CCM tukiendelea kuzuia mikutano ya kisiasa tuna wakati mgumu mbeleni

Ndiyo shida ya watu wasiojua siasa, ambao wanalishwa sumu ya uhasama. Siasa haina uadui, hebu muangalie Lowassa,Raila Odinga nk..

Kesho ukijakuona akina mbowe wako ikulu na Lissu anamimina juice huku wakicheka, sijui hiyo chuki yako itaingia wapi.
Mimi binafsi hata siku moja nikishakujua una chembechembe za uccm tayari ni adui yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ccm imefanya vizuri sana kuzuia mikutano hadi uchaguzi ukaribie hii itasaidia sana watu kutapika yote ya Miaka 4 na ccm watashindwa wajibu hoja IPI. Maana awajui upinzani watakuja na hoja zetu ili wao wajiandae kuzijibu. Aliempa ushauri wa kuzuia mikutano kawatendea vyema sana watz na hili litawachanganya sana ccm 2020 maana watashindwa wajibu hoja ipi ni nyingi watz wanataka majibu.
 
Ccm kuzuia mikutano ya kisiasa ni afya kwa upinzani mfano mpaka sasa hawajui upinzani watakuja na hoja na ajenda zipi ambapo wananchi wanangoja kwa hamu kupata majibu.2020 hawana uwezo wa kujibu hoja nyingi zilizotengenezwa na ccm.Watu watakapoanza kutapika watarusha makombora mazito ambayo sidhani kama ccm wataweza kuyajibu yote. Ccm wanashindwa kujua weakness ya upinzani iko wapi sababu wamewafunga mdomo kisiasa hii ni mbaya sana sababu ujui mshindani wako atakuja na hoja zipi. Kumbuka ccm imeshindwa kutimiza ahadi nyingi za 2015 mfano Milioni 50 kila kijiji,maslai bora kwa Watumishi, kuinua elimu.nk.Pia upinzani watulie wasubirie wakati wa kampeni ndio waanze kushusha makombora mazito watembelee mule mule kwenye waraka wa maaskofu na jumuia ya ulaya na hoja za Lissu ndio hoja kuu zinazosubiria majibu.
 
Tufanye wanachama wote tumepiga kura 2020 mana ndo mkakati uliopo hapo utatoka kwel kamanda

Sent using Jamii Forums mobile app


Kila Chama kuna kuwa na mkakati wa kuvuna kura za wapiga kura wapya wanaoingia ktk chaguzi kwa mara ya kwanza, ambao kimsingi si wote ni wanachama wa vyama vya Siasa.
Hamasa za chaguzi ndy huingiza wanachama MAKINI wapya baada ya chaguzi.

CCM ya leo si ile ya 2015., Ukweli ndiyo huo.
Jaribu kusikiliza/kusoma nn viongozi wao wakizungumza etc etc.
Haihitaji akili kubwa kuliona hilo.

Na pia hili la kurudi Nyumbani, kwa waliondoka 2015 ktk chama ni udhaifu tosha.

Chama kikubwa kingepambana kuzalisha vijana wapya kukiendeleza Chama, na kuachana na ya zamani.
Tatizo lipo!!

Vyama vingine vimepigwa Ban, isingekuwa hiyo Ban hapa saa hz tungezumza mengine.
Hii miaka 3 ingekuwa jibu kwako.
Time will tell.

Haipo mantiki yeyote ya kufanikisha wanachama wote kukipigia kura CCM.
 
Nadhan nimejariwa kuongea ukwel na kusimama kwenye kwel daima mana nimeiona nikiandika lile linahusu chama changu wanakuja MASHABIKI wa chama na kunishambulia kwa nguvu nyingi katika thread tofautitofauti ,Mfano thread iliyohusu kumjibu lissu kipind anatuchafua ughaibun kuwa apuuzwe,thread kuhusu suala la korosho kuwa tulichemsha na ikaja thread ya wasaidizi wa mh. rais kutuchosha watetezi wao mitandaoni mana kila siku wanaharibu.
Pia hata hiki nimekileta hapa watakuja tena MASHABIKI kunidhiaki bila kujua mimi ni mwana CCM penye kwel nitaongea kwel daima kwenye uongo nitakaa pembeni daima. Mana imetokea tabia nyie wasaka vyeo kuwa na haraka kuliko hata wenye imani na kijani katika damu ko lolote chama kikishauriwa nyie kazi yenu ni kumtolea kashfa anaetoa ushauri ambao hamtaupenda.
Turudi katika topic, Nadhan jana ilikuwa siku ya Wanawake duniani lakin katika pitapita zangu mitandaoni kuna khari ambayo niliona kule Geita jinsi Wanawake wa Bavicha walivyosherekea siku yao nikaona kwa hari hii kuna ugumu mbeleni mana pamoja na kuwekewa ngumu yote lakin walituonesha namna ambavyo wapo hai na kukataza mikutano yao kote bado nguvu wanayo.
Mana kiukwel wanawake wetu wa CCM walizidiwa pale katika kuufurahia siku yao nikaona kuna haja ya hii sera kuachana nayo ili wote tuwe huru ili tuwapime nguvu bila hivo hii sera itakuja ku backfire upand wetu mana tutabweteka kuwa tuna nguvu lakin hatujui waliyonayo watanzania mioyoni mwao inakuwa kama tunawalazimisha kutupenda wakat matendo ndo yafanye watupende.
Mimi ni muumini wa uwanja huru ili tucheze wote tushindane wote ili ijulikane nan mshindi katika hii michezo lakin upand mmoja ukiwa unacheza mwingine unaambiwa hamna kugusa mpira ingawa upo uwanjani hata mashabiki wa upand unaocheza wataona huu si mchezo bali wamepoteza viingilio vyao.



NB; CCM ina wenye chama na wanachama zingatia hilo kabla ya kuja kunitukana hapa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekukubali kiongozi, umeongea jambo LA msingi sana, ni vizuri hivi vyama vikashindana kwa hoja na sio kuyumia msaada wa poilisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom