CCM tusiache kulindana, Tunaona wenzetu wanavutwa mmoja mmoja mahakamani

Sioni shida kujitokeza na kusema ile ada yetu ya kulindana tusiiache, sasa kumekuwa na msukumo wa watu wasiojulikana kutaka au kuwafikisha mahakamani wenzetu ambao wakati ulee walikuwa ndio tegemezi na walisimamia na kukipa chama uthubutu.

Hizi hila za wapinzani koko zinaonekana kuzaa matunda wamemfunga Kijana ngangari kabisa Ole Sabaya kama haitoshi wanamnyemelea Braza Paul Makonda kesho na kesho kutwa Nape na wengine wengi itakuwa wamo kwenye list of shame yao,

Tufahamu hawa hawakitakii mema Chama Chetu cha CCM ,wanajenga chuki ndani yetuwanataka tuchukiane ili watuvamie na kututawala, ni lazima tuzinduke na ile taratibu ya kulindana tusiiwache.

Kwa vyovyote vile hiki kitu ni lazima kiwepo, tusiwache tukavurugwa na vyama vya ukoo,Chama chetu ni Chama Dume na lazima kingurume na kina taratibu zake, tufuate taratibu zetu ikiwemo kulindana.
Na hata mkilindana hamtabaki salama,mpaka mtakapojua kuwalinda na wengine.
 
Back
Top Bottom