kukipigania Chama ila wanaoonekana ni wale walio karibu na Viongozi?
Sawa tunawatakia kila la kheri waje tuchape kazi ila 2020 litazuka songombingo tuweke akiba ya maneno
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
8,913
2,000
sasa nani mwenye moyo wa kusubiri? kama sisi wenyewe tumesota miaka yote hiyo kukipigania Chama ila wanaoonekana ni wale walio karibu na Viongozi?
Sawa tunawatakia kila la kheri waje tuchape kazi ila 2020 litazuka songombingo tuweke akiba ya maneno
Hilo songombingo siyo la kitoto, ila kwa kua chama kipo chini ya mfalme na mwanae mtanyooshwa, yeyote atayeleta fyokofyoko kukiona.
 

Mwaipungu

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
293
250
Habari za Weekend Mabibi na Mabwana.

Kumezuka Wimbi la wahamiaji kutoka Upande wa wenzetu wakijinasibisha kuielewa sana Itikadi ya Chama Chetu ni jambo zuri sana kwa chama chochote cha siasa kupata wanachama.

Lakini mimi kama Mwana CCM kada ambaye sijayumba toka niipokee kadi yangu Mwaka 1998 Julai makao Makuu ya Chama Dodoma nachelea kuwatahadharisha Viongozi wangu kiwa makini sana na hawa wanaorudi CCM kwa kuridhishwa na sera na Utendaji wa Rais Magufuli. Itikadi au imani ya Chama haijengwi kwa siku moja au mbili. Nina uhakika kati ya hawa waliotangaza kujiunga na CCM tukiamua kufanya hata msako wa kushtukiza katika majumba yao au Ofisi wanazofanyia kazi hakuna hata mmoja tutakayemkuta na Ilani ya Chama Chama Cha Mapinduzi au Documents yeyote inayomtambulisha kama mwana CCM.
Natoa Tahadhari kuwa makini na hawa wanachama wa Kukodi.

Jumapili Njema:
Kuna msemo wa kizungu unasema "a man who stands for nothing can easily fall for anything" nadhani hapo sasa ccm wanze na msemo huu.
 

Sandinistas

JF-Expert Member
Jul 5, 2013
2,336
2,000
Prof. Shivji alipata kuuliza iwapo operesheni vyeti itafuatiwa na elimu feki. Kwa siasa hizi za kitoto zinazogharimu nchi nimeamini ni kweli elimu feki imetamalaki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom