ngalelefijo
JF-Expert Member
- Jun 26, 2012
- 3,709
- 2,272
Sorry, wewe ni ccm? Nijibu niunganishe dotSasa narudi kwako mkuu.
Toka hata kabla ya uhuru, rais aliyetembelea vyema hadi vijijini huko Mbeya ni Mwalimu.
Mwalimu ana kumbukwa hata alipotembelea kijijini kwetu Mpuguso kabla ya uhuru.
Babu yangu ananihadithia jinsi alipoenda kuongea na wanafunzi, wananchi na machifu pale Mpuguso.
Na Mwalimu alishiriki kula kyindi, ugali wa dona pamoja na babu yangu pale shuleni, middle school Mpuguso.
Baada ya uhuru, Mwalimu alihakikisha barabara ya Tanzania ~Zambia, ile ya Malawi zinajengwa.
Viwanda vya chai, hasa kile cha Katumba, kiwanda cha Zana Za Kilimo~Iyunga, Kiwanda cha nguo Songwe, Kiwanda cha simenti na viwanda vingi vidogo vidogo.
Vyote alileta Mwalimu.
Na hilo maana yake ajira.
Hebu nijulishe Allen Kilewella, Mwinyi alitufanyia nini?
Nothing, pamoja na ahadi kedekede.
Mkapa je?
Yeye ndo akaviuza kabisa hata vile viwanda vichache, na ajira kwishney.
Si mbaya sana kwa vile hili lilikuwa tatizo la nchi nzima.
Vijana wakaanza kuwa disilludioned, CCM ILIANZA taratibu kukosa unaarufu.
Nyerere hayupo tena!
Mwandosya akaonekana kuwa hope, maana alipokuwa waziri wa Uchukuzi ingalau alishawishi serikali kujenga uwanja mpya wa ndege Songwe.
That was a spark of hope.
KOSA!
Mwandosya kugombea urais!
Hapo all hell broke loose.
JK na mtandao walirusha kila aina ya dongo, mara mtoto wake kasomeshwa na makumpuni ya simu.
Mwisho mtandso wakaona waivuruge kabisa base ya huyu Prof.
Na base hiyo ni CCM Mbeya.
The rest you know.
Lakini tunafarijika maana licha ya vijana wa CHADEMA kumfanyia fujo JPM, yeye haangalii hilo, kaonyesha kwa vitendo MAENDELEO HAYANA VYAMA.
Sent using Jamii Forums mobile app