CCM tunahujumiwa na Makundi lakini wananchi bado wana Imani na sisi: Daima CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM tunahujumiwa na Makundi lakini wananchi bado wana Imani na sisi: Daima CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vijijini Lawama, Apr 13, 2012.

 1. Vijijini Lawama

  Vijijini Lawama JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 300
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nashindwa kuelewa nikisikia viongozi na wanachama wa CCM wakisema kuwa kinachowapa ushindi CDM ni makundi ndani ya Chama hicho.CCm ni chama kilichojaa wasomi wenye mashahada ya ajabu sana. Hivi unahitaji kumulikiwa na tochi kujua kwamba CCM wameshindwa kuongoza nchi na kuwaletea wananchi ustawi wa kijamii na kiuchumi na hiyo ndo chuki kubwa ambayo inawafanya washindwe katika chaguzi za hivi karibuni? Wasomi wa magamba wako wapi? Na magamba hawana tena uwezo wa kubadili hali hii kwa sababu tayari nchi inatembelea mguu mmoja kiuchumi wemekwiba vya kutosha na hawawezi tena kujenga viwanda na makampuni yaliyoachwa na wakoloni kwa muda mfupi ili kuishawishi jamii kuwaamini tena. Huduma za kijamii zimezorota na hata maisha yamekuwa aghali na jibu lao kubwa ni kuanguka kwa uchumi wa dunia, je uchumi wa dumia umeanguka Tanzania tu ambako mfumuko wa bei mkubwa kuliko.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  CCM inakufa kifo kibaya sana
   
 3. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unamaanisha kifo cha brain concussion
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  mimi mtu akitaja ccm ananichefua sana,ni sawa na kunitajia kibwetere,idd amin,adolf hitller,musolini,nk
  wote hao walianza vizuri ila walivyomalizia sitaki hata kusikia.
   
 5. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Ccm haitakiwi kufa kifo cha moja kwa moja, kinachotakiwa ni kuipa LIKIZO YA KUTAWALA FOREVER, huku ikiwa inapumlia i.c.u. Hukumu itajitolea yenyewe, 2015 ni mbali sana, lakini tutafika japo si wote tulio na hasira na ccm.
   
 6. engwe1980

  engwe1980 Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jamani CCM hakika inakufa na kifo chake ni kibaya mno! CDM ikae imara isije ikawapokea wale ambao watajifanya wanajitoa CCM na kujiunga na CDM pindi ikikaribia uchaguzi wa 2015. Wengi ni wachumia tumbo, kumbuka walivyo mtosa Mpendazoe.
   
Loading...