CCM tuambiane ukweli: Ushindi wetu wa 2020 haunogi kabisa. Tunatokaje hapa?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Raha ya ushindi ni kunoga kwake. Raha ya uchaguzi ni kushinda halafu kutamba kama mwenye magamba membamba. Kunyakua kiti cha Urais; viti vya Ubunge na Udiwani kufuatiwe na 'utamu' wa kidemokrasia.

Kati ya mihimili ya dola iliyopo: Serikali, Bunge na Mahakama, Bunge ndiyo uwanja wa kisiasa hasa. Ndipo mshindi wa uchaguzi mkuu anapojitamba na kuonekana akitamba. Anatamba kwa wingi wake; hoja zake na mbwembwe zake nyinginezo.

Bunge hili ni tofauti. Wananchi hawaamini hata lilivyopatikana (wanatilia shaka uhalali wa kura na mchakato wa kuwapata Wabunge). Uwiano uliopo kati ya CCM na vyama vya upinzani Bungeni unatunyima kama chama kutamba na kufurahia ushindi wetu uchaguzini. Tutambe nini ikiwa Bunge 'zima' ni CCM watupu?

Watanzania walio wengi kwasasa hawalifuatilii Bunge kwenye vikao vyake na mijadala yake. Wamelipuuza na kulipotezea. Wanawatazama Wabunge kama wanavyowatazama wajumbe wa NEC au KK ya CCM wanapokutana hukohuko Dodoma. Hakika, Bunge hili ni kama kikao cha CCM.

Ushindi wetu wa 2020 haunogi kabisa. Tumepata lakini tumekwama. Tunatokaje hapo?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Naona mleta mada umerudi hewani baada ya kupotea muda nrefu ukiuguza maumivu ya Lisu kushindwa uraisi na Chadema kukosa wabunge umeugulia wee naona unajikongoja kurudi hewani
Na Membe baada ya kutemwa ndo kabisaaaaa maana akijifanya mpiga debe wa Membe.
 
Mmewakosea sana wale CCM wenzenu walioshinda kihalali kwenye ule uchaguzi, sasa nao wanaonekana hawana maana.
 
Naona mleta mada umerudi hewani baada ya kupotea muda nrefu ukiuguza maumivu ya Lisu kushindwa uraisi na Chadema kukosa wabunge umeugulia wee naona unajikongoja kurudi hewani
Na Membe baada ya kutemwa ndo kabisaaaaa maana akijifanya mpiga debe wa Membe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vichwa maji mmeambiwa ukweli acheni kelele, mlidhani mkiiba ndio utakuwa mwisho wenu kumbe mmejitengenezea aibu inayowatafuna kila siku.
 
Naona mleta mada umerudi hewani baada ya kupotea muda nrefu ukiuguza maumivu ya Lisu kushindwa uraisi na Chadema kukosa wabunge umeugulia wee naona unajikongoja kurudi hewani
CCM ya sasa ni genge fulani hivi lenye sifa za ajabu ajabu!
 
Umesema kweli. Bahati mbaya walio karibu na "MUNANGWA" ni wenye kusifu na kuabudu.

Ukweli ni kuwa Ccm ilipora ushindi. Na daima mali ya uporaji haunogi kama mali ya kuvuja jasho.

Tatizo naliona kwa vyombo vyetu vya kusimamia haki na utawala bora . Bado havitajatengwa na Ccm. Bado viongozi wa vyombo hivyo ni watiifu kwa Ccm hata kwa kuhalalisha vya haramu.
 
CCM ni kundi la magaidi kama ISS. Huwezi kufanya uchafu walioufanya katika uchaguzi uliopit ukasema hicho ni chama cha siasa. Hilo ni kundi la kigaidi sawa na ISS kinachowatofautisha na ISS ni areas of operations ni tofauti na modes of operation
"Modus Operandi". Nimeipenda hii!.
 
Back
Top Bottom