CCM, tuonee huruma, hatutapendwa kwa kuburuza vyama vingine bali tujisafishe sisi wenyewe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM, tuonee huruma, hatutapendwa kwa kuburuza vyama vingine bali tujisafishe sisi wenyewe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAKUNDA, Sep 4, 2012.

 1. M

  MAKUNDA Senior Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetumia muda mwingi kutafakari hali ya kisiasa inavyoenedea hapa nchini.

  Napenda niweke wazi kabisa mimi ni mwana CCM na ni mwanachama hai maana hata kadi yangu imelipiwa ada hadi mwaka 2014. Katika hali ya kutafakari nimepata kuona kuwa sijambo la kuficha tena na katika hili CCM inaelewa wazi kuwa upepo wa kisiasa kwake hauendi vizuri na chama kinachoelekea kuchukua nafasi yake ni CHADEMA. Nitakuwa mnafiki sana iwapo nitashindwa kukiri ukweli huu kuwa hoja za kitaifa zinazotolewa na CHADEMA, hasa matatizo yanayoikabili nchi yakihusishwa na CCM ni ukweli mtupu.

  CCM imeruhusu ufisadi kuwa utamadunu wake, watu wanakwapua raslimali za nchi huku umma wa watanzania ukiteseka katika hili CCM ielewe wazi kuwa watu hawako tayari kuona jambo hili linaendelea. Nimekuwa nikihudhuria vikao mbalimbali vya chama moja kati ya ajenda ambayo sasa inaelekea kuwa ya kudumu ni juu ya kwanini CCM imepoteza mvuto kwa watu.

  Roho yangu huwa inaniuma maana swali hili majibu yake tunayo lakini tunajidai kupapaza kama vile hatuoni. Najua kuwa it is too late kwa CCM sasa hivi kujisafisha, la maana ni kuandaa exit plan chama kingine kitawale nchi kwa mfumo ulio wa kidemokrasia badala ya kuwa na kushikiana mitutu kwa ukaidi tu. Sasa hali mefukia katika climax, chama kimeanza kutumia vyombo vya dola ku-suprees demokrasia hadi kusababisha mauaji, hasa hili ndilo limekoleza chumvi kwa wanachi kuichukia CCM, hata mie nimesikia uchungu mwingi kiasi cha kuona kuwa nashiriki katika utendaji dhambi iwapo nitaendelea kuiunga Mkono CCM.

  Eee, Mungu naomba unisamehe maana najiona msaliti wa umma kwa kendelea kuwa mwana CCM.

  Najua wapo wanazi wasiopenda ukweli wanaweza kusema najifanya kuwa mwana-CCM wakati ni mwanachama wa chama kingine hasa CHADEMA inayotisha kwa jinsi inavyokubalika kama moto kwenye kichaka kikavu. Napenda niwahakikishie mie ni mwana-CCM wakati ukifika nitajitambulisha.

  Wana JF hebu angalieni hili, daima ukiona timu inacheza defensive game ujue mambo yameiendea kombo, timu inayojiamini upeleka mashambulizi mbele huku ikijilinda isifungwe. Hii ndiyo hali iliyonayo CCM, kwa wakati huu haina hoja yoyote ya kupeleka maashambulizi mbele, bali imabaki kueleza oho! CHADMEA hao ni wapuuzi, hata wao wakipewa nchi watafanya hayo hayo, tusikubali kurubuniwa n.k Hoja za nguvu ziko wapi CCM? Sikubaliani na hali hii na wito kwa wana- CCM wenzangu, taabu na shida haziangalii unavaa rangi gani, dhiki na tabu zinatukumba wote hivyo kutokubali ukweli huo ni ujinga na uzandiki.

  Hivi CCM, jiulize Mtoto wa Kikwete RZ1 kapata mtaji wapi wa kuweka vituo vya mafuta nchi nzima na malori lukuki?Lakini Jua watanzania wanaona! Najihisi uchungu sana hasa ninapoona wanachi vijijini wanashinda porini kwa kujificha ili wasitkamatwe kwa kutolipa michango ya ujenzi wa sekondari ya Kata, huku wapo watu wanao jichotea mabilioni ya Hela ambayo yangetosha kujenga vishule vyote vya Kata bila kudai senti kwa mwnanchi.

