Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Kwa mujibu wa tangazo liliroshwa na star tv,kesho TBC1 kwa kushirikiana na Star tv,wataonyesha moja kwa moja sherehe za kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi(CCM) zitakazofanyika mjini Singida kesho na mgeni rasimi atakuwa mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Raisi mstaafu Jakaya Kikwete.
Binafsi sina shida na TBC1 kuonyesha live sherehe hizo, ila nachotaka kujua ni fedha kiasi gani CCM wameilipa TBC1 na tunawataka waonyesha nyaraka za malipo hayo kwani wote tunakumbuka uamuzi wa hivi karibuni wa serikali kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kwa kile tulichoambiwa ni TBC1 kutumia fedha nyingi(bilioni 4 kwa mwaka) kurusha matangazo hayo live na hivyo kuigharimu serikali fedha nyingi.