CCM toeni majibu ya mambo haya kabla ya 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM toeni majibu ya mambo haya kabla ya 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kavulata, Aug 13, 2012.

 1. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,207
  Likes Received: 1,564
  Trophy Points: 280
  Naipongeza CCM kwa kuingoza nchi hadi kufikia leo, hakuna ubishi kuwa CCM huwezi kuitenganisha na kila kilichofanyika na ambacho hakikufanyika ndani ya taifa letu kiwe kizuri ama kibaya kwakuwa CCM ndico chama iliyokuwepo madarakani tangu kupata uhuru. 2015 kuna uchaguzi mkuu naomba CCM mchague mtu ambaye atasaidiana na chama na serikali kujibu maswali yafuatayo:

  Pamoja na barabara, shule, amani (utulivu), lugha ya kiswahili na uhuru wa kuabudu:

  1. Kwanini kuna migomo mingi ya wafanyakazi?
  2. Mifuniko ya septic tanks barabarani, mafuta ya transfoma za Tanesco, vyuma vya madaraja vinaiibwa na Nani na kwanini?
  3. Wakinamama na watoto wengi nchini wanakufa kwanini?
  4. Ajali za barabarani na majini zinasababishwa na nani na kwanini?
  5. Vijana wanakimbilia mijini kwanini?
  5. Kwanini kitivo cha uhandisi na wahandisi wanaohitimu toka vyuo vyetu hawawezi kutengeneza japo trekta moja likatembea barabari?
  6. Vijana wetu wanafanyia biashara zao popote hata pasiporuhusiwa kwanini?
  7. Wananchi karibu wote hawana maji ya uhakika kwanini?
  8. Watu wanajisaidia na kutupa taka popote kwanini?
  9. Muungano unalalamikiwa na nani na kwanini?
  10. Wanafunzi wanafeli sana mitihani yao ya NECTA kwanini?
  11. Shilingi yetu inashuka thamani kwanini?
  12. Idadi ya walipa kodi nchini ni ndogo kwani?
  13. Miji yetu imejengwa kiholela kwanini?
  14. Wakulima na wafugaji wanalima na kufuga kiholeta hadi leo kwanini?
  15. Nani na kwanini kuna watoa na wapokea rushwa wengi nchini?

  Haya ndio maswali ya mtu wa kawaida kama mimi Kavulata ambayo mwaka 2015 ningependa kukiuliza CCM na Serikali yake kabla sijaipa mamlaka ya kuniongoza tena. CCM amefanya au haikufanya nini hadi maswali kama haya yakajitokeza?

  Pia ni maswali ambayo chama kinachoomba ridhaa ya kuiongoza nchi ningependa kiwe na uwezo wa kunieleza kwa ufasahasa namna/mbinu kitakachozitumia zilizotofauti na za CCM kuifanya hali iwe tofauti na ilivyo sasa punde kiingiapo madarakani.

  Uzoefu unaonyesha hata vyama pinzani hawana mbinu mpya punde waingiapo madarakani, hali inabaki ileile ama hafifu zaidi. Naangalia mifano ya vyama pinzani barani Afrika vilivyofanikiwa kushika madaraka na hali ikabaki vile vile, mfano, Kenya, Zambia, Malawi, Nigeria, Ghana, Liberia, DR Congo, Uganda, n.k.

  Tujiulize tatizo ni nini, CCM, wananchi wenyewe, serikali, mataifa ya nje, rasilimali zetu, sheria zetu, waalimu wetu?
   
 2. Ngangasyonga

  Ngangasyonga JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2010
  Messages: 456
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  16. Kwa nini huduma za afya zimezorota?? wao wakiumwa kidogo tu haoo Apollo kutibiwa
  17. Kwa nini watoto wao hawasomi shule za serikali????
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​sababu kiongozi wao mkuu ni dhaifu saana
   
 4. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  18. Kwanini fedha za nchi zimetoroshewa uswis na ccm iko kimya 19. Kwa nini wafanyabiadhara wakubwa hawalipi kodi
   
 5. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Hwawezi kuleta majibi ya mambo yalowashinda kwa miaka hamsini. Wataishia kukutukana tu!
   
 6. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  20 kwnini mafisadi hawakamatwi na kufikishwa mahakamani 21 kwanini jei kei anasafiri bila sababu za msingi

  endeleeni wakuu mi napata mbege
   
 7. m

  majebere JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Maswali ya kumuuliza yesu unauliza ccm kweli wewe ni bogus kabisa.
   
 8. m

  majebere JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Mtu kunya porini ni kosa la ccm?
  Mtoto kutokuwa na akili ya elimu ni kosa la ccm?
  Watu kufa ni kosa la ccm?
  Wabongo kuwa wizi ni kosa la ccm?
  Watu kuomba ruswa ni kosa la ccm?
  Ndio maana nikakwambia maswali ya kuuliza mitume unauliza chama.
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hebu nieleze Slaa atatumia mbinu gani ya kumzuia mtu kunya kichakani? Nimepitia sera ya CDM na sijaona sehemu inayo zungumzia hili swala.
   
 10. M

  MKATA UFUTA Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You need to think deep and critically. JF ni jukwaa la Weledi.
   
 11. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Huko gizani ndugu,kumbe haujui kuwa serikali ni mojawapo wa kitu kinacho iandaa jamii {socialisation and civilisation
  ]
   
 12. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,480
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu CCM inahusika kwa majibu yafuatayo
  1. KUNYA POLINI - Hii ni kutokana na watu wengi kuto kusoma na umasikini wa kushindwa kuchimba na kujenga vyoo, pia sababu nyingine ni upindishwaji wa sheria kwani mabwana afya wetu wanapochukua hatua juu ya hili baadhi ya viongozi wa CCM hutoa amri waachwe kwani ni wapiga kura wao.

  2. MTOTO KUTO KUWA NA AKILI - Hili unatakiwa ujue lishe bora umjenga mtoto kiakili na kimwili sasa kama lishe ni duni unategemea nini na hii inatokana na CCM kusababisha maisha kuwa magumu.

  3. WATU KUFA - Hili unatakiwa ujue Serikali ina jukumu la kulinda watu wake wasife kwa kuzuia ajali za barabarani pamoja na Tiba na kinga za magonjwa.mbona ulaya vifo ni vichache?

  4. WABONGO KUWA WIZI - Hili linasababishwa na serikali ya CCM kwani hadi leo wezi wangapi wa mali ya umma hususani wanasiasa wameisha fungwa?

  5. RUSHWA - Pia ni la CCM kwani tumeona mikataba mikubwa ilivyo na dosari na hadi mingine inaenda kusainiwa Nje ya nchi, hivyo hii inaonyesha Rushwa ni halali ndani ya Utawala wa CCM

  Kwa hiyo ndugu yangu Mitume haiihusiki ni CCM inahusika kutuondelea haya.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii kwa Dar utaikuta kwa wachaga wa gerezani na tabata!
   
 14. t

  thatha JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kuna mtoto wa kiongozi wa chama gani cha Siasa anasoma shule za Serikali? sasa hao wakishika nchi si ndo itakuwa zaidi?
   
 15. t

  thatha JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Safi sana Mkuu, kumbe na wewe unajua, sasa yule mmafia wao akishika nchi itahamishiwa Hai kabisaaaa. teh teh teh
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hakuna nafuu ya chama chochote.
  Rushwa haina chama, kabila wala dini (JOSEPH SELASINI).
  Mimi naona kama ulichokiandika hapo pumba tupu.
  Ni bora watanzania wote wakawa wala rushwa kuliko, kabila moja kuandaliwa kuwa wala rushwa wa baadaye.
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Chemsha ubongo wako, usiwe mchango mwepesi kama mnywa mbege hivyo. Elezea utawandawazi, mabadiliko ya tabia nchi na mtikisiko wa uchumi duniani unavyoathiri maendeleo hasa ya nchi za dunia ya tatu, siyo kuropoka 2.
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Unajua bwana Majebere watu kama hao hawana hoja ya msingi wanachokiuliza ni kile 2 ambacho wanasikia wanasiasa wanaongea majukwaani. Wanashindwa kuelewa kuwa manasiasa siku zote anatafuta umaarufu tu na hana lolote.

  Mimi nafikiri maswali kama hayo wangekuwa wanawauliza wafuasi wa vyama vyao wanavyoweza kuyashughulikia waone watakavyojikanyaga.

  CCM inamwambia mwanachi ajisaidie porini? teh teh teh, kweli sasa CDM wanaelekea kuwaongoza watanzania waliolishwa uongo hadi vichwa vikalala. Nadhani hivi sasa MBOWE akisema mchango si pesa bali kila mnazi wa CDM aje na mke wake na amwache kwangu wataitikia PEEEEEEEEPLES.
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ni kweli JF ni jukwaa la weledi na bwana Majebere yuko sahihi kabisa unajua kuna thread zingine zinarushwa humu JF as if wanaochangia ni wale watu wa vijijini ambao wakiona helcopter za wanasiasa wanazikimbilia na akitoka kwenye mkutano ukamuuliza kilichosemwa atakwambia MBOWE alishuka kikakamavu na magwanda , teh teh teh. Big up bwana majebere.
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Naona unasikiliza sana bunge ni kama ume-pick kero ambazo Mawaziri wamezielezea kwenye hotuba zao za bajeti na kuahidi kuzishughulikia. Endelea kujifunza utaimarika kimawazo.
   
Loading...