CCM Tupeni Katiba Mpya Kuzingatia Matakwa Wananchi au Mtupishe Njia April 08, 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Tupeni Katiba Mpya Kuzingatia Matakwa Wananchi au Mtupishe Njia April 08, 2011

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Uwezo Tunao, Mar 31, 2011.

 1. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hapo nyuma wananchi tulionyesha wasiwasi mkubwa na nyinyi kujihusisha na katiba kwa peke yenu, baada ya kutuibia uchaguzi wetu October 2010 ikatuondoa kabisa imani kwenu lakini bado mkajing'ang'aniza kwamba tuwaamini na kazi hii nyeti; ajabu bado tena mmeingiza ule ule mtindo wenu wa usanii hata kwa mambo yasiohitaji mzaha.

  Kwa mtaji wa matangazo ya muswada mliogeuza juu chini na kulitoa kwenye gazeti rasmi ya serikali sasa imetuacha bila masuali zaidi kwamba kazi hii kamwe hamuiwezi na wala si wa kuaminika na lolote tena kwa kuchagua kuweka pembeni wadau wengine na kujifanyia tu mambo mpendavyo sirini.

  Tunasema kama mnadhani ni mzaha tena na msirudishe matakwa sahihi ya umma badala ya matakwa ya serikali kwenye katiba basi uvumilivu wetu kuwapa muda zaidi ni mpaka hapo April 08, 2011 ambapo baada ya hapo mtakua mmetushinikiza kwenye mfululizo wa maandamano mpaka kieleweke.
   
 2. e

  emma 26 Senior Member

  #2
  Mar 31, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Na Rabia Bakari

  MBUNGE wa Jimbo la Ubungo (CHADEMA), Bw. John Mnyika amedai kushtushwa na maudhui ya muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa
  mwaka 2011 uliochapwa katika Gazeti la Serikali toleo No. 1 Vol. 92 la Machi 11, mwaka huu, akidai kuwa hauna nia ya dhati ya kuleta mabadiliko ya katiba.

  Bw. Mnyika alisema jana kuwa kilichomshtua zaidi ni mamlaka makubwa aliyonayo rais katika muswada huo, ambapo maudhui yamedhihirisha tahadhari aliyotoa mara kadhaa kwamba serikali haina dhamira ya kweli ya kuhakikisha panakuwepo na mchakato mzuri wa kuwa na katiba mpya.

  Alisema kuwa muswada huo umelenga kuhalalisha yote ambayo yalitangazwa kufanywa na rais kuhusu mchakato wa katiba mpya na kupingwa na wadau mbalimbali, ambapo sasa yanataka kupewa uhalali kwa sheria inayotaka kutungwa na bunge kupitia muswada huo.

  "Muswada huo unataka kumpa mamlaka rais ya kuunda tume ya kuongoza mchakato mzima wa katiba bila kuhusisha bunge ama wadau wengine wa msingi. Muswada huo pia utaka kumpa rais mamlaka ya kuteua wajumbe wa tume husika bila kushauriana na mtu yoyote isipokuwa Rais wa Zanzibar.

  Muswada huo unaelekeza kuwa katika kuteua wajumbe, rais atazingatia uwakilishi wa makundi ya kijamii, lakini makundi husika hayatajwi hata kwa ujumla wake na hivyo kuacha mamlaka yote ya kuamua uwakilishi kubaki kwa rais," aliongeza.

  Mambo mengine yaliyomo kwenye muswada huo, Bw. Mnyika aliyataja kuwa ni pamoja na kumpa rais mamlaka ya kutengeneza hadidu rejea za tume jambo ambalo lilipaswa kufanywa na bunge kwa kuwa sehemu ya sheria husika ama kufanywa na Mkutano Mkuu wa Kikatiba.

  Aliongeza kuwa kwa kutoa mamlaka ya kuunda hadidu rejea kwa rais mwanya umetolewa kwa mtu mmoja kuweka mipaka ya nini kinastahili kufanywa na tume wakati wa mchakato wa katiba mpya na hivyo kuminya wigo wa mabadiliko.

  "Muswada huo unataka tume iwasilishe ripoti yake kwa rais ambaye atampa nakala Rais wa Zanzibar na baadaye kumwelekeza waziri mwenye dhamana kupeleka bungeni yale atayoamua rais. Muswada huu kwa kuwa na kifungu hiki utaendeleza yaliyofanywa na marais waliopita kuhusu ripoti na mapendekezo ya tume zingine na hivyo kukwamisha mabadiliko ya kweli," alisema Bw. Mnyika.

  Pamoja na hayo, aliongeza kuwa muswada huo unataka kutoa mamlaka finyu kwa jukwaa linalohusiana na mambo ya katiba tofauti na mkutano mkuu wa kikatiba ambao ungekuwa na mamlaka zaidi katika mchakato husika.

  Aidha kwa mujibu wa Bw. Mnyika pia, muswada huo unataka kutoa mamlakama kubwa kwa rais kuteua wawakilishi wa chombo kikuu zaidi katika mchakato wa katiba bila kushauriana na kundi lolote ama wananchi kuhusika katika uteuzi ama kuwa na wawakilishi walioteuliwa na makundi yenyewe, mathalani vyama vya siasa, asasi za kiraia, taasisi za dini, vyama wa wakulima, vyama vya wanafunzi, vyama wa wafanyakazi na wengineo.

  Alisema muswada huo unataka Rais ashauriane na Rais wa Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pekee ambapo pia unatoa mamlaka makubwa zaidi ya rais kuamua hata kufanya bunge la kawaida kuwa ndilo bunge la katiba, jambo ambalo linaweza kurejesha udhaifu uliofanywa katika mchakato wa katiba inayotumika sasa ambapo umma uliporwa wajibu na mamlaka yake ya kushiriki moja kwa moja katika kupitisha katiba.

  "Muswada kwa ujumla haujaeleza muda wa mchakato wa katiba na vipindi vitavyotumiwa na vyombo mbalimbali katika hatua mbalimbali za mchakato wa katiba; ama kutoa mamlaka ya kuwekwa kwa muda huo kwa chombo chenye uwakilishi mpana wa umma kama mkutano wa katiba au bunge na hivyo kutoa mwanya kwa mchakato mzima kucheleweshwa," alisema.

  Bw. Mnyika alikumbusha kuwa mnamo Februari 9 mwaka huu, alitoa tamko kuwa alipokea kwa tahadhari uamuzi wa Serikali kupitia kwa Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kubadili misimamo ya awali kuhusu mchakato wa katiba mpya na kuamua kukubaliana na mwito wa kutaka mchakato husika uanzie bungeni kupitia kutungwa kwa sheria ya bunge ya kuratibu na kusimamia mchakato husika kama alivyokuwa akitoa mwito kwa nyakati mbalimbali.
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kongamano la Katiba lilivyoleta msisimko
  [​IMG]

  Nasra Abdallah

  HIVI karibuni Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) iliandaa kongamano kuhusu mchakato wa uundaji wa katiba mpya.

  Katika kongamano hilo watoa mada wakuu walikuwa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Issa Shivji na Mwandishi mkongwe wa habari, Jenerali Ulimwengu ambao walianza kuchokonoa mada kwa kueleza historia, dhana na haja ya kuwa na katiba mpya.
  Profesa Shivji anasema lengo la kuanzishwa kwa Udasa ni kutetea maslahi ya wanyonge kwa kuendesha mijadala yenye maslahi kwa taifa itakayojenga hoja na si jazba hivyo suala la kujadili uundwaji wa katiba mpya ni kati ya jukumu lao.

  Maana na dhana ya Katiba

  Anasema zimekuwepo tafsiri nyingi kuhusu maana ya katiba ikiwemo ile inayosema ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa, tafsiri ambayo kwa sasa inaonekana kupitwa na wakati.

  Anafafanua kuwa maana sahihi na dhana ya katiba ni kielelezo cha muafaka wa kitaifa ambapo jamii, watu watakubaliana misingi mikuu ya kiuchumi na kijamii katika kuendesha nchi yao.

  Chimbuko linatokana na wananchi hivyo katiba itabaki kuwa mali ya wananchi, hivyo kutokana na uundwaji wake na ni muhimu katiba ikapita mikononi mwa wananchi.

  Kwa nini Katiba mpya?

  Anasema zipo sababu zinazosababisha katiba mpya kuundwa ikiwemo madai ya kupitwa na wakati pamoja na kuwepo kwa gazeti moja lililodiriki kuandika mapungufu 90 yanayoonekana katika katiba ya sasa, jambo ambalo iwapo angepata nafasi ya kuorodhesha yangefika 200 .
  Anasema hoja nyingine ni ile inayoonyesha katiba kuwa na viraka jambo ambalo serikali inaweza kuifanyia tu marekebisho.

  Profesa Shivji anasema kuwa kama ndivyo kuna katiba za nchi nyingine ambazo zinamiaka mingi ikiwemo ya India ambayo ina miaka 60.
  Anasema kwamba wengi wanaotoa kasoro hizo hawajasoma katiba ya sasa vizuri.

  "Kwangu mimi sioni kama katiba ina mapungufu ila ninachohitaji ndugu zangu ni kuundwa kwa katiba mpya hoja kubwa ikiwa ni kwamba zote zilizopita hazikushirikisha wananchi kama ambavyo tafsiri inasema," anasema.

  Historia fupi ya katiba iliyopo

  Profesa Shivji anasema kwa kipindi cha miaka 50 tangu tupate uhuru, nchi ishawahi kuwa na katiba tano ya kwanza ikiwa ya mwaka 1961 iliyojulikana kwa jina la katiba ya uhuru ambayo ilitungwa na Waingereza kwa maslahi yao.

  Katiba nyingine ni ya mwaka 1962 ambapo ilitungwa na Bunge la wakati huo na kupitishwa kama sheria kuu ambapo wakati huo wabunge 71 walikuwa wanatoka chama cha TANU.

  Katiba ya 3 ni ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyokuwa na lengo la kupatanisha muungano na Rais ndiye aliyepewa madaraka ya kuitunga.

  Pia anasema mwaka 1965 Bunge lilitunga katiba ya 4 ambayo iliitwa katiba ya chama kimoja na ya 5 ni ile ya mwaka 1977 chimbuko lake likiwa ni mapatano ya Muungano, ambapo ilijadiliwa kwa saa 3 tu na kupitishwa kuwa sheria mama.

  Kwa mujibu wa Profesa Shivji anasema katiba hizo zote hazijashirikisha wananchi na hivyo hazikuwa na uhalali wa kuwepo. Anasema katiba itakayoundwa ni muhimu ikashirikisha wananchi ndiyo itakuwa uhalali wa kisiasa na kisheria ili wapate katiba yao.

  Profesa Shivji anaeleza kuwa mchakato huo lazima wananchi waachwe wajadili, waelimishwe bila ya kutishwa ili waanze na mijadala midogomidogo na kuhitimisha kwa mkutano mkuu.

  Anasema mchakato wa pili unatakiwa kupitia bungeni na kumalizia kwa mkutano wa kura za maoni kama chombo maalumu cha maamuzi ya uundwaji wa katiba mpya.

  Hata hivyo anatahadharisha kwa vyama vya upinzani kutokubali suala la mjadala wa uundwaji wa katiba mpya lipelekwe bungeni kwa kuwa ni sawa na kuamua hoja hiyo ikaamuliwe na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao wana viti vingi.

  Anasema ni bora suala hili likabakia mikononi mwa wananchi na kwani itakuwa rahisi kutoa shinikizo kwa rais katika kuundwa katiba hiyo kuliko kushinikiza Bunge. Anavitaka vyama vya siasa kuangalia suala hilo kwa upana zaidi badala ya kuingiza siasa zaidi.

  Hoja Shivji ilikuja baada ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA), kuonyesha wasiwasi juu ya kutaka lipelekwe bungeni kwanza kwa madai ya kufanyiwa marekebisho baadhi ya vipengele vya sheria Ibara ya 98, inayosema Bunge ndilo lenye mamlaka ya kubadilisha katiba.

  Hata hivyo Shivji akitolea ufafanuzi hoja hiyo anasema bunge halina uwezo wa kupinga katiba na kwenye katiba hakuna sheria inayopinga mjadala wa kitaifa kama huu wa kujadili katiba mpya.

  Anasema hata ikitokea mchakato huu ukapelekwa bungeni, kamwe sheria hizo hawawezi kuzifanya zibadilishwe.
  Kwa upande wake kada wa CHADEMA, Mabere Marando, anasema kuwa mpaka sasa katiba mpya imeanza kuandikwa kutokana na tukio la vurugu zilizotokea hivi karibuni mjini Arusha.

  Marando anasema damu iliyomwagika katika vurugu hizo ndio wino wa kwanza wa kuandikia dibaji ya katiba hiyo huku harakati zikiendelea.
  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, anasema mada aliyoitoa Profesa Shivji kwamba uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa na uhalali kutokana na kupendwa na sio katiba iliyomuweka madarakani, lakini hakuelezea kuhusu uhalali wa viongozi waliomfuata nyuma.

  Lipumba anasema katika ilani ya CCM hakukuwa na suala la katiba wala katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa bungeni hapakuwa na suala hilo hivyo kuna haja ya kuwa na mshikamano katika suala hilo kwani bila ya hivyo nchi inaweza kuingia kwenye machafuko.

  Kwa upande wake, Jenerali Ulimwengu anasema katiba msingi wake ni falsafa za Waingereza na kuongeza kuwa pamoja na mabadiliko mbalimbali yaliyowahi kufanywa hakuna hata katika mabadiliko hayo kushirikisha wananchi.

  Ulimwengu anasema haoni kama kuna gharama kubwa ya mchakato wa kuundwa kwa katiba ukilinganisha na machafuko yanayoweza kutokea baadaye.

  Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Ananilea Nkya, anaonyesha wasiwasi wa ushiriki wa wanawake katika mjadala huo wa uundwaji wa katiba mpya.

  Anasema kwa muda mrefu anafuatilia mijadala hiyo hata katika vyombo vya habari lakini suala la ushirikishwaji wa wanawake limekuwa dogo ukilinganisha na wanaume.

  Anaitaka serikali kuhakikisha inawekeza kwa wananchi ili kujua ni nini kilichopo katika katiba iliyopo kwanza kwa kutumia redio, televisheni na magazeti inayoyamiliki kwa kutoa elimu kupitia vipindi mbalimbali.
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0


  Kwa nini ghafla tu Mhe Kikwete aingiwe na hamu ya kutuandikia Katiba;jambo ambalo hata siku moja haikuwahi kuwa kwenye ndoto yake wala ya chama chama chake????

  Nia na harakati za wananchi kujiandikia katiba mpya ikitekwa na mtu yeyote, aanze kufanyia kazi chumbani kwake peke yake na wale waalikwa wake pasipo kupitia bungeni na kushirikisha wananchi wote tangu hatua za awali, na kwamba CCM ichezee juhudi hizi hata uchaguzi mkuu 2015 ikafanyika bila katiba mpya ya kuandikwa moja kwa moja na wananchi, basi Maafa yajayo kitaifa tusijesema yametushwa kitu wakati sasa hivi tunaliumba wenyewe.
   
 7. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Demokrasia ya kweli ambayo JK alidai kuimarika nchini INAKATAA KABISA SOLO-DANCE KIND OF DECISIONS. Na hili hata Dr Benson Bana analifahamu sana na alipashwa kulizingatia alipokua akimshauri raisi.

  The backfire of this strategy to seek to play political cards on the constitution is bound to be too dear and very fatal on the sponsors of the 'Ikul Avenue' school of thought over constitution need to change immediately for that of 'Bunge Avenue'.

  Kwa nini Mhe Kikwete anawakimbia wabunge, anaogopa nni kule bungeni??? The World is eagerly waiting to see for itself how independent and honourable is the Parliament of the United Republic of Tanzania when it comes to giving direction to an ENTIRELY DEMOCRATICALLY PEOPLE-CENTRED NEW CONSTITUTIONALISATION in our country.
   
 8. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0

  Nguvu ya Umma isiyoratibiwa imeanza kufanya kazi nchini


  Wednesday, 30 March 2011 10:52


  [​IMG]

  Editha Majura

  KILA kona nchini Tanzania yanasikika malalamiko ambayo msingi wake ni ugumu wa maisha ambao unasababishwa na mambo kadhaa wa kadhaa. Wanasiasa nao wanahaha kutafuta kuungwa mkono na wananchi kwa lengo la kushika au kuendelea kuwa madarakani.

  Harakati hizo za kisiasa zinafanywa kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na semi na mitindo anuai, mathalani kujivua gamba, operesheni sangara, operesheni zinduka na nyinginezo.

  Lengo la kila Chama ni kuufikia na kuuhamasisha umma ili ukiunge mkono.Harakati hizo hivi karibuni zimeibua dhana kwamba nchi inaweza kupoteza amani kutokana na baadhi ya mbinu zinazotumiwa na wanasiasa. Inadhaniwa kuwa nguvu ya umma inaweza kuchochewa kwa lengo la kuuondoa uongozi uliopo madarakani.

  Hata Rais Jakaya Kikwete, akihutubia taifa mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu, alikishutumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwamba maandamano na mikutano ya hadhara ya nchi nzima kinayofanya ambayo ilianzia mikoa ya Kanda ya Ziwa ina ajenda ya siri ya kutaka kuuondoa uongozi wa nchi madarakani isivyo halali.

  Mtaalamu wa siasa ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bashiru Ally, anabainisha kuwa nguvu ya umma siyo dhana hamasishi bali huleta maana inapohalalisha mapambano dhidi ya mfumo unaothibitika kuumiza umma. Anasema nguvu ya umma hailengi mtu, chama wala kundi fulani la watu.

  Ally anasema nguvu ya umma kabla haijafikia hatua ya kuleta mabadiliko, hutafakari na kubaini kuwa madhara yanayoipata kutoka kwa kundi, mtu au chama fulani yanatokana na mfumo, hapo ndipo nguvu ya umma huratibiwa kukabiliana na mfumo huo na kwamba siyo lazima uongozi ulio madarakani uondolewe, ingawa hutokea mabadiliko makubwa ndani yake.

  Vuguvugu la nguvu ya umma nchini linaweza kuleta mabadiliko ya kiuongozi?
  Ally anasema Tanzania ni sawa na Chuo Kikuu cha nguvu ya umma kwa sababu hata uhuru wake ulipatikana kwa nguvu hiyo, nembo ya chama tawala (CCM) yaani ni jembe na nyundo inamaanisha nguvu ya umma (wakulima na wafanyakazi).

  "CCM kipo kwa nguvu ya umma. Asili ya Tanzania ni kuongozwa kwa nguvu ya umma bila shaka unakumbuka enzi za Hayati Mwalimu Nyerere…, matatizo yalianza miaka ya 80 baada ya serikali kuingia kwenye mtego uliovishwa vazi la biashara huria…, ambao unalazimisha serikali kulinda maslahi ya mwekezaji badala ya maslahi ya umma," Ally anaeleza.

  Anasema ili nguvu ya umma isababishe mabadiliko yenye kuleta manufaa, lazima iratibiwe ingawa yeyote anayejipa jukumu hilo lazima akumbane na kigingi cha kuitwa mchochezi. Hata hivyo iwe isiwe, pale nguvu ya umma inapohitajika inatokea tu kwa sababu hakuna mwenye uwezo wa kuzuia matakwa ya umma.

  " Yeyote anayejitolea kuunganisha umma ili ukabiliane na mfumo kandamizi ni lazima adhibitiwe kwa kuitwa mchochezi lakini nguvu ya umma haidhibitiki, wakati unapowadia umewadia," Ally anabainisha.

  Katika hali ya kawaida nguvu ya umma huratibiwa kupitia makundi maalumu katika jamii, kama vile vikundi vya wanawake, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima; Ushirika, vyama vya vijana na vile vya kiraia kwa lengo la kupinga mfumo ambao umethibitika kukandamiza jamii.

  Awali kila kikundi hufanya mapambano peke yake kwa namna inavyoonekana inafaa, lakini malengo yanaposhindikana kufikiwa, ndipo umuhimu wa kuungana unapoonekana na hatua za makundi hayo kuunganisha nguvu dhidi ya mfumo husika inapotekelezwa.

  Hatua hiyo ya kuunganisha nguvu ya vyama na vikundi vyote ndiyo inayoonekana kuwa ngumu hapa nchini na hivyo kuashiria hatari ya kuibuka nguvu ya umma isiyoratibiwa. Hatari hiyo inatokana na makundi hayo ambayo kwa kujua au kutojua, kugawanyika, jambo linaloleta ugumu katika kuwezesha uratibu wa nguvu ya umma.

  Kwa mfano vyama vya wafanyazi, vimegawanyika na kila kukicha vinashambuliana kwa namna tofauti. Kadhalika vile vya wakulima, wafanya biashara, wanawake na hata vyama vya vijana.

  Ally anasema ili nguvu ya umma ilete matunda bora kwa jamii ni lazima vikundi hivyo viungane kwa nia moja tu ya kukabiliana na mfumo bila tofauti za kisiasa, kidini wala kabila.

  Mtazamo wa Ally kuhusu vyama vya siasa kusababisha nguvu ya umma kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchini ni kwamba hilo haliwezekani kwa sababu wanasiasa karibu wote hawaumizwi moja kwa moja na ubovu wa mifumo ya huduma kwa jamii.

  Aidha jamii ya Watanzania imeng'amua kuwa dhana wakilishi haina uwezo wa kuikomboa dhidi ya mifumo kandamizi hivyo linalotarajiwa ni jamii yenyewe kuondoa tofauti zake na kuungana kwa lengo la kujiletea mabadiliko, kwa maslahi yake yenyewe.

  "Jukumu la kuwa na uongozi bora ni la umma wenyewe, umma wenyewe hutekeleza jukumu lake la ama kuuondoa madarakani uongozi uliopo au kushinikiza yafanyike mabadiliko makubwa," Ally anaeleza.

  Hata sasa nchi inapitia kipindi cha mabadiliko yanayotokana na nguvu ya umma isiyoratibiwa. Ally anatoa mfano mmoja wapo kuwa ni matibabu yanayotolewa na aliyewahi kuwa Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, (KKKT), Ambikile Mwaisapile, Loliondo mkoani Arusha.

  Mwaisapile almaarufu Babu, alianza kutoa tiba ya magonjwa yote sugu ukiwamo UKIMWI siku nyingi lakini tiba hiyo imepata umaarufu mkubwa baada ya vyombo mbalimbali vya habari kutangaza shuhuda za baadhi ya waliokunywa na kuponywa na tiba hiyo ambayo hutolewa kwa kipimo cha kikombe kimoja tu.

  Kufuatia shuhuda hizo kutiwa nguvu na baadhi ya madaktari baada ya vipimo kuonyesha maradhi yaliyokuwa yakiwasumbua hayapo tena, idadi ya watu kuelekea kwa babu kunywa kikombe cha dawa iliongezeka kwa kasi kubwa. Katika kinachosadikiwa kuwa ni serikali kutekeleza jukumu lake la kulinda raia dhidi ya hatari au ashirio la hatari, ilitangaza kuzuia tiba hiyo.

  Hata hivyo Serikali ya Mkoa wa Arusha ilitamka wazi kuwa ni vigumu kutekeleza uamuzi huo kwa sababu ya wingi wa watu wanaoamini na kufuata tiba hiyo. Baadaye Uamuzi huo ulilegezwa na mpaka leo matibabu yanaendelea. Ingawa tiba inatolewa kwa imani, wanaotibiwa hawabaguliwi kwa imani zao.

  Kilichozuia Serikali kushindwa kutekeleza jukumu lake hilo ni umoja wa watu ambao haujali tofauti zao za dini, siasa, umri, jinsia, elimu wala kabila bali unaoashiria kukosa imani na mfumo wa kisayansi duniani katika kutibu magonjwa sugu badala yake kuamini tiba inayotolewa na babu Mwaisapile. Ally anasema huo ni mfano halisi wa jinsi nguvu ya umma inavyofanya kazi.

  SOURCE: Nguvu ya Umma isiyoratibiwa imeanza kufanya kazi nchini
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Re: Mufti Mkuu ana siri nzito kuhusu CHADEMA? 3.4.2011 kuteta tena na maimam Dar

  Tatizo lako wewe ni kwamba uko bize sana kuwatisha jamii isiotishika hata nyuklia; unawatisha watu ambao utahitaji miaka mingi sana kuwaelewa kwamba wameumbwa na udongo wa aina gani na kufunikwa na nguvu zipi.

  I see, yours is just but more than a sweet fantasy story - go and tell it to the birds!!! Tangu lini shirika la CCM iitwayo BAKWATA, sawa tu na UVCCM ikawa ni kinara wa ndugu zetu Waislam nchini?? Waislamu safi wasionunulika kwa mafisadi tunawafahamu sana, tunawaheshimu sana na wala hata siku moja hawawakilishwi na makeke za kitapeli ka hizi unazoleta wewe hapa JF.

  Kawambie waliokutuma kwamba hata kule CHADEMA Waislamu wapo na ni waumini wazuri wasiotawaliwa maisha yao BAKWATA-CCM bali unyenyekevu na utii wao ni kwa Allah tu.

  [​IMG] Originally Posted by Muhadhiri [​IMG]
  mbona sijasikia tzdaima likumtukana kardinal? naona mufti mara anawatumia waislam. mara humu jf hana elimu.kama mnamuheshimu hayo yote ya nini? twende msikiti farouq tukamsikilize   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MAGWIJI HAWA WA JF WAKO WAPI??

  Zakumi, Father Masanilo, Puretta na Malecela mko wapi siku hizi wenzetu?? Ndio tuseme mumeamua kuegesha jumla??

  I for one is greatly missing your critical minds around just in a very deep way.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Eti Watanzania wala hawana mpango wowote na katiba mpya na kwamba kwanza hata hawajui nini hicho????????????? This is too sick and mos irritating for someone to utter in his mouth!!!!!!!!!!

  Sasa mtajua kwa vitendo kwamba kumbe suala la katiba mpya haswaaa ndio mapigo yetu ya moyo kila mmoja wetu nchini na kwamba haki yetu tutaitetea kwa gharama yoyote ile!!!!!!!!
   
Loading...