CCM: Tunafuatilia mienendo ya viongozi wetu wanaopotosha umma, kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wetu

Ntashangaa president Samia na Mohamed mcherenga , na Shaka , na mkuu wa TISS, Kama wataacha kumshughulikia huyu taperi mmoja asiye na heshima kwa mamlaka,

Wakimuacha wajiandae atafanya upuuzi na dharau zaidi ya hizo..

Gwajima inatakiwa itumike namna Kama yakufuta maandishi kwenye kitabu, azimwe tu, Ni mtu hatari sana
BAVICHA mnaumiaje na mambo yanayotokea CCM?
 
Ingawa alijitetea kuwa maoni yake ni ya binafsi kama mtu wa Mbinguni na si kama mbunge wa Kawe.
 
  • Kicheko
Reactions: G4N
Kwanza ifahamike wametoa maoni na msimamo wao na kile wanachokiamini. Kutaka kulazimisha anachosema Rais kiwe ni sheria na amri inaonyesha ni kwa namna gani hamjastarabika.

Hata Magufuli alifanya hivi kwa Makamba, Nape na wengine na tuliona namna uwajibikaji na mlengo wa siasa zetu ulikoelekea. Wacheni watu wazungumze wanayoona yanafaa.

Kama kisheria wamekosea waambieni wamekosea sheria gani na mchukue hatua according to your laws and scriptures na siyo kuja na maamuzi ya kijima.

Et Rais amesema sasa yeye kama hataki kukosolewa apishe ofisini wapo watakaokubali kukosolewa. Hatutaki kurudi kule tulipokuwa asee, huwezi kujibu hoja nyamaza na usilazimishe kukubaliwa kila jambo.

Jenga hoja watu wapate mantiki then watachambua na kupata ukweli. Badilikeni wazee wana huku hatuwaelewi kabisa. Mkiona kukosolewa hamuwezi tingisheni nyama msepe.
 
Paruaneni wenyewe yameshatokea makundi ambayo hayatarudi nyuma hesabu inapigwa 2025
 
Kumekucha!

Gwajima na wale wa Tozo za miamala: bila shaka Madelu na Jobo, sasa ni rasmi watakuwa wuamekalia Kuti Kavu:

View attachment 1869356

Kwamba mama keshatoa msimamo na wao wanajifanya vidume? Wao wanadinda na kutoa misimamo yao kwa maslahi binafsi?

Utovu mkubwa huu wa nidhamu kwa madam president ambaye pia ndiye mwenyekiti wa CCM hauvumiliki tena.

Tayari wako kwenye notice.

--------
My take:

Marudio ya sinema ya Diallo na Msukuma yanaonekana yako karibu.

View attachment 1869368

Tusubiri sasa moto faya tokea kwake Chief Msukuma mzee wa mipasho.
Wahutu kwa kujitutumua,eti hii nguchiro nayo inajiita Msukuma,pambaf!
 
Kufukuzwa uanachama na ubunge kwaheri. Hata hivyo ubunge kwake sio issue, alishajitosheleza .
 
Wanaweza wakamzimisha Gwajima Ila tupo wengine tutaongea pia , hakuna haja ya kutishana , kama Mungu alitoa Uhuru Kwa mwanadamu mkaidi , lakini still to-date amepewa Uhuru wa maamuz inakuwaje Sisi wote tunaoenda chooni kuanza kuchimbana mkwara wa kiduwanzi....!!! Gwajima katoa hoja , tupeni side effect ya chanjo , component yake na uhalali wa ku- circulate kwenye maisha ya kibinadamu then anakuja boya mmoja anaita press conference kuchimba mkwara ...
 
Suala la chanjo ya UVIKO ni ajenda ya ulimwengu mzima.

Kila atakayerefusha mdomo kuipinga huishia kufa au kuanguka publically.

Kuna mawili...

1) Utafutwa ubunge

2. Utauliwa.
 
Gwajima ni asset na sio liability, atasamehewa na maisha yataendelea. But huyu atakuja kuwa Mtikila wa pili atasumbua sana na shida yake ni madaraka makubwa zaidi worst case scenarion huyu anatokea kanda ya ziwa ( kanda ambayo ina wapiga kura wengi pia)halafu fitina anazijua. Pili amesimama kutoka kwenye kundi la dini that is why he is an asset and not a liability.
 
Suala la chanjo ya UVIKO ni ajenda ya ulimwengu mzima.

Kila atakayerefusha mdomo kuipinga huishia kufa au kuanguka publically.

Kuna mawili...

1) Utafutwa ubunge

2. Utauliwa.

Mambo yaliyoko nyuma ya covid-19
 
Hawezi kufutwa ubunge, kwasababu Gwajima ni jeuri kuliko Mwenyekiti wa CCM na pia ametumwa na hao hao CCM kumtingisha Rais SSH ili wamweke kwenye tisini asigombee 2025.

Kifupi, Gwajima anatimiza agizo la wana CCM wenye uchu wa madaraka ya urais (Mwigulu Nchemba & Co Ltd In Collaboration With Sukuma Gang) kumfanyia hujuma, figisu na fitina Rais SSH.

Simple logical theory wanayotumia Mwigulu Nchemba & Co Ltd; Rais SSH anatakiwa atingishwe kisawasawa,

1) Afitinishwe na wananchi kwa kupandisha kodi/tozo kwa wanyonge (Miamala Ya Simu, Wakulima, Wavuvi). Hapa ametumika Mwigulu Nchemba.

2) Afitinishwe na vyombo vya Usalama. Hapa ametumika Gwajima.

3) Afitinishwe na dunia nzima kwa kuwapa viongozi wa upinzani kesi za Ugaidi. Hapa vimetumika vyombo vya Police.

4) Akose kuungwa mkono na CCM wenyewe ndani kwa ndani kwa kuona hana msimamo thabit. Hapa itatumika CCM yenyewe kwenye vikao vya NEC taifa.

5) Upinzani wapambishe moto kudai Katiba Mpya. Hapa wametumika Upinzani na Viongozi Wa Kiroho.

6) Mwigulu aanze mapema ya kutafuta point kwa wananchi kwa kufanya ziara yenye msafara kama wa JPM. Atembee kusikiliza kero za wananchi ili wamwone Rais SSH hana time na wananchi na yupo bussy kwenda ziara nje ya nchi kama Burundi. Mwigulu kaishaanza hizi ziara.

7) Mapigo yaanzie Kaskazini - Magharibi (Mwanza) kwa upinzani kudai Katiba Mpya kwa nguvu zote, na ya Mwigulu Nchemba yaanzie kusikini (Mtara - Tunduma) kujifanya anasikiliza kero za wananchi. Wakati Jeshi La Polisi likicheza na Magharibi (Dar Es Salaam) kwa kumshikilia Freeman Mbowe na viongozi wengine wa upinzani kwenye kesi ya Ugaidi. Formation Three In One.

Rais SSH cha ajabu bado hajaisoma sinema hii, akiendelea kuwalea hao viumbe hachomoki kwenye kikaango cha CCM wenye uchu wa madaraka, ndio kwanza 2021 mpaka 2025 ni mwendo masafa marefu na Rais SSH ajiandae kwa kuvaa viatu vizuri tu.

Mtamwonea huruma Rais SSH kwa jinsi mambo yatakavyo mkalia vibaya muda si mrefu. WANAMCHAKAZA NA KUMJERUHI VIBAYA MUDA SI MREFU.
 
Back
Top Bottom