  TUMECHOKA, TAFADHALI ENDELEZA MASHAMBULIZI MTUKOMBOE, HUKU MKIJIHADHALI MSIJE MKASAMBARATISHWA kwa mbinu za vyombo vya CCM.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Mkuu mawazo yako ni mazuri sana,lakini hao mabwepande wamejisahau siku wakishtuka kutakuwa kumekucha.Ujumbe wako ni murua kabisa
   
 3. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,380
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Sasa Mkuu kulia lia hakusaidii!
  Una onaje uka jivua gamba kabisa maana umekiri kua chama cha mwabwepande hakiuziki!
  Tafadhali kiongozi hebu jipime then uchukue hatua!
   
 4. m

  manduchu Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa hili la kutumia dola kuikandamiza cdm, limesaidia sana kukipa chati cdm na kufanya wananchi wachukie ccm.
   
 5. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nina wazo.Kwanini wapenda amani na maendeleo ya nchi na haki walioko kwenye vyote wasiungane pamoja ili kuikomboa nchi hii? Nami ni mwana CCM lakini napenda haki sitaitetea CCM inapofanya hujuma na kuuwa watu. Kuua ni dhambi mbaya sana na inaleta laana kwa taifa. Hayashime wanaCCM wote wanaopenda amani tukatae hii move inayoendekezwa sasa ya kuua raia. Hivi Nape yupo wapi mbona kawa kimya sana au mafisadi wameshamgaragaza?
   
 6. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,182
  Likes Received: 10,534
  Trophy Points: 280
  Ccm haina tena mvuto kwa wananchi...Lolote wanalojitahidi kufanya kwa ajili ya chama chao linawageuka na kuwamaliza.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kwanza nikupongeze kwa bandiko zuri, pili kwa kuwa mkweli kiitikadi, tatu kwa kutoegemea itikadi yako na nne ni kuitakia mema nchi yako.

  Mngekuwa na uhuru wa kutoa mawazo ndani ya ccm, huu ulikuwa wakati muafaka wa kuandamana kupinga mauaji ya raia, mngeandamana ccm nchi nzima kumwambia mwenyekiti wenu kuwa hamkumchagua kuwa mwenyekiti kuiongoza serikali kuua raia wake, mngemtaka akomeshe hilo mara moja, achukue hatua dhidi ya wote wanaotuhumiwa kuihalifu sheria na haki za binadamu.

  Lakini kwa kuwa mambo ni kinyume chake, haishangazi kuona ccm ikijinyonga yenyewe! hatukuwa na sababu ya kuisikitikia, lakini tufanyeje! hakuna jinsi.

  Mkuu MAKUNDA, ukipata nafasi umshauri mwanakijiji mwenzio mwigulu nchemba asiendelee kuwaaibisha kaka na dada zenu wanyiramba, mnapoteza heshima ya kabila lenu mbele ya jamii, mnapitwa kwa mbali sana na watani zenu wanyaturu wanaopaishwa na Tundu Lisu anayetetea wanyonge, mwigulu anatetea wauaji kwa nguvu zake zote!!! What a shame!!!!!!!!

  Mwisho nakubaliana na akili yangu kuwa kwenye akili yako kuna maarifa, usikawie, yatumie haraka uingie nawe kwenye historia njema.

  Kama kweli uovu unakukera uambie umma leo, ni kweli ama la kuwa mwalimu Ntaandala na mwenzie ndio walimsaidia Lameck madelu kurudia shule ya msingi na kuitwa mwigulu nchemba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Nikupongeze kwa kusema ukweli kwamba CCM itafute njia ya kuondoka madarakani kwa amani. Baada ya utawala wa muda mrefu,matatizo yote ya nchi hii inatuhumiwa CCM! Na huo ndio ukweli! Busara ni kuwapisha wengine! Kuendelea kulazimisha kutawala ni kutaka kubomoa taifa na mauaji tunaanza kushuhudia! Kuanzia jana na leo naongea na wana CCM wa ngazi tofauti,wote wana huzuni na hasira na tukio la jumapili kule Nyololo Iringa. Nawashangaa baadhi ya watetezi wa CCM humu kutetea uhalifu ambao wenzao huku mitaani hawakubaliani nao.
   
 9. m

  masluphill Senior Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Mh umemalizia na manenomazito hongera sana kwa ma info haya.Kijana mwingine mwenye issue na info za uhakika kuhusu hili la ''TUPOI'' kubadili jina ili afaulu shule AZIMWAGE tumchane,waliosoma nae P'se fanyeni kweli kwa maslahi ya taifa tummalize mpambe wa mafisadi.
   
Loading...