CCM tupeni ripoti ya kujivua gamba v/s maandamano ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM tupeni ripoti ya kujivua gamba v/s maandamano ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Albedo, May 22, 2011.

 1. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Katika kipindi cha Miezi Miwili hapa tanzania Vyama vikubwa vya Siasa hapa Tanzania CHADEMA na CCM vimefanya harakati zenye lengo la kuwaambia wananchi ni kwa nini waungwe mkono wao na si mwingine.

  Katika kufanya Hivyo CHADEMA ilifanya Maandamano ya Amani na kufanya Mikutano ya hadhara ikiwa na lengo la kuwaonesha wananchi ni kwa nini basi Chenyewe kinapswa kupewa Dola na si CCM. Kama lengo kuu la chama cha Upinzani kinachojitayarisha kuchukua Nchi, CHADEMA kimeendeleza harakati za kuwafanya Wananchi Waichukie CCM ambayo ndiyo inayounda Serikali iliyoko Madarakani. Kwa kweli CHADEMA kama chama cha Upinzani kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuleta Chuki ya Wananchi dhidi ya Serikali. Kwa hilo nawapongeza CHADEMA kama chama cha siasa, kwa sababu bila ya kuwafanya Wananchi waichukie Serikali iliyoko Madarakani huwezi Kuchukua Dola.

  CCM katika kile kinachoonekana ni Kujaribu kupambana na Nguvu ya CHADEMA kilifanya kile walichokiita " Kujivua Gamba" na wamezunguka sehemu mbali mbali kuwaelezea Wananchi juu ya kile walichokiita "Dhana" ya kujivua Gamba. Tuliona kule Songea CCM walifanya Mkutano siku moja kabla ya CHADEMA hawajafanya wao ( Picha za Mikitano hiyo ya CCM zimekuwa ni Siri kubwa). Katika Mikutano hiyo CCM walitumia Mbinu zile zile zilizotumiwa na CHADEMA katika kujipatia Umaarufu miongoni mwa wananchi. Tuliona CCM wakimtuhumu Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa kwa kile walichokiita " Siri' ya Mshahara wa dr. Slaa na Ufisadi wa Mbowe. Baada ya Mikutano hiyo ya Kuelezea "Dhana" ya kujivua Gamba nilitarajia yafuatayo na Tuhuma za Ufisadi dhidi ya Viongozi wa Ngazi za juu wa CHADEMA

  1: Wananchi kumzomea Dr. Slaa kila apitapo
  2: Wananchi Kumzomea Freeman Mbowe kwa Ufisadi wake
  3: Wananchi kuyakataa Maandamao ya CHADEMA

  Naomba niwaalike watetezi wa CCM na "Dhana" ya kujivua Gamba waje hapa jamvini na Kutupa Tathmini juu ya Mwitikio wa Wananchi juu ya "Kujivua Gamba". Watuwekee Picha za Mikutano waliyofanya CCM Songea, Singida na Kwingine
   
 2. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bado CCM ipo katika mchakato wa kujivua magamba, taarifa za utekelezaji wa shughuli za chama huwasilishwa katika halmashauri kuu ya chama si JF
   
 3. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,039
  Likes Received: 3,069
  Trophy Points: 280
  Tusisahau pia Uv-ccm mkoa wa Dar,walitofautiana na kamati kuu ya ccm,badala ya siku90 zilizosemwa awali za watuhumiwa kujivua gamba wao walitoa siku21,na wakaenda mbali na kusema kama sivyo wataitisha maandamano mkoa wao kushinikiza hlo,watuambie wamekwama wapi maana tayari siku21 zimeisha
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Unajua kwenye mikutano yetu (CCM)watu wanarudisha kadi za CHADEMA kwa masharti ya kutopigwa picha.
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mnaonaje kama Mkitushirikisha Kwa Njia hata ya Picha

  AU MNAONA AIBU?
   
 6. M

  MPG JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli sisi CCM kwenye ziara zetu ktk mikutano tulikosa watu kabisa huwezi amini,hata ilipobidi kubeba watu kutoka vjijini kwenye malori bado tulikosa watu bwana NAPE na MKAMA walibaki wakiwa na kikundi cha makumi ya watu,ila kwenye mikutano ya CHADEMA kulikuwa na maelfu na maelfu ya watu mpaka sisi wana CCM presha inapanda inashuka;hakika CHADEMA chama Tawala na DR ni RAIS,ila mi bado ni mwana CCM daima,licha ni chama kisichokuwa na sifa ya kuongoza dola sehemu yoyote Duniani.
   
Loading...