CCM tukiendelea kuzuia mikutano ya kisiasa tuna wakati mgumu mbeleni

Hapo umenena mwanaccm mwenzangu. Ile ya Geita iwe ni somo tosha kwa ccm. Ukiangalia zile picha wanawake wa ccm utadhani wapo msibani jinsi walivyonywea na nyuso kuwa shuka. Kama unakimbia peke yako kila siku utajiona mshindi mpaka siku utakapokimbia na wenzako ndio utajua kuwa wewe si lolote.

CCM bila polisi hakuna kitu. Ukiitenga ccm na polisi basi imeshakufa. Sasa hicho ni chama gani kinachoishi kwa kushikiliwa na polisi kila siku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia mutakuwa na LUNDO la mambo ya KUJIBU maana yaliyotokea nchini yote yamewekwa KIPORO.
Mungeachia siasa huru,mungekuwa mumeshapropagate baadhi ya hoja,lakini safari hii,kama kinga yenu ni KUWATANDIKA watanzania wasio wajinga,basi kazi munayo.
 
Nadhan nimejariwa kuongea ukwel na kusimama kwenye kwel daima mana nimeiona nikiandika lile linahusu chama changu wanakuja MASHABIKI wa chama na kunishambulia kwa nguvu nyingi katika thread tofautitofauti ,Mfano thread iliyohusu kumjibu lissu kipind anatuchafua ughaibun kuwa apuuzwe,thread kuhusu suala la korosho kuwa tulichemsha na ikaja thread ya wasaidizi wa mh. rais kutuchosha watetezi wao mitandaoni mana kila siku wanaharibu.
Pia hata hiki nimekileta hapa watakuja tena MASHABIKI kunidhiaki bila kujua mimi ni mwana CCM penye kwel nitaongea kwel daima kwenye uongo nitakaa pembeni daima. Mana imetokea tabia nyie wasaka vyeo kuwa na haraka kuliko hata wenye imani na kijani katika damu ko lolote chama kikishauriwa nyie kazi yenu ni kumtolea kashfa anaetoa ushauri ambao hamtaupenda.
Turudi katika topic, Nadhan jana ilikuwa siku ya Wanawake duniani lakin katika pitapita zangu mitandaoni kuna khari ambayo niliona kule Geita jinsi Wanawake wa Bavicha walivyosherekea siku yao nikaona kwa hari hii kuna ugumu mbeleni mana pamoja na kuwekewa ngumu yote lakin walituonesha namna ambavyo wapo hai na kukataza mikutano yao kote bado nguvu wanayo.
Mana kiukwel wanawake wetu wa CCM walizidiwa pale katika kuufurahia siku yao nikaona kuna haja ya hii sera kuachana nayo ili wote tuwe huru ili tuwapime nguvu bila hivo hii sera itakuja ku backfire upand wetu mana tutabweteka kuwa tuna nguvu lakin hatujui waliyonayo watanzania mioyoni mwao inakuwa kama tunawalazimisha kutupenda wakat matendo ndo yafanye watupende.
Mimi ni muumini wa uwanja huru ili tucheze wote tushindane wote ili ijulikane nan mshindi katika hii michezo lakin upand mmoja ukiwa unacheza mwingine unaambiwa hamna kugusa mpira ingawa upo uwanjani hata mashabiki wa upand unaocheza wataona huu si mchezo bali wamepoteza viingilio vyao.



NB; CCM ina wenye chama na wanachama zingatia hilo kabla ya kuja kunitukana hapa.


Sent using Jamii Forums mobile app
kwa huu moto wa Lissu lazima CCM mtanena kwa lugha!
 
WAPINZANI WA NCHI HII NI WEPESI SANA SIJUI TUNAWAOGOPEA NIN WAKAT CHAMA KINA KILA MTU WA KUCHEZA VIZURI KATIKA NAFASI YAKE KO HAWAWEZ KUSHINDA KATIKA MECHI YA AINA YOYOTE ILE ILE MCHANGANI,CHAMANZI AU KWENYE NYASI NDANDATULA(kinyakyusa )

Sent using Jamii Forums mobile app

Una hakika wa hayo uliyosema ??

Umejaribu kutuaminisha kuwa ni mpenda ukweli na amani, daima unajitenga na UONGO.

Thibitisha kuwa CCM imeweza kushinda uchaguzi ulio huru na wa haki,

Kama unazungumzia ule ushindi wenye kutegemea msaada kutoka vyombo vya Dola,
Utaeleweka.
 
Una hakika wa hayo uliyosema ??

Umejaribu kutuaminisha kuwa ni mpenda ukweli na amani, daima unajitenga na UONGO.

Thibitisha kuwa CCM imeweza kushinda uchaguzi ulio huru na wa haki,

Kama unazungumzia ule ushindi wenye kutegemea msaada kutoka vyombo vya Dola,
Utaeleweka.
Nina uhakika chama kina wanachama million 15 kushindana na chama chenye wanachama million 3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa utawala huu ambao ccm mikutano yes, wapinzani no, na vile vile tuliambiwa hakuna mikutano watu wafanye kazi, sasa hizi kazi zinafanywa na upinzani tu ccm wao hawafanyi kazi
 
Back
Top Bottom