VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,800
Najua kuwa kwasasa wanaCCM wenzangu wengi wanaamini kuwa katika mazingira ya kisiasa ya sasa CCM haipitiki kiuchaguzi. Makada wenzangu wengi wanaamini kuwa hakuna chama chochote cha upinzani au mpinzani binafsi atakayeweza kuishinda CCM kwenye uchaguzi mdogo au hata mkuu wa mwaka 2020. Tunaamini kuwa CCM iko sahihi kwa kila jambo na ushindi ni lazima.
Kwangu mimi kama kada kindakindaki na mwanasiasa mkongwe chamani na nchini, siamini hivyo. Siamini kuwa mwaka 2020 lazima CCM ishinde. Kama kada niliyepikwa chamani tangu miaka ya themanini, naamini kuwa siasa ni kama upepo na uelekeo wake. Siasa hubadilika bila kutoa tahadhari. Namini kuwa mwaka 2020 ni mbali sana katika mabadiliko ya upepo wa kisiasa lakini ni karibu sana katika kujiandaa kujibu hoja.
Hapa kati kunaweza hata kukatokea chama kipya cha kisiasa. Tena kwa kumegeka hata kwa CCM yetu. Hapa kati, panaweza kujitokeza sera au muuzasera mahiri kuliko mshairi na kuwafunika wote waliotangulia. Hapa kati, panaweza kuibuka kashfa au chuki kwa walio na uhakika wa kuchaguliwa na hatimaye kukataliwa kwelikweli. Hapa kati, panaweza kutokea 'wasaidizi wa ushindi' wa CCM wakabadilika. Wakawa wavivu na wenye wivu.
Kinga pekee kisiasa, ili kuwa na uhakika wa kushinda tena, ni kutekeleza Ilani na ahdi za wagombea wetu wa mwaka 2015. Tutakachopaswa kuonesha mwaka 2020 ni utekelezaji wa Ilani na ahadi zetu kwa wananchi. Si vinginevyo. Wananchi wanatupima CCM kwa Ilani yetu ile ya mwaka 2015 kabla ya kutuamini tena kwa Ilani ya mwaka 2020. Watataka kuyaona mazuri yetu kupitia utekelezaji wa Ilani yetu. Utekelezaji wa Ilani na hadi ni kila kitu.
Kutegemea Tume ya Uchaguzi, Polisi na mfumo kuturejesha madarakani kumepitwa na wakati. Kila kada, katika nafasi yake na mahali alipo, asimamie utekelezaji wa Ilani na hadi zetu za 2015. Kuamini kuwa wapinzani wameishiwa nguvu ni kujihatarisha sana kisiasa. Ni kujiweka rehani. Ni kujipalia makaa ya moto. CCM haina haja ya kutegemea Tume kushinda. Haina haja kutegemea Polisi kushinda. Haina haja ya kutegemea mfumo kushinda. Inapaswa kujiandaa kama chama. Muda unayoyoma.
Ukonga na Monduli 'tutashinda' lakini chamoto tutakiona!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam