CCM tuachie madaraka kwa amani

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,034
28,201
Najitolea kuwa mwanaccm wa kwanza kuwaasa wanaccm wenzangu hasa vijana wakiongozwa na Nape,Makamba na Mchemba.

Nianze kwa kusema kuwa CCM imekuwa chama makini kwa muda mrefu,umakini wa ccm umetambulika kitaifa na kimataifa hivyo ni muhimu kulinda heshima hii.

Kwa miaka ya karibuni ni busara kukubali kuwa chama chetu kimeingiliwa na mafisadi na hasa wafanyabiashara ambao wamesababisha chama kuwatupa waasisi na wafuasi wake watiifu kama vile wakulima na wafanyakazi.hiki ndio chanzo cha chuki dhidi yetu kutoka kwa raia,wapinzani wetu wametumia kosa hili na wakaweza kukumbatia maslahi ya waasisi na wafuasi asili wa ccm.

Chama kimeshindwa kulea makada kuanzia ngazi ya chini na badala yake kimeendekeza udugu na ufalme.

Chama kimeruhusu mafisadi kuamua na kutenda dhidi ya misingi na matakwa ya wajamaa walioanzisha na kuilea ccm.

Chama hakina kiongozi mwenye kauli ya mwisho,kwa ufupi tumeacha chama mikononi mwa waropokaji.

Tumetengeneza matabaka kiasi kwamba maamuzi yanatoka juu kuja chini na sio chini kwenda juu.

Maoni na ushauri wangu ni kuwa ni lazima tukae chini na kuangalia kwa nini haya yametokea na tufanye nini.

Kushindwa uchaguzi na kupoteza hatamu ya kushika dola ni jambo la kawaida sana kwenye siasa.hivyo ni vyema tukahakikisha kuwa mabadiliko ya kiutawala nchini yanatokea kwa amani ili kuiweka taswira safi ya chama na taifa kwa ujumla.

Tuiache chadema ishike nchi kama tulivyokubali kuingiza siasa za vyama vingi nchini.

Sipendi kuona machafuko ya kisiasa chini ya utawala wa ccm.

Sijaridhika na mwenendo wa chama kwani yale tunayokubaliana kwenye vikao halali vya chama hayatekelezwi na badala yake watu binafsi wanaibuka na hoja zao ambazo zinatuacha kama vituko mitaani.

Bado hatujajibu hoja za msingi kama vile kwa nini wale wanaoitwa mafisadi hawajachukuliwa hatua,hapa namtaja chenge na lowassa na badala yake wanaendelea kuogopewa na kupewa nyadhifa chamani.

Kama tumeshindwa kujibu hoja kuu ya upinzani kamwe tusitarajie kupendwa.

Mwisho nitoe rai kwa wanaccm wa zamani tukutane na kukirudisha chama katika misingi yake ya awali.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
CCM iachie madaraka kwani walishashindwa uchaguzi?

Chama
Monga vyeru

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Ukweli lazima usemwe ilikujisahihisha, bahati mbaya mkuu chama chenu ni kama sikio la kufa daima halisikii dawa.
 
Ukweli lazima usemwe ilikujisahihisha, bahati mbaya mkuu chama chenu ni kama sikio la kufa daima halisikii dawa.

doa la ccm ni moja tu,tukilisafisha hili hata kwa gharama yoyote tutashinda uchaguzi kwa kishindo.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Naungana na wewe asilimia mia..........

Naongeza hali,

Waliokiteka chama wakiachie wenye mioyo safi wakiendeshe.
 
doa la ccm ni moja tu,tukilisafisha hili hata kwa gharama yoyote tutashinda uchaguzi kwa kishindo.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Mkuu doa gani hilo moja? mbona mengi mpka ragi ya chama imevurugika!
 
Mkuu doa gani hilo moja? mbona mengi mpka ragi ya chama imevurugika!
doa ni kukumbatia wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi.hii ndiyo hoja kuu walitosimamia chadema toka 2005 mpaka leo.ndiyo hoja iliyoipa chadema nguvu 2010 na ndio hoja itakayotuondoa madarakani 2015.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
doa ni kukumbatia wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi.hii ndiyo hoja kuu walitosimamia chadema toka 2005 mpaka leo.ndiyo hoja iliyoipa chadema nguvu 2010 na ndio hoja itakayotuondoa madarakani 2015.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Nimekubali mkuu upo sahihi, kumbe mengine ni madogomadogo, je mtafanikiwa mkuu kuwaondoa mafisadi maana kuanzia ikulu kuja

kwa fisadi wa meno ya tembo, wazee wa Richmond, Rada nk mbona msitu wenyenye ni hatari na unatisha. Nani atenda ikulu

kumvisha paka kengele????
 
Najitolea kuwa mwanaccm wa kwanza kuwaasa wanaccm wenzangu hasa vijana wakiongozwa na Nape,Makamba na Mchemba.

Nianze kwa kusema kuwa CCM imekuwa chama makini kwa muda mrefu,umakini wa ccm umetambulika kitaifa na kimataifa hivyo ni muhimu kulinda heshima hii.

Kwa miaka ya karibuni ni busara kukubali kuwa chama chetu kimeingiliwa na mafisadi na hasa wafanyabiashara ambao wamesababisha chama kuwatupa waasisi na wafuasi wake watiifu kama vile wakulima na wafanyakazi.hiki ndio chanzo cha chuki dhidi yetu kutoka kwa raia,wapinzani wetu wametumia kosa hili na wakaweza kukumbatia maslahi ya waasisi na wafuasi asili wa ccm.

Chama kimeshindwa kulea makada kuanzia ngazi ya chini na badala yake kimeendekeza udugu na ufalme.

Chama kimeruhusu mafisadi kuamua na kutenda dhidi ya misingi na matakwa ya wajamaa walioanzisha na kuilea ccm.

Chama hakina kiongozi mwenye kauli ya mwisho,kwa ufupi tumeacha chama mikononi mwa waropokaji.

Tumetengeneza matabaka kiasi kwamba maamuzi yanatoka juu kuja chini na sio chini kwenda juu.

Maoni na ushauri wangu ni kuwa ni lazima tukae chini na kuangalia kwa nini haya yametokea na tufanye nini.

Kushindwa uchaguzi na kupoteza hatamu ya kushika dola ni jambo la kawaida sana kwenye siasa.hivyo ni vyema tukahakikisha kuwa mabadiliko ya kiutawala nchini yanatokea kwa amani ili kuiweka taswira safi ya chama na taifa kwa ujumla.

Tuiache chadema ishike nchi kama tulivyokubali kuingiza siasa za vyama vingi nchini.

Sipendi kuona machafuko ya kisiasa chini ya utawala wa ccm.

Sijaridhika na mwenendo wa chama kwani yale tunayokubaliana kwenye vikao halali vya chama hayatekelezwi na badala yake watu binafsi wanaibuka na hoja zao ambazo zinatuacha kama vituko mitaani.

Bado hatujajibu hoja za msingi kama vile kwa nini wale wanaoitwa mafisadi hawajachukuliwa hatua,hapa namtaja chenge na lowassa na badala yake wanaendelea kuogopewa na kupewa nyadhifa chamani.

Kama tumeshindwa kujibu hoja kuu ya upinzani kamwe tusitarajie kupendwa.

Mwisho nitoe rai kwa wanaccm wa zamani tukutane na kukirudisha chama katika misingi yake ya awali.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

tatizo washalewa madaraka hawawezi kukuelewa tena,hapo kutatua matatizo ya jamii iliyowaweka madarakani rather most of their efforts inaelekezwa katika mikakati na mbinu chafu za kushinda uchaguzi mkuu ujao,lengo lao kuu nikuhakikisha nchi hii inakabidhiwa kwa mwanaccm mwingine 2015 kwa gharama yoyote ile.
 
Thubutu wajaribu kulazimisha kunyamazisha wananchi kwa kuwaua kutumia polisi na usalama walinda wizi. kama The Hague haijawavuta.
 
Mkuu umesema vyema, ni vizuri ccm wakawaachia wananchi wa tanzania waamue nani wa kuwaongoza kupitia sanduku la kura,vingevyo ccm watalivuruga taifa letu na kuliacha vipande vipande kwa tamaa ya madaraka. Maslahi ya taifa kwanza,vyama baadae.
 
Thubutu CCM wakubali kuachia madaraka kirahisi namna hiyo, viongozi wake wana kutu mioyoni mwao, hata hawaifeel tabu ya wananchi, ukiwaona machoni kama watu mioyoni mwao wanachowaza khs wa TZ anajua Mungu.

CCM kuondoa ufisadi haiwezi na haitakuja kuweza sababu ni nyingi lakini kubwa ni hii, watamuondoa nani wamuache nani, si munakumbuka LOWASA alivyomkazia Mheshimiwa Mkuu kule dodoma "ni kipi nilichofanya ambacho wewe hukijui" sasa huyo ni mmoja, bado jairo, chenge na wengine kibao CCM ni janga, kukabiliana nayo inabidi kila mpenda NCHI hii awe na moyo kama wa SLAA, sio siasa za kinafiki kama za NAPE.
 
CCM iachie madaraka kwani walishashindwa uchaguzi?

Chama
Monga vyeru

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Inaelekea una matatizo ya kufikiri,ndio maana unaona kuwa na blackberry ni jambo la kujivunia.Muwakilishaji mada amejieleza vizuri sana.Kwa mtu mwenye nia njema na nchi yetu, hoja yake na nini CCM inapaswa kufanya ni wazi.Nani hajui kwamba CCM inashinda uchaguzi kwa wizi wa kura?CCM iache wizi wa kura,anayeshinda uchaguzi aachiwe kuitawala nchi.Tamko la CHADEMA kwamba CCM wakiiba kura wataingia msituni ili kuwakomboa Watanzania kutoka kwenye uonevu wa CCM ni la hatari sana.Kama CCM isipokuwa makini, itaiingiza nchi yetu katika matatizo makubwa sana.
 
Doa sio moja labda wewe madoa mengine huyaoni kwa makusudi au upofu: Rushwa kwenye uongozi, serikalini, Bungeni hata Mahakamani. Undungunaizesheni, Wizi wa mali za umma, Usimamizi mbovu wa huduma za jami mahospitalini shule, vyuoni na vyuo vikuu. Tazama gazeti la uhuru la leo Ukahaba vyuo vikuu. Ni matokeo ya sera mbovu za CCM. Ndugu yangu yapo madoa mengi kuzidi hata ya Chui. Sijui utaondoa doa lipi uliache lipi ili Chui awe na rangi ipi. Najua unayaona yote haya ila unatamani kuyapuuza. Usifanye hivyo.
doa ni kukumbatia wale wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi.hii ndiyo hoja kuu walitosimamia chadema toka 2005 mpaka leo.ndiyo hoja iliyoipa chadema nguvu 2010 na ndio hoja itakayotuondoa madarakani 2015.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
"Mtu akianza kula nyama za watu, ataendelea kuila tu! Hataiacha dhambi hii mpaka dhambi hiyo itakapo mtafuna na naomba Mungu dhambi hii imtafune." Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, 1995.
Inaelekea una matatizo ya kufikiri.Muwakilishaji mada amejieleza vizuri sana.Kwa mtu mwenye nia njema na nchi yetu hoja yake na nini CCM inapaswa kufanya ni wazi.Nani hajui kwamba CCM inashinda uchaguzi kwa wizi wa kura?CCM iache wizi wa kura,anayeshinda uchaguzi aachiwe kuitawala nchi.Tamko la CHADEMA ni la hatari sana,na kama CCM isipokuwa makini itaiingiza nchi yetu katika matatizo makubwa sana.
 
lema kuachiwa ubunge wake ni mojawapo ya mambo inayotakiwa kuyafanya ccm kwa sasa!amani itawale.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
hapo mjomba umenena ya kweli, samahani lakini maana mi naona hii ni kama ndoto sababu sipati picha ccm ikiachia ngazi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom