jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
Najitolea kuwa mwanaccm wa kwanza kuwaasa wanaccm wenzangu hasa vijana wakiongozwa na Nape,Makamba na Mchemba.
Nianze kwa kusema kuwa CCM imekuwa chama makini kwa muda mrefu,umakini wa ccm umetambulika kitaifa na kimataifa hivyo ni muhimu kulinda heshima hii.
Kwa miaka ya karibuni ni busara kukubali kuwa chama chetu kimeingiliwa na mafisadi na hasa wafanyabiashara ambao wamesababisha chama kuwatupa waasisi na wafuasi wake watiifu kama vile wakulima na wafanyakazi.hiki ndio chanzo cha chuki dhidi yetu kutoka kwa raia,wapinzani wetu wametumia kosa hili na wakaweza kukumbatia maslahi ya waasisi na wafuasi asili wa ccm.
Chama kimeshindwa kulea makada kuanzia ngazi ya chini na badala yake kimeendekeza udugu na ufalme.
Chama kimeruhusu mafisadi kuamua na kutenda dhidi ya misingi na matakwa ya wajamaa walioanzisha na kuilea ccm.
Chama hakina kiongozi mwenye kauli ya mwisho,kwa ufupi tumeacha chama mikononi mwa waropokaji.
Tumetengeneza matabaka kiasi kwamba maamuzi yanatoka juu kuja chini na sio chini kwenda juu.
Maoni na ushauri wangu ni kuwa ni lazima tukae chini na kuangalia kwa nini haya yametokea na tufanye nini.
Kushindwa uchaguzi na kupoteza hatamu ya kushika dola ni jambo la kawaida sana kwenye siasa.hivyo ni vyema tukahakikisha kuwa mabadiliko ya kiutawala nchini yanatokea kwa amani ili kuiweka taswira safi ya chama na taifa kwa ujumla.
Tuiache chadema ishike nchi kama tulivyokubali kuingiza siasa za vyama vingi nchini.
Sipendi kuona machafuko ya kisiasa chini ya utawala wa ccm.
Sijaridhika na mwenendo wa chama kwani yale tunayokubaliana kwenye vikao halali vya chama hayatekelezwi na badala yake watu binafsi wanaibuka na hoja zao ambazo zinatuacha kama vituko mitaani.
Bado hatujajibu hoja za msingi kama vile kwa nini wale wanaoitwa mafisadi hawajachukuliwa hatua,hapa namtaja chenge na lowassa na badala yake wanaendelea kuogopewa na kupewa nyadhifa chamani.
Kama tumeshindwa kujibu hoja kuu ya upinzani kamwe tusitarajie kupendwa.
Mwisho nitoe rai kwa wanaccm wa zamani tukutane na kukirudisha chama katika misingi yake ya awali.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA