CCM Tumieni akili ya ziada kwenye Propaganda, mnajitia aibu sana... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Tumieni akili ya ziada kwenye Propaganda, mnajitia aibu sana...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hossam, Mar 25, 2012.

 1. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,367
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Wanajamvi,

  Napenda kuwashauri ccm watumie akili ya ziada katika kupiga propaganda zao huko Arumeru kwa kuwa janja ya nyani ishagundulika na zaidi sana wanatia aibu sana.

  Walianza na Mkapa kupotosha umma juu ya Vicent, hapa Mkapa alionyesha ni jinsi gani amechoka kufikiri na ni jinsi gani alivyo mlevi wa ubabe na kuropoka. Binafsi sikushangaa kwa kuwa nawajuwa magamba wasivyoweza kufikiri mbali, mbinu wanazotumia ni za miaka ya sabini enzi zile wenzake na Mkapa walivyoonyesha ufinyu wa kufikiri kwa akili zao kuwatuma wampindue Nyerere, hawa sasa yamewarudia kwa sababu Mkapa sasa anatakiwa kusema sababu zilizopelekea kifo cha Mwalimu. Katika kuingilia mambo ya ukoo yasiyomhusu Mkapa angeishia kuropoka jukwaani tu kwamba 'nina mashaka na uhalali wa Vicent kutumia ubini wa 'Nyerere''. Na akamalizia 'yawezekana huyu akawa Nyerere mwingine na sio baba wa taifa', yeye Mkapa kujifanya kungwi wa ukoo wa Mwalimu sasa kajikuta kajipakaza kinyesi usoni...

  Mwigulu naye haishi mabalaa mara NGO ya kulisha mbwa, mara Nassari ni bachela, yaani ilimradi upuuzi tu na hakuna cha maana. Mwigulu angesema kifupi tu 'hakuna NGO inayoongozwa na Nassari ikaweza kutatua matatizo yote ya Wameru kwa kuwa kila NGO ina malengo yake na ina eneo maalum la operations' hapo angesomeka, kuropoka ***** huo anaonyesha jinsi gani anavyoyumbishwa na siasa za chooni.

  CCM wakakaa na kuamua kuandika ujumbe mchafu wakidai umeandikwa na Zitto. Hivi ni katika kampeni tu ndipo mitafaruku ya vyama huonekana eti eehh?? Hivi hawa magamba walishindwa vipi kutoa vipeperushi tu vinavyoelezea Arumeru na hatma yao wakichagua upinzani? Yaani mijitu mikubwa na akili zao, kwa gharama kubwa na muda wa kutosha wakafikiri hadi mwisho wa akili zao na kuamua kutoa uharo huo? Kweli ya ngoswe kuitwa hivyo mwachie yeye...

  Si hayo tu, huyu Homo habilis naye kaibuka na hoja ya wizi wa Dk Slaa wa michango ya ujio wa papa, yaani katika siku zote kaona leo tu? Mwisho wa akili za Wassira ni kusema 'nimepata habari hizi Vatican', sasa ameona akisema vatican ndio tumuone ana mtandao ama tumuogope? Mbona yeye ni bingwa wa kuuchapa usingizi bungeni, anapata wapi muda wa kufuatilia yasiyomhusu huko vatican, na kama ni kwelu Slaa aliiba michango basi iweje katika waroma zaidi ya milioni 10 wasijue na hali wao ndio walichanga na aje kujua huyu homo habillis?

  Sioi mwenyewe aibu tupu, baba yake hakuweza kuwatatulia kero Wameru ataweza yeye Mkwe wa Lowassa!? Hata kuongea jukwaani ni shida vipi akipewa ubunge si atakuwa kama Haruni na Musa wa agano la kale?

  Tuweni na ustaarabu jamani, hubirini sera za vyama vyenu na mipango ya kuwaokoa wameru, acheni toilet politics, msiwe na akili za harakaharaka kama Majimarefu mnatia aibu.

  Pangu Pakavu.
   
 2. r

  rwazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umenena boss hawa jamaa wamefikia mwisho,hakuna kiongozi yeyote mwenye akili ccm.mkapa twambie kwanini ulimuua mwalimu
   
Loading